baadhi ya wapiganaji wa Boko haram wakiwa 'kamili' na zana zao |
ABUJA, Nigeria
ZAIDI ya wanamgambo 300 wa kundi la Boko Haram wameuawa katika zoezi la
kijeshi huko Kaskazini-Mashariki ya Nigeria, limesema jeshi la Nigeria.
Baadhi ya askari wamekamatwa na silaha kadhaa zimeharibiwa, alisema
msemaji wa jeshi hilo, Chris Olukolade.
Pia katika tukio hilo askari wawili walipoteza maisha yao na
wengine 10 walijeruhiwa wakati wa zoezi hilo la siku mbili huko katika jimbo la
Borno, aliongeza.
Hatahivyo, vifo hivyo havijathibitishwa.
Jeshi la Nigeria lilituhumiwa katika siku zilizopita kuwa limekuwa
likitoa taarifa za uongo kuhusu kujeruhiwa kwa maadui.
Boko Haram wamevamia raia huku wakiwaua maelfu wa askari tangu
kundi hilo lianzishe vurugu kwa ajili ya kuanzisha taifa lao la kiislamu mwaka 2008.
Nigeria, Chad, Cameroon na Niger hivi karibuni vimeunda jeshi la
muungano na kudai kuwa limekuwa likifanya vizuri dhidi ya Boko Haramu.
Tisho la kundi hilo linaelezwa ndiyo sababu ya kuahirishwa kwa Uchaguzi Mkuu wa nchini huo uliokuwa ufanyike Jumamosi iliyopita na kupelekwa mbele hadi majuma sita yaani Machi 28.
No comments:
Post a Comment