Rais wa FIFA, Sepp Blatter aliyekerwa na kitendo chga kibaguzi kilichofanywa na amshabiki wa Chelsea dhidi ya mtu mweusi mjini Paris. |
PARIS, Ufaransa
RAIS wa Shirikisho la Kimataifa la Soka Sepp Blatter amewalaumu
mashabiki wa klabu ya Chelsea, kwa kitendo chao cha kumzuia mtu mweusi kuingia ndani ya treni
huku wakiimba nyimbo za kibaguzi jijini hapa.
Blatter amelaaini kitendo hicho kilichofanywa na baadhi ya mashabiki
hao wa Chelsea cha ubaguzi wa rangi dhidi ya mtu huyo mweusi na kumzuia kuingia
katika treni jana Jumanne.
Baadhi ya mashabiki wa Chelsea wameonekana katika mkanda wa video
wakizuia mlango wa treni kabla hawajamsukuma mtu huyo huku wakiimba nyimbo za
kibaguzi:
"Sisi wabaguzi, sisi wabaguzi na hicho ndicho tunachokitaka."
Tukio hilo lilitokea baada ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya
uliofanyika jijini hapa na Chelsea kutoka sare ya kufungana bao 1-1 na Paris
Saint-Germain kwenye uwanja wa Parc des Princes, huku klabu hiyo ikijibu haraka
kuwa kitendo hicho sio cha kiungwana.
Ni wiki moja tu baada ya kocha wa zamani wa AC Milan Milan Arrigo
Sacchi kutoa kauli kuwa "kuna weusi wengi" katika ligi ya vijana ya
Italia, ambapo Blatter akijibu matukio yote hayo katika mtanda wake wa kijamii
wa Twitter.
Matukio ya kibaguzi katika michezo yamekuwa kama ugonjwa sugu, huku adhabu dhidi ya wahusika yakielezwa kuruhusu kuendelea kuyahamasisha.
No comments:
Post a Comment