LICHA ya kiungo klabu ya
Chelsea Nemanja Matic amepunguziwa adhabu yake kutoka mechi tatu mpaka
mbili lakini bado anatarajiwa kukosa mchezo fainali ya Kombe la Ligi
Jumapili hii.
Chama cha Soka cha Uingereza-FA kiliamua kupunguza adhabu
hiyo baada ya kuridhishwa na utetezi uliotolewa na Chelsea.
Matic mwenye
umri wa miaka 26 alitolewa nje Jumamosi iliyopita wakati Chelsea
walipotoa sare ya bao 1-1 dhidi ya Burnley baada ya kumchezea vibaya
Ashley Barnes.
Katika taarifa yake, klabu hiyo imedai kushtushwa na
kusikitishwa kuwa Matic bado atatakiwa kutumikia adhabu.
Matic sasa
atakosa mchezo wa fainali wa Kombe la Ligi dhidi ya Tottenham Hotspurs
ambao utafanyika katika Uwanja wa Wembley na mchezo mwingine dhidi ya
West Ham United utakaochezwa Machi 4.
No comments:
Post a Comment