Picha ya baadhi za vurugu za soka nchini Misri |
CAIRO, Misri
LIGI Kuu ya Misri ambayo ilisimamishwa, itaendelea tena
mwezi ujao lakini bila ya kuruhusiwa mashabiki kuishuhudia michezo hiyo kutokana na kukithiri kwa matukio ya vurugu yaliyoleta maafa ya mashabiki hivi karibuni.
Ligi hiyo ilisimamishwa baada ya kutokea vurugu
uwanjani na kuua watu karibu 19 kutokana na vurugu hizo za mashabiki na polisi
nje ya uwanja jijini hapa Februari 8 mwaka huu.
Baada ya kikao cha Jumatano, Baraza la Mawaziri la
Misri katika taarifa yake lilisema kuwa, ligi inaweza kuendelea "bila ya
mashabiki baada ya kumalizika kwa siku 40 za maombolezo ".
Hata hivyo, taarifa hiyo haikusema bayana ni lini hasa
ligi hiyo itaanza kuchezwa huku mashabiki wakizuiwa kushuhudia mechi hizo.
Maafa hayo yalitokea kabla ya mchezo kati ya klabu za jijini
hapa ya Zamalek na ENPPI wakati polisi na mashabiki walipopambana.
Polisi walilipua mabomu ya machizo na kurusha silaha
nyingine kwa mashabiki hao, ambao walikuwa wakilazimisha kuingia uwanjani
kushuhudia pambano hilo.
Hiyo iliuwa ni mara ya kwanza kwa idadi maalum ya
mashabiki kuruhusiwa kuingia uwanjani kushuhudia mechi za ligi tangu Februari
2012, wakati mashabiki 72 wa Al Ahly walipokufa walipokuwa wakipambana na
wenzao wa Al Masry kwenye uwanja wa Port Said.
No comments:
Post a Comment