Na AFISA HABARI WA TAZARA
DEREVA wa treni ya mizingo ya Mamlaka ya
Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara) Ali Kilumanga (57), amefariki dunia
huku askari 10 wa jeshi la Polisi nchini
wakinusurika kifo kwenye ajali ya
treni iliyotokea karibu na stesheni ya Makambako
mkoani Iringa.
Mkurugenzi
Mtendaji wa TAZARA, Akashambatwa
Mbikusita-Lewanika aliwaambia waandIshi wa habari jijini Dar es Salaam
jana kuwa ajali hiyo ilitokea juzi saa 11:40 jioni na kuhusisha Treni No
0755
ya shirika hilo, iliyokuwa ikiokea Dar es salaam kwenda Kapilimposhi Zambia.
Alitaja chanzo cha ajali hiyo ni hitilafu
iliyojitokeza kwenye mfumo wa breki na hivyo kushindwa kufunga breki na baadae
kuacha njia na kisha kupunduka, ambapo
dereva wa akiba wa treni hiyo, Mashaka Bujilima alilipata majeraha na
kupelekwa Hospitali ya Ilembula iliyopo wilayani Njombe na baadae kuruhusiwa
baada ya kupata matibabu.
" Tumepokea kifo cha mpedwa wetu Kalumanga kwa masikitiko na hazuni kubwa kwa
kuwa amekuwa nasi kwa muda mrefu,lakinisasa kametutoka jina la bwana
lihimidiwe,’’ alisema Akashambatwa.
Alisema Treni hiyo ilikuwa imebeba shehena
ya mizigo mbalimbali ikiwa ni pamoja na injini za teni mbili, magari 16 ya
mbolea, magari tisa ya mafuta ya treni na mengine ni magari ya vifaa
mbalimbali,ambapo tathimini ya hasara ya mali, inaendelea kufanyiwa uchunguzi.
"Timu ya wataalamu mbalimbali na
waandamizi, mara moja imenzisha uchunguzi kwa kina sababu ya ajali hii ya kutisha , lakini ripoti ya awali
imewasilishwa kwa serikali mbili za
Tanzania na Zambia," alisema Akashambatwa.
Aidha Akashambatwa, alisema kuwa kwa
huzuni kubwa wametuma rambirambi
zao kwa familia ya marehemu na kuwapa
pole kwa niaba ya familia nzima ya TAZARA.
Mwisho |
No comments:
Post a Comment