KIUNGO wa zamani wa kimataifa nchini aliyewahi kung'ara na timu za Simba na Taifa Stars, Khaleed Abeid, ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa Chama cha Umoja wa Wachezaji Soka Tanzania, SPUTANZA.
Khaleed ameteuliwa pamoja wajumbe wengine sita kuiongoza kamati hiyo kwa minajili ya kusimamia uchaguzi mkuu wa SPUTANZA unaotarajiwa kufanyika Oktoba 20.
Uteuzi huo ulitangazwa jana na Katibu Mkuu Msaidizi wa SPUTANZA, Abeid Kasabalala alipozungumza na MICHARAZO na kuwataja wengine waliopo katika kamati hiyo kuwa ni Hashim Memba ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo.
Kasabalala aliwataja wengine wanaounda kamati hiyo ni Sued Mwinyi anayekuwa Katibu wa Kamati pamoja na wajumbe wanne akiwamo nyota za zamani wa timu za Yanga na Pan Africans.
"Wajumbe wa kamati hiyo ni Is'haka Hassani 'Chukwu', Carlos Mwinyimkuu, Saad Mateo na Hamis Shaaban," alisema Kasabalala.
Kasabalala aliongeza mpaka sasa zoezi la uchukuaji na urudishaji wa fomu kwa ajili ya uchaguzi wao unaendelea na zoezi hilo litahitimishwa keshokutwa kabla ya kamati yao kupitia majina kwa ajili ya kuyachuja.
Mwisho
No comments:
Post a Comment