TENGA ASEMA TFF, SERIKALI KUKUTANA KUMALIZA UTATA WA TRA
Tenga |
SHIRIKISHO
la soka Tanzania (TFF) pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na
Michezo, wanatarajiwa kukutana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa ajili ya
kuzungumzia mustakabali mzima wa suala la makato katika michezo mbalimbali.
Hatua hiyo
inafuatia TRA kuzifunga akaunti za udhamini wa ligi hiyo kama shinikizo kwa
TFF kulipa makato ya kodi kwenye
mishahara ya timu ya taifa ‘Taifa Stars’ tangu kipindi cha kocha Mbrazil Marcio
Maximo kwa madai kwamba imekuwa haikatwi kodi za mishahara ya makocha na hivyo
kufikia sh milioni 157,407.968.00.
Rais wa TFF,
Leodger Tenga amesema leo kwamba kitendo walichokifanya TRA ni jambo la heri
kwani kinaonyesha majukumu ya Serikali katika soka.
Alisema
ukaribu uliopo sasa baina ya Serikali chini ya Rais Kikwete na soka ni mkubwa
kutokana na ukweli kwamba inachangia kwa
kiasi kikubwa kulipa mishahara ya makocha wa timu za Taifa.
Alisema
suala hilo linahitaji mazungumzo baina ya pande hizo ili kuweza kulipatia
ufumbuzi na hakuna haja ya kuilaumu TRA kwa sababu inafuata taratibu
zilinazostahili kwa mujibu wa kanuni.
“Hawana njia nyingine ya kufanya hivyo
ufumbuzi ni sisi ni kukutana na Wizara na TRA ili kulizungumza hili na katika
siku mbili hizi tunarajiwa kukutana,”alisema
Tenga
aliongeza kuwa TFF haina uwezo wa kulipa fedha hizo na kwamba hela
zilizochuliwa si za Shirikisho hilo bali ni za ligi kuu Bara ambazo zimetolewa
na wadhamini wake, kampuni ya simu za mkononi,Vodacom kwa maelekezo maalum.
“Ni jambo nyeti na lazima lifanyiwe kazi,
hatuwezi kumlamu mtu na nimatumaini tutakapoketi pamoja tutapata
ufumbuzi,”alisema.
Aidha, Tenga
alisema wanatarajia kuzungumzia suala la makato ya michezo mbalimbali ambayo
yamekuwa yakilalamikiwa na vilabu kwa muda mrefu.
“Changamoto za namna hiyo tumekuwa
tukizifanyia kazi kwa muda mrefu na ndiyo maana tangu mwaka 2005 asilimia ya
makato ya TFF imekuwa ikipunguzwa, nadhani ni kuendelea kuwa na subira.
No comments:
Post a Comment