NYOTA wa filamu ambaye pia ni mwanamitindo na muimbaji wa muziki wa kizazi kipya nchini, Baby Madaha anatarajiwa kufanya ziara ya maonyesho katika nchi nne tofauti za Afrika.
Ziara hiyo itakayoanza mapema mwezi ujao na itakayochukua muda wa
mwezi mzima itamshirikisha msanii huyo na wakali wengine ambao
watapangwa katika ratiba hiyo kutoka nchini.
Akizungumza na MICHARAZO, Madaha alisema ziara hiyo itahusisha
nchi za DR Congo, Zimbabwe, Angola na Msumbiji na itaratibiwa na 'super
market' moja kubwa nchini inayomilikiwa na Jumanne Kishimba.
"Kaka yangu natarajia kufanya ziara ndefu ya kujitangaza kimataifa
nje ya nchi ambayo itakuwa ya maonyesho ya muziki na filamu katika nchi
nne za Afrika, ziara itakayochukua muda wa zaidi ya wiki tatu," alisema
Baby Madaha.
Mkali huyo alisema katika ziara hiyo mratibu mkuu atakuwa muigizaji mwingine nchini Mariam Mndeme 'Mamuu'.
Alisema kwa sasa anaendelea na maonyesho ya ndani ambapo wiki hii
anatarajiwa kuwa jijini Mwanza kabla ya kuanza maandalizi ya safari hiyo
ambayo amedai itamsaidia kujitangaza na kuitangaza Tanzania kimuziki na
filamu nje ya mipaka.
"Kwa sasa naelekea Mwanza kwa ajili ya maonyesho kadhaa kabla ya
kujiandaa na safari hiyo," alisema Baby aliyeibuliwa na shindano la
Bongo Star Search (BSS) la mwaka 2008.
No comments:
Post a Comment