Mamuu (kulia) akiwa na Baby Madaha walioicheza filamu hiyo ya Tatakoa |
MWANAHABARI aliyejitosa kwenye fani ya uigizaji na utayarishaji wa filamu nchini, Mariam Mndeme 'Mamuu' amefyatua filamu mpya iitwayo Tatakoa iliyowashirikisha nyota kadhaa nchini.
Mamuu, aliyewahi kuwa mtangazaji wa TBC na kufanya kazi katika magazeti ya Global Publisher, alisema filamu hiyo ni ya pili kwake baada ya awali kuitoa 'Pooja'.
Mwanahabari huyo aliiambia MICHARAZO kuwa, filamu hiyo ya 'Tatakoa' iliyowashirikisha wakali kadhaa ipo hatua ya mwisho kabla ya kuachiwa hadharani.
Mamuu alisema mbali na yeye wakali wengine waliyoicheza filamu hiyo ni pamoja na Baby Madaha, Frola Mvungi, Salma Jabu 'Nisha', Husna Idd 'Sajenti'. Alice Bagenzi 'Rayuu', Jumanne Kihangale 'Mr Chuz'. Kupa, Zerisha na wengine.
"Baada ya kimya kirefu tangu nilipotoa Pooja, nimekuja na filamu nyingine mpya iitwayo 'Tatakoa' ambapo mimi na Mr Chuz ndiyo wahusika wakuu, huku Baby Madaha akicheza jana 'Jini-Joka'," alisema Mamuu.
Msanii huyo alisema filamu hiyo kazi hiyo mpya ni mwanzo wa kuwapa mashabiki wake burudani ndani ya mwaka huu, akiwa pia mbioni kuratibu kipindi maalum kwa ajili ya walemavu waliokata tamaa waliopo maeneo ya vijijini.
"Nimeona kama mwanajamii napaswa kutoa mchango wangu kwa walemavu kwa kuandaa kipindi hicho kutakachokuwa kikionyesha matatizo ya watu hao na kusaidia kupata misaada itakayowawezesha kujikwamua kiuchumi," alisema Mamuu.
Mamuu alisema kipidni hicho anachokirekodi kuwasaidia walemavu anapigwa tafu na kigogo mmoja wa serikalini ambaye ji waziri, lakini aliyekataa kumtaja jina kwa sasa na mwingine ni Wema Sepetu
No comments:
Post a Comment