MASHINE ZA UMRI ZAWAUMBUA 'VIJEBA' VYA MICHUANO YA AFRIKA
UDANGANYIFU wa umri wa wachezaji kutoka barani Afrika umekuwa ni jambo la kawaida, lakini teknolojia mpya iliyobuniwa ya kutumia mashine kupima umri sahihi wa wachezaji umeanza kuwaumbua wachezaji 'vijeba' wanaochjachakachua umri ili kujifanya wadogo.
Teknokojia hiyo imewaumbua wachezaji tisa
na kuondolewa kwenye michuano ya mataifa ya Africa chini ya umri wa
miaka 17 yanayofanyika nchini Morocco baada kipimo cha kugundua umri
kupitia kiganja cha mkono kuonyesha kwamba wana umri mkubwa zaidi
kuliko inavyopaswa.
Miongoni mwa wachezaji watatu wanatoka Congo-Brazzaville, Ivory Coast na Nigeria wamefungiwa kabisa kushiriki kwenye mashindano yoyote.
Mashine ya Magnetic Resonance Imaging (MRI) ilitumika kupima viganja vya wachezaji ili kujua ukweli wa umri wao.
Wachezaji
ambao wameondolewa kwenye michuano hiyo ni kutoka Congo
Cherlevy-Diabala Carim, Hardy Binguila na Bermagin Kangou, kutoka Ivory
Coast ni Dagou Britto, Abdul Diarrassouba na Siriki Dembele, na kutoka
Nigeria ni Onyinye Ndidi, Ibrahim Abdullahi and Emmanuel Asadu.
Vikosi vya timu zote tatu vimepunguzwa mpaka kufikia wachezaji 18.
FIFA
walianza kufanya utafiti wa umri wa wachezaji kwa kutumia technolojia
ya MRI mwaka 2003 lakini wakaanza kuifanyia majaribio machine hiyo
kwenye michuano ya U-19 World Cup in Nigeria.
Matokeo ya
vipimo kwenye michuano ya kombe la dunia U-17 kuanzia 2003, 2005 na 2007
yalionyesha kwamba asilimia 35 ya wachezaji walikuwa wamezidisha umri
unaoruhusiwa.
Wadau wa soka wanatamani kipimo hicho kianze kutumika pia hapa nchini ili kubaini baadhi ya wachezaji 'vibabu' lakini wakijitambulisha wakiwa na umri mdogo, jambo ambalo hata wenyewe wanajishangaa wanavyoongopa.
Credit to shaffihdauda.com
No comments:
Post a Comment