STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, April 16, 2013

Coastal Union, kuvuna nini leo kwa JKT Ruvu Mkwakwani?


Kikosi cha Coastal Union watakaoikaribisha JKT Ruvu
MICHUANO ya Ligi Kuu Tanzania Bara inayoelekea ukingoni, inatarajiwa kuendelea leo kwa pambano moja la kukata na shoka kati ya Coastal Union ya Tanga dhidi ya wageni wao maafande wa JKT Ruvu ya Pwani.
Pambano hilo litachezwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Mkwakwani-Tanga, ambapo kila timu itakuwa ikihitaji ushindi ili kufikia malengo tofauti waliyonayo, Coastal ikiwania kuingia kwenye Tatu Bora na JKT kujinasua toka kwenye mstari wa hatari wa kushuka daraja.
Coastal ambayo katika mechi yake ya mwisho ilikumbana na kipigo cha kushtukiza toka kwa wanaoburuza mkia, African Lyon, ina pointi 32 na ushindi katika pambano la leo itawafanya wakwee nafasi moja hadi ya tano na kuiengua Mtibwa Sugar itakayoshuka dimbani kesho.
Hata hivyo maafande wa JKT ambo wamekuwa na msimu mbaya safari hii, wanapigana kuondoka katika janga la kuteremka daraja kutokana na ukweli mpaka sasa ipo nafasi ya 12 ikiwa na pointi 22 tu sawa na Toto African, wakizizidi pointi mbili timu zilizozopo mkiani Lyon na Polisi Moro ambazo zina pointi 19 kila moja.
Kwa mazingira ilizonazo timu hizo ni wazi pambano la leo litakuwa gumu na lenye ushindani mkubwa ikizingatiwa kuwa, mashabiki wa Coastal wamekosa furha kitambo na timu yao kiasi cha kupost maoni yenye kukera dhidi ya uongozi na wachezaji wao.
Ligi hito inatarajiwa kuendelea tena kesho kwa michezo kadhaa likiwamo pambano la Yanga dhidi ya JKT Mgambo ambao kupitia kocha wao mkuu, Mohammed Kampira wameapa kuwazuia vinara wa ligi hiyo wasiwafanye daraja la kutwaa ubingwa msimu huu.
Yanga inaoongoza msimamo wa ligi ikiwa na pointi 52 na inahitaji pointi sita tu kutawazwa mabingwa wapya baada ya waliokuwa wakilishikilia Simba kutemeshwa mapema wakati ligi ikiwa bado inaendelea kwa vile itawafanya wafikishe pointi 58 ambazo hazitaweza kufikiwa na Azam wanashika nafasi ya pili ambao wakishinda mechi zake nne tatu zilizosalia itafikisha pointi 56 tu.
Mechi zitakazopigwa kesho kwa mujibu wa ratian ya ligi hiyo ni kama ifuatavyo;
Mgambo JKT vs Yanga,
Kagera Sugar v Toto Africans (japo Toto imetishia kutoicheza mechi hiyo ya leo, ikihofia upangaji matokeo)
Mtibwa Sugar v JKT Oljoro

No comments:

Post a Comment