Rami Rabia |
Nahodha Nadir Cannavaro (kati) aliyewaua Al Ahly wiki iliyopita akiwa na nyota wenzake, Athuman Idd Chuji na Haruna Niyonzima. Bila shaka kesho wataendelea kuwapa raha Watanzania kwa kuing'oa Ahly. |
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Misri, wachezaji hao wanatarajia kushuka dimbani kesho kukabiliana na Yanga kwenye mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayochezwa kwenye uwanja wa Mexx, jijini Alexandria.
Kuongezeka kwa wachezaji hao kunaifanya Mashetani hao Wekundu wa Misri kuchekelea wakiamini Yanga itakufa kama walivyouwawa wao ugenini kwa kuwalaza bao 1-0 kwa goli la kichwa cha kuchupia cha nahodha, Nadir Haroub Cannavaro.
“Rabia yu tayari kwa mechi dhidi ya Young Africans baada ya kupoma jeraha la bega aliloumia wakati akiichezea Mafarao na kusshinda 2-0," mtandao wa Ahly uliandika taarifa hiyo.Taarifa hiyo iliongeza pia kiungo wao Moussa Yedan naye atakuwepo katika mechi hiyo ya Jumapili, ingawa itawakosa mshambuliahji wao Emad Meteb aliye majeruhi wa misuli.
Hata hivyo Yanga waliokamili gado jijini humo, inaripoti wana ari kubwa baada ya kufanya mazoezi leo katika uwanja huo watakaoutumia kesho baada ya kushtukizwa na wenyeji wao kwamba mechi imehama toka Cairo.
Kitu cha kufurahisha mechi hiyo haitakuwa na watazamaji na kuwapa nafasi nzuri Yanga kuwashikisha adabu Wamisri hao na ikiwezekana kuwavua taji kwenye ardhi yao ya nyumbani kama walivyowahi kufanya watani zao Simba dhidi ya Zamalek waliokuwa watetezi wa michuano ya mwaka 2003.
Taarifa kutoka Misri zinasema kuwa kikosi cha wachezaji wa Yanga wapo fiti wakiwa hakuna majeruhi haya mmoja na kwamba iwe isiwe ni lazima Mashetani Wekundu hao wafe licha ya hila zao za kuchelewa kutajwa uwanja wa mchezo huo kama inavyotakiwa na taratibu za soka za kimataifa.
Mungu ibariki Tanzania Ibariki Yanga kesho iweze kuvunja rekodi kwa kuing'oa Al Ahly kwao.
No comments:
Post a Comment