Arteta kifungwa mkwaju wake wa penati |
Lukaku akishangilia bao lake ambalo halikuisaidia Everton kwa Arsenal leo |
Mtokea benchi Oliver Giroud akiwatoka washindi na kufunga moja ya mabao yake mawili leo |
KIUNGO Mesut Ozil amefunga bao boa na kusaidia jingine lililtumbulizwa kimiani na Oliver Giroud wakati Arsenal ikiifumua Everton kwa mabao 4-1 na kutinga hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la FA kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2009.
Ozil ambaye amekuwa na wakati mgumu kwa mashabiki wa Arsenal tangu alipokosa mechi ya Arsenal dhidi ya Liverpool walipofungwa mabao 5-1 na kuja kukosa penati kwenye Ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern, alionyeha kiwango cha juu katika mchezo huo uliochezwa uwanja wa Emirates.
Kiungo huyo wa Ujerumani alifunga bao la kuongoza dakika ya 7 kwa pasi ya Santi Cazorla kabla ya Romelu Lukaku kuisawazishia Everton bao dakika ya 32 na kufanya timu hizo ziende mapumziko zikiwa sare ya 1-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa Arsenal kujiongezea bao la pili kwa amkwaju wa penati dakika ya 68 iliyofungwa na Mikel Arteta kabla ya mtokea benchi Giroud kufunga mengine mawili dakika za saba za mwisho za mchezo huo.
Mchezaji huyo alifunga bao lake la kwanza na la tatu katika mchezo huo dakika ya 83 akimalizia kazi ya Bacary Sagna na dakika mbili baadaye kuongeza jingine baada ya kazi nzuri ya Ozil na kuiofanya Arsenal kuibuka kidedea kwa maba0 4-1 na kutina Nusu Fainali ya michuano ya Kombe hilo.
Michezo mingine ya Robo Fainali ya michuano hiyo itachezwa kesho kwa mechi itakayozikutanisha Sheffield United dhidi ya Charlton Athletic mechi itakayochezwa mapema kabla ya Hull City kuvaana na Sunderland na Manchester City usiku kuvaana na Wigan Athletic.
No comments:
Post a Comment