Et'oo akishangilia bao lake |
Eto'o akipongezwa baada ya kufunga bao la utangulizi |
Nahodha John Terry akimpongeza Eto'o |
Samuel Ot'oo alikuwa wa kwanza kuifungia Chelsea bao dakika tano baada ya kuanza kwa kipindi cha pili kabla ya Edin Hazard kuongeza la pili kwa mkwaju wa penati dakika ya 65 baada ya Younes Kaboul kumchezea vibaya Et'oo kosa lililomfanya alimwe kadi nyekundu na kutolewa uwanjani.
Kocha Jose Mourinho alifanya mabadiliko ya haraka haraka akimtoa Etoo na nafasi yake kuchukuliwa na Demba Ba ambaye hakuwa na ajizi baada ya kufunga mabao mawili katika dakika ya 88 na 90 yaliyotosha kuihakikisha Chelsea kukaa kileleni ikiwa na pointi 66 saba zaidi ya iliyonayo Liverpool na Arsenal zenye 59 kila moja..
Katika mechi nyingine za mapema Cardiff City ikiwa nyumbani iliisasambua Fulham kwa kuicharaza mabao 3-1, Southampton ikiwa ugenini ilipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji wao Crystal Palace, huku Norwich City na Stoke City ilitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.
No comments:
Post a Comment