STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, March 2, 2014

Jide waing'arisha Sikinde kizamani

Lady Jaydee a.k.a 'Anaconda'
Baadhi ya wanamuziki wa Sikinde, wakiwajibika jukwaani
BENDI kongwe ya muziki wa dansi ya Mlimani Park 'Wana Sikinde' imeanza kurekodi nyimbo za zamani ikishirikisha baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya ili kuzipa vionjo tofauti.
Sikinde imeanza na wimbo wa 'Duniani Kuna Mambo', ambao imeurekodi kwa kumshirikisha mkongwe Muhidini Gurumo 'Kamanda' na nyota wa muziki wa kizazi kipya, Lady Jay Dee.
Katibu wa bendi hiyo, Hamis Milambo alisema wimbo huo tayari umeshasambazwa kwenye vituo vya redio na kuanza kurushwa hewani wakijipanga kurekodi nyimbo nyingine hapo baadaye.
Milambo alisema wanataka kurekodi nyimbo zao zote za zamani kwa lengo la kukumbusha kizazi cha sasa kazi kubwa iliyofanywa na bendi hiyo katika kuendeleza muziki wa Tanzania.
Alisema nyimbo hizo baadhi zimeshasahaulika kutokana na mfumo wa zamani wa kurekodi na utunzaji ulivyokuwapo na hivyo wanataka kuzirudia na kuziweka kisasa ili kusaidia kudumisha muziki wao.
"Tumeanza na wimbo wa Duniani Kuna Mambo ambao tumeimba na Lady Jay Dee na Mzee Gurumo na umeanza kuruka hewani, baada ya hapo zitafuata nyingine tukishirikisha wasanii mbalimbali," alisema.
Milambo alisema pia bendi yao iliyoasisiwa mwaka Agosti 1978 inaendelea kurekodi nyimbo mpya kwa ajili ya albamu yao ijayo waliyopanga kuizinduliwa maadhimisho yao ya miaka 36.

No comments:

Post a Comment