NCHI ya Congo imetangaza kugoma kwenda Nigeria kucheza pambano lao la kuwania kufuzu Fainali za Afrika za 2015 kwa ilichodai inahofia tisho la ugonjwa wa Ebola.
Hata hivyo Shirikisho la Soka
la Nigeria (NFF) limedai kuwa halijapata taarifa yoyote rasmi kutoka
Shirikisho la Soka la Afrika-CAF juu ya madai ya Congo Brazzaville
kuelekea katika mchezo huo uliopangwa kuchezwa huko Calabar.
Congo ambao watakuwa wageni wa Nigeria
katika mchezo huo utakaochezwa Septemba 6 mwaka huu wametuma malalamiko
CAF kueleza wasiwasi wao juu usalama katika mchezo huo.
Congo
wamesisitiza hawatakwenda katika mji wa Calabar au mwingine wowote
nchini Nigeria kwa ajili ya mchezo huo kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa
Ebola.
Ugonjwa huo usiokuwa na tibaumeripotiwa kuua zaidi za watu 1427 katika miji ya nchi za Liberia, Guinea, Sierra Leone na Nigeria, huku wengine zaidi ya 2,615 wakiambukizwa toka
ugonjwa huo ulipolipuka Machi mwaka huu.
Kocha wa timu ya taifa ya
Congo, Claude Leroy amesema itakuwa ngumu na hatari kwenda Nigeria kwa
ajili ya mchezo huo na kudai kuwa hata majirani zao Cameroon tayari
wamefunga mipaka yao ili kuepusha maambukizi zaidi.
Hata hivyo NFF
wamesisitiza kuwa mchezo utafanyika kama ulivyopangwa katika Uwanja wa
UJ Esuene uliopo mji wa Calabar.
No comments:
Post a Comment