STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, August 27, 2014

Giroud awapa presha Arsenal

HUENDA Olivier Giroud akakaa nje ya dimba kwa miezi mitatu ijayo baada ya vipimo kuonyesha kuwa amevunjika mfupa katika unyayo wakati wa mechi dhidi ya Everton Jumapili kwenye Uwanja wa Goodison Park, kwa mujibu taarifa kutoka Ufaransa.
Jarida la Ufaransa la L'Equipe limeripoti matokeo hayo ya majeraha ya Giroud yamezua hofu kwa Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger na kwamba sasa atalazimika kurudi sokoni kwa kasi kununua mshambuliaji.
Wenger alikuwa amesisitiza kwamba hana mpango wa kusajili mshambuliaji katika dirisha hili la usajili wa majira ya joto, akiamini kuwa usajili mpya wa Alexis Sanchez, huku hivi karibuni Theo Walcott akitarajiwa kurejea pamoja na uwapo wa Yaya Sanogo kungemwezesha kuwa na safu bora ya ushambuliaji.
Hata hivyo, kitendo cha Giroud kutokea benchi katika Uwanja wa Goodison Park Jumamosi na kusawazisha kulimpa matumaini kocha huyo, hatua iliyomfanya kumtabiria kuwa atamaliza Ligi Kuu England akiwa na mabao 25.
Kama taarifa hizo zitathibitishwa, mipango yake hiyo itafanyiwa mabadiliko, wakati huu ambao chumba cha majeruhi cha  Arsenal kikianza kusheheni wagonjwa ndani ya wiki mbili hizi za mwanzo wa msimu mpya.
Kuwa majeruhi kwa Giroud, kutamlazimisha Wenger kusaka huduma ya mshambuliaji wa Queens Park Rangers, Loic Remy, licha ya mapema majira haya ya joto kutupilia mbali uwezekano wa kumsajili Mfaransa huyo.

No comments:

Post a Comment