KIPIGO cha aibu cha mabao 4-0 toka kwa timu ya daraja la kwanza ya MK Dons waliowang'oa kwenye Kombe la Ligi kimemzindua Kocha wa Manchester United, Luis Van Gaal ambaye amehamishia nguvu zake kumnasa kiungo wa Juventus, Arturo Vidal.
Van Gaal na Afisa mkuu wa klabu hiyo Ed Woodward
wanahaha kusaka saini ya Vidal baada ya kumaliza
kusajili Angel Di Maria jana.
United imekuwa ikipinga kumhitaji Vidal
kwa kipindi kirefu lakini sasa wanadaiwa kuanza mazungumzo
kama wanayofanya dhidi ya Ajax Amsterdam kwa ajili ya kumsajili Daley
Blind.
Majeruhi pekee ndiyo yalioonekana kumzuia Van Gaal kumsajili nyota huyo
wa kimataifa wa Chile ambaye ana thamani ya paundi milioni 30 lakini
kutokana na matokeo mabovu ya hivi karibuni klabu imeona hakuna jinsi
bali kutumia fedha ili wajiimarishe.
Upasuaji wa goti msimu uliopita
ulimzuia Vidal kuitumikia Juventus toka mwishoni mwa Machi mwaka huu
ingawa baadae alipona na kupata muda wa kuwepo katika kikosi cha Chile
katika michuano ya Kombe la Dunia.
Ujio wa Vidal, 27 United kutasaidia kuimarisha safu ya kiungo ambayo imeonekana
kuyumba na kupelekea kipigo cha mabao 4-0 jana dhidi ya timu ya daraja
la chini ya MK Dons katika mchezo wa Kombe la Ligi.
Kama United
wakifanikiwa kumsajili Vidal watakuwa wamefikisha kiasi cha paundi
milioni 150 walizotumia msimu huu kwa ajili ya usajili baada ya kuvunja
rekodi nchini Uingereza kwa uhamisho wa Di Maria.
No comments:
Post a Comment