Ritta Kabati alipokuwa kitoa mtazamo wake kuhusu viti maalumu vya ubunge |
MBUNGE wa Viti
Maalumu Mkoa wa Iringa, Ritta Kabati (CCM) amesema moja ya mambo
anayounga mkono katika mchakato wa Katiba Mpya ni kufutwa kwa viti
maalumu vya ubunge.
Akizungumza
hivi karibuni nje ya jengo la CCM Mkoa wa Iringa, Kabati alisema Viti
Maalumu vina faida zake katika mchakato wa maendeleo lakini
vinawadhalilisha sana wanawake.
“Siku hizi
wabunge wanawake wa viti maalumu tunaitwa wabunge wa vitanda maalumu,
huu ni udhalilishaji kwa sababu wengi wanahisi upatikanaji wake una
mahusiano yasiofaa,” alisema.
Alisema
utaratibu unaotumiwa na nchi kama Uganda na Rwanda kupata wawakilishi
wanawake katika mabunge yao ndio unaopaswa kutumiwa na Tanzania na kama
ikishindikana basi wanawake nao wapewe nafasi sawa na wanaume ya
kugombea moja kwa moja kwenye majimbo ya Uchaguzi.
“Tumetembelea
Uganda na Rwanda, kule hawaiti viti maalumu vya wanawake, wanaita viti
vya wilaya vinavyoshindanisha wanawake wa vyama mbalimbali katika wilaya
hizo,” alisema.
No comments:
Post a Comment