KOCHA wa Mabingwa wa Ligi Kuu ya England, Manuel Pellegrini amethibitisha kuwa kiungo wa zamani wa Chelsea, Frank Lampard keshokutwa ataanza mazoezi na wachezaji wa Manchester City kwenye uwanja wa Carrington kwa ajili ya msimu mpya wa ligi hiyo.
Pellegrini alisema kuwa Lampard atakuwa mchezaji muhimu kwenye mechi za ligi kuu na ligi ya mabingwa mpaka atakapoondoka kwenda Marekani mwezi Januari mwakani.
City imewasili nyumbani kutoka Marekani ilipokuwa katika maandalizi ya ligi na kucheza mechi kadhaa za kimataifa maalum kabla ya jana jumapili kupoteza nafasi ya kucheza fainali ya michuano hiyo kwa kufungwa kwa penati ikiwa ni mecxhi yao ya pili katika siku nne kupoteza kwa mikwaju ya penati.
Baada ya mechi, Pellegrini kwa mara ya kwanza alizungumzia kumsajili Frank kwa mkopo na kusema maamuzi ya kumchukua kiungo huyo wa kimataifa wa England mwenye miaka 36 ni kumfanya awe fiti kabla ya kuanza kuichezea klabu yake ya New York City mwakani.
Lampard alijiunga na New York City akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na Chelsea.
Pellegrini alisema: "Kuanzia jumatano ijayo ataanza kufanya kazi na timu na atacheza mpaka januari na tutaona baada ya hapo".
"‘Kwa wakati huu atafanya kazi na kikosi na atakuwa mmoja wa wachezaji wa kikosi. Atapambana kusaka nafasi"
"Anajua tuna timu nzuri, tuna wachezaji wengi katika nafasi yake na yeye ameongezeka. Tuna mechi nyingi sana hususani za ligi ya mabingwa, kwahiyo ni mtu muhimu sana kwa timu".
No comments:
Post a Comment