STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, August 4, 2014

Mcongo wa Azam atimka kwao, Ghana, Mhaiti bado majaribuni

Kiungo Lofo Serge aliyetimkia kwao
Kiungo Joseph Peterson wa Haiti anayeendelea kujaribiwa
MABINGWA wa soka nchini, Azam wanaendelea kuwapima kwa mara ya mwisho wachezaji wawili wa kimataifa kutoka Haiti na Ghana, huku nyota mwingine wa DR Congo Lofo Serge akitimka kwao baada ya majaribio yake.
Wachezaji wanaoendelea kujaribiwa kabla ya kuamuliwa hatma yao ni kiungo Joseph Peterson wa Haiti na beki Ben Achaw kutoka Ghana, wakati Serge ambaye ni mshambuliaji akimaliza majaribio yake na kutimka.
Akizungumza na MICHARAZO, Meneja wa Azam, Jemedari Said alisema wachezaji wote wameonyesha viwango vya hali ya juu katika kusaka soka, ila hatma yao itaamuliwa na kocha Joseph Omog mwenye maamuzi ya mwisho.
Jemedari alisema Serge alitua nchini baada ya kutumiwa tiketi na uongozi wao na muda wake ulikuwa wa wiki moja, wakati wenzake walitua wenyewe nchini na watamalizia wiki yao ya pili kabla ya kuondoka.
"Serge alijaribiwa kwa wiki moja na kwa uzoefu na umaarufu wake siyo jambo la ajabu kumaliza mapema na hao wengine waliokuja wenyewe wanamalizia wiki yao ya mwisho kabla ya kocha kuamua hatma yao," alisema Jemedari.
Meneja huyo alisema kwa waliowashuhudia wachezaji hao wakati na kikosi cha Azam watakubaliana naye kwamba ni wachezaji wazuri, ila kocha ndiye atakayeamua iwapo kama watafaa uitumikia timu yao.
"Kama wataonekana wanavitu vya kuisaidia timu basi watafahamishwa hata wakiwa makwao, lakini kwa hakika karibu wote wanaonekana wazuri," alisema Jemedari nyota wa zamani wa kandanda nchini aliyetamba Majimaji-Songea.
Kabla ya kujaribiwa Azam Serge anayeichezea pia timu ya taifa ya nchi yake, aliwahi kutamba na timu za AS Paulino Kinshasa, TP Mazembe, AS Aviacao, Sagrada Esperança, AS Vita, FC Brussels na Maccabi Netanya.

No comments:

Post a Comment