LIGI ya Wanawake Mkoa wa Dar es Salaam inatarajiwa kuanza Agosti 28 mwaka huu katika viwanja vya Benjamin Mkapa, Bandari na Makurumla.
Ofisa
Habari wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA),
Mohamed Mharizo alisema kuwa ligi hiyo ni moja ya mkakati wao wa
kuimarisha mchezo ili uweze kuwa na hamasa kwa wanawake.
Alizitaja timu zitakazoshiriki ligi hiyo kuwa ni Mburahati Queens, Evergreen Queens, Sayari, Real Tanzanite, Uzuri Queens, Simba Queens, BYC Queens, JKT Queens, Lulu Queens, Mchangani Sisters, TMK Queens, Msimamo Queens na Mikocheni Queens.
“Kwa
kweli ligi ya wanawake nayo ni muhimu kama ilivyo kwa wanaume, lengo
letu ni kuona wanawake wanakuwa na ligi yao na sisi tunaona hili ni
jambo zuri ambalo litasaidia kupata wachezaji wa timu ya taifa (Twiga
Stars).
Mharizo aliyaomba makampuni na taasisi mbalimbali kujitokeza kudhamini ligi hiyo ili iweze kuleta ushindani kwa timu shiriki.
No comments:
Post a Comment