MUINGEREZA
Andy Murray ameanza vizuri kampeni zake za kutwaa ubingwa wa mashindano ya
Dubai baada ya kuibuka na ushindi wa seti 6-4 7-5 dhidi ya Gilles Muller.
Mscotland
huyo, mwenye umri wa miaka 27, alipata ushindi huo kwa kutumia saa moja na
dakika 45, na sasa atacheza na Joao Sousa katika raundi ya pili, ikiwa ni wiki
mbili baada ya kumshinda Mreno huyo katika mashindano ya Australian Open.
Bingwa
anayeongoza kwa ubora Novak Djokovic naye alianza vizuri mashindano hayo baada
ya ku
James
Ward ambaye ni Muingereza anayeshikilia nafasi ya pili kwa ubora, alijikuta
akishindwa kufanya kweli baada ya kushindwa mara mbili katika hatua ya kufuzu
na kupoteza kwa 6-4 6-4 dhidi ya Muhispania Feliciano Lopez, anayeshikilia
nafasi ya 13 kwa ubora duniani.
Muingereza
huyo sasa atakwenda Glasgow kujiunga na timu ya Uingereza itakayocheza mchezo
wa Davis Cup dhidi Marekani, utakaofanyika kuanzia Machi 6-8 huko Emirates.
Murray
anatarajia kukawia kujiunga na wenzake huko Scotland endapo ataendelea kufanya
vizuri huko Dubai baada ya leo kuanza vibaya mchezo huo katika jaribio lake la
kwanza, lakini alifanya vizuri na kuibuka na ushindi katika seti hiyo ya
kwanza.
Djokovic
anashiriki kwa mara ya kwanza tangu alipotwaa taji la Australian Open Februari
mosi na anaangalia kuwa mtu pekee wa 12 kushinda taji la 50.
No comments:
Post a Comment