Mtanzania Nasry Daud Aziz atakayejiunga na kituo hiki cha Senegal |
MWANASOKA chipukizi Nasry Daudi
Aziz aliyezaliwa Agosti 21, 2001 amechaguliwa kujiunga na kituo cha kukuza
vipaji cha Aspire Football Dream kilichopo katika mji wa Dakar nchini Senegal.
Mradi wa Aspire nchini ulianza mchakato wa kusaka
vijana mwezi Machi - Mei, 2014 ambapo vijana wengi walijitokeza na kuchaguliwa
vijana 14 ambao walikwenda katika mchujo mwingine uliofanyika nchini Uganda
uliowashirikisha vijana zaidi ya 50.
Kijana huyo ni
miongoni mwa wachezaji 17 waliochaguliwa kati ya vijana 34 walikuwepo nchini
Senegal kwa muda wa mwezi mmoja, ambapo kulikuwa na vijana wengi kutoka nchi mbalimbali
barani Afrika na Amerika ya Kusini.
Kituo cha Aspire
kilichopo Dakar nchini Senegal ni miongoni mwa vituo viwili vinavyoongozwa na
mtoto wa mfalme wa Qatar na timu ya Barcelona, kituo kingine kipo mjini Doha.
Nasry Daud Aziz anatarajiwa
kuondoka nchini Februari 28 mwaka huu kuelekea Dakar ambapo atakua kwenye kituo
hicho kwa mkataba wa miaka miatano.
Kutoka nchini Tanzania Nasry anakua ni kijana
wa tatu kujiunga na kituo hicho, wengine ni Matine Taganzi na Orgenes Morrel
ambaye aliitwa kwenye timu ya Taifa Stars maboresho na kocha Mart Nooj.
No comments:
Post a Comment