Joe Hart akiojkoa mkwaju wa penati ya Messi usiku wa jana |
Messi akiwa haamini kama mkwaju wake umezuiwa na kipa wa Man City |
Messi akiwa amelala chini baada ya kukosa penati |
Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina alikuwa na nafasi ya kuipa ushindi Barcelona wa mabao 3-1 katika dakika za majeruhi lakini Joe Hart alifanikiwa kuokoa mchomo wake.
Messi pia amekosa penati katika mchezo dhidi ya Levante, Septemba mwaka jana na Brazil wakati akiitumikia timu yake ya taifa Oktoba lakini Enrique anaamini kuwa nyota huyo bado ni mpigaji mzuri na anamuamini.
Kocha huyo amesema wale wote wanaokosa penati ni wale wenye uthubutu wa kufanya hivyo na Messi bado ataendelea kuwa mpigani wao.
Katika mchezo huo wa mkondo wa kwanza uliofanyika katika Uwanja wa Etihad, Barcelona ilifanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-1, ikiwa ni siku chache ikitoka kupokea kipigo cha bao 1-0 nyumbani Camp Nou dhidi ya Malaga katika Ligi Kuu ya Hispania (La Liga).
Kukosa penati hiyo ya juzi imemfanya Messi kulingana na Cristiano Ronaldo, Luis Figo and Andy Shevchenko katika michuano hiyo ya Ulaya wakitanguliwa na Ruud Van Nistelrooy aliyekosa mabao manne na Thierry Henry anayeongoza kwa kukosa penati tano.
Pia ni penati ya 13 kwa mkali huyo wa mabao wa Cataluna kati ya mikwaju 59 aliyopiga akiwa na klabu ya Barcelona, huku kwa upande wa nchi yake ya Argentina Messi amekosa mbili kati ya 12 alizopiga
No comments:
Post a Comment