Bruce Kangwa |
Kikosi cha Zimbabwe 'Thje Might Warriors |
HARARE,
Zimbabwe
KWA mashabiki wa klabu za Simba na Yanga, Donald Ngoma, Thabani Kamusoko na Methodi Mwanjali ni nyota wa aina yao, wanawategemea kwenye mechi zao za Ligi Kuu Bara. Sasa sikia hii. Wachezaji hao kwao wala si mali kitu, kwani kikosi cha timu ya taifa ya Zimbabwe nchi wanayotokea imeita nyota wake kwa ajili ya Fainali za Afcon 2017, bila ya wachezaji hao.
Nyota Khama
Billiat aliyeshika nafasi ya pili katika tuzo za Mwanasoka Bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani ya bara hilo, pamoja na kiungo mwenzake na nahodha Willard Katsande ni miongoni mwa
wachezaji nane wanaocheza soka Afrika Kusini ambao wameitwa katika kikosi cha
Zimbabwe.
Mchezaji Zimbabwe katika
mashindano ya mwaka huu imepangwa katika Kundi B, ambapo watacheza na Mabingwa
wa zamani Algeria na Tunisia na Senegal, wakati timu mbili za juu zitatinga
robo fainali.
Hii itakuwa
mara ya tatu kwa Zimbabwe kushiriki fainali hizo, ambazo walitolewa katika
raundi ya kwanza nchini Tunisia mwaka 2004 na kupata pigo kama hilo nchini
Misri miaka miwili baadae.
Mshambuliaji wa
pembeni Billiat alikuwa mchezaji muhimu aliyeisaidia timu ya Afrika Kusini ya
Mamelodi Sundowns wakati iliposhina taji la Ligi ya Mabingwa wa Afrika kwa mara
ya kwanza mwaka jana.
Pia mchezaji
huyo alikuwa mmoja kati ya wachezaji watatu waliofikia hatua ya mwisho ya
kumsaka mchezaji bora wa Afrika kwa timu za ndani iliyotwaliwa na kipa Mganda Dennis Onyango, akimtangulia pia Rainford Kalaba wa DR Congo.
Katsande kutoka
klabu maarufu Soweto ya Kaizer Chiefs naye alifanya kazi kubwa, baada ya
kujipanga mbele ya mabeki wakati katika ushambuliaji.
Kikosi Kamili cha
Zimbabwe
Makipa: Donovan
Bernard (How Mine), Takabva Mawaya (ZPC Kariba) na Tatenda Mkuruva (Dynamos).
Mabeki: Teenage
Hadebe, Lawrence Mhlanga (wote kutoka Chicken Inn), Onismor Bhasera (SuperSport
Utd/Afrika Kusini), Bruce Kangwa (Azam/Tanzania), Oscar Machapa (V Club/Ivory
Coast), Elisha Muroiwa (Dynamos), Costa Nhamoinesu (Sparta Prague/CZE),
Hardlife Zvirekwi (CAPS Utd).
Viungo:
Kudakwashe Mahachi, Danny Phiri (wote wa Golden Arrows/Afrika Kusini), Khama
Billiat (Mamelodi Sundowns/Afrika Kusini), Willard Katsande (Kaizer
Chiefs/Afrika Kusini,nahodha), Marvelous Nakamba (Vitesse Arnhem/Uholanzi),
Washambuliaji:
Tinotenda Kadewere (Djurgardens/Sweden), Cuthbert Malajila (Wits/Afrika
Kusini), Nyasha Mushekwi (Dalian Yifang/China), Knowledge Musona
(Ostend/Ubelgiji), Tendai Ndoro (Orlando Pirates/Afrika Kusini), Evans Rusike
(Maritzburg/Afrika Kusini), Mathew Rusike (CS Sfaxien/Tunisia)
Kocha wa kikosi
hicho ni Kallisto Pasuwa.
No comments:
Post a Comment