STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, March 15, 2015

HAKUNA UFISADI UNUNUZI KIVUKO CHA MV DAR ES SALAAM

Mtendaji Mkuu wa TEMESA, Eng. Mercelin Magesa
WAKALA wa Ufundi na Umeme (TEMESA) umesema hakuna ufisadi wowote ambao umefanyika katika mchakato mzima wa ununuzi wa Kivuko cha Mv Dar es Salaam.
Kauli hiyo Temesa imetolewa na Mtendaji Mkuu wa wakala huo Mhandisi Marcelin Magesa ikiwa ni siku moja baada ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuilalamikia Serikali kwa uamuzi wake wakununua Kivuko hicho wakati hakina tija kwa jamii.
Magesa alisema maandalizi ya awali ya ununuzi wa Kivuko hicho yalishirikisha wadau wote ambapo lengo lake ni kutoa huduma ya usafiri wa majini katika ukanda wa bahari ya Hindi.
Mtendaji Mkuu huyo alisema mpango wa ununuzi wa Kibuko hicho uliwasishwa katika Bunge la Bajeti la mwaka 2012/13 ambapo ulitengewa fedha ambapo fedha zingine zilitengwa bajti ya 2013/14 na 2014/15.
"Napenda kuweka wazi suala hili kwani juzi habari zilizotoka kwenye baadhi ya vyombo vya habari zinaonesha kuwa kuna mapungufu lakini utaratibu ulifuatwa kwa kutangazwa zabuni ambapo kampuni ua Ms. Johs Gram-Hanssen ya Denmark ndio ilishinda zabuni ya ujunzi wa Kivuko hicho kwa dola za Kimarekani 4,980,000 sawa na fedha za Tanzania sh.bilioni 7.916,955,000," alisema Magesa.
Alisema ujenzi wa Kivuko cha Mv Dar es Salaam, ulifanyika hatua kwa hatua ambapo kilifanyiwa ukaguzi mara nne Novemba 2013, Februari 2014, Julai 2014 na Septemba 2014 ambapo kiliingizwa majini kufanyiwa majaribio.
Magesa alisema kutokana na utaratibu wa ukaguzi huo ni dhahiri kuwa Kivuko hicho ni kipya, na kauli kuwa sio kipya zinahitaji kupuuzwa.
Mtendaji Mkuu alisema lengo la Kivuko hicho ni kupunguza msongamano ambao umekuwa ukiongezeka katika jiji la Dar es Salaam.
Alisema kwa sasa Temesa inaendelea kutoa huduma za usafiri nchini katika vituo mbalimbali 28  ambapo tangu mwaka 2012 wamenunua vivuko vitano vipya.
Mhandisi huyo alivitaja vivuko hivyo kuwa ni Mv Kilambo, Mv Mafanikio vinavyotoa huduma Mtwara, Mv Malagarasi Kigoma, Mv Tegemeo Mwanza na Mv Dar es Salaam

Monday, March 9, 2015

Barcelona wapaa kileleni kwa kuua 6, Messi apiga 'hat-trick' ya 24

Messi akifurahia kufunga baio
Messi akifanya vitu vyake
Messi ni shiida
Akijiandaa kufunga penati iliyozaa bao lake la kwanza
Barcelona wakipongezana
Suarez akishangilia bao lake

MSHAMBULIAJI Nyota wa Argentina, Lionel Messi alifunga hat trick ya 24 ya La Liga, huku Luis Suarez akifunga mabao mawili wakati Barcelona wakiizamisha Rayo Vallecano.
Ushindi huo umeifanya Barcelona kukwea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Hispania, La Liga wakiishusha Real Madrid ambayo Jumamosi ilifungwa ugenini na Deportivo la Coruna.
Barcelona walianza kuandika bao la kwanza dakika ya tano kupitia kwa Luis Suarez akimalizia kazi nzuri ya Xavi kabla ya Gerrard Pique kufunga la pili dakika ya 49.
Messi alianza kuandika karamu yake ya mabao kwa kufunga bao la tatu la Barcelona kwa mkwaju wa penati dakika ya 56 kabla ya kuongeza jingine dakika ya 63 na 68.
Bao la sita la Barcelona lilifungwa dakika za lala salama na Suarez akimaliza kasi nzuri ya Messi.
Rayo Vallecano walipata bao lao la pekee la kufutia machozi katika dakika ya 81 kwa mkwaju wa penati kupitia Bueno.

Arsenal, Man Utd ni vita tupu leo FA, Liverpool yabanwa

http://soccer.indonewyork.com/wp-content/uploads/2015/03/mufc-arsenal-fa-cup-3-15.jpegLONDON, England
TIMU za Manchester United na Arsenal leo zinakutana katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la FA.

Tayari kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amekiri kuwa mchezo huo utakuwa mgumu kutokana na uzoefu wa timu hizo katika mashindano hayo. Timu hizo ndizo zilizotwaa taji hilo mara nyingi.

Wenger alisema anaamini timu itakayoibuka na ushindi leo ndio itakuwa bingwa wa kombe hilo.

Mchezo huo utapigwa kuanzia saa 4:45 usiku kwa majira ya Afrika Mashariki.

“Ninauona huu ni mchezo mgumu na utakaotoa sura halisi ya ubigwa hasa ikizingatiwa kuwa atakayeibuka mshindi ndiye anayeweza kutwaa taji hili mwishoni, “alisema kocha huyo.

Aidha, nahodha wa Manchester United, Wayne Rooney atacheza mchezo huo huku akiwa na kumbukumbu ya mataji tisa, lakini katika vikombe hivyo, halipo la FA.

Rooney akiwa na timu hiyo mwaka 2005 wakati timu yake hiyo ilipocheza na Arsenal pamoja na mwaka 2007 ilipocheza na
Chelsea, haikuweza kushinda kombe hilo.

“Kwa miaka mingi hatujafikia hatua ya kucheza fainali kwa mchezo huu tunaweza kuondoa gundu na kufikia fainali kirahisi na kulitwaa taji hilo, ”alisema alisema Rooney.
Katika mechi nyingine ya michuano hiyo iliyochezwa usiku wa kuamkia leo, Liverpool ilibanwa nyumbani na Blackburn na sasa watarudiana kupata mshindi wa kuungana na timu ya Aston Villa iliyotangulia kwa kuilaza West Bromwich Albion.

Simba waitafuna Yanga Taifa, Okwiiiiii aleta maafa

Okwi (25) akishangilia bao na wachezaji wenzake

Raha ya ushindi
Elias Maguli akimtoka beki wa Yanga aliyeanguka
Na Rahma Junior
BAO pekee la kiufundi lililofungwa na Emmanuel Okwi katika dakika ya 51 limeiwezesha Simba kuizima Yanga katika pambano la Ligi Kuu Tanzania Bara.
Okwi, raia wa Uganda alifunga bao hilo baada ta kupenyezewa pande safi na Ibrahm Ajibu na kumchungulia kipa Ally Mustafa Barthez aliyekuwa ametoka eneo lake la kujidai na kupiga 'mashine' ya umbali wa mita 27 na kuiandikia Simba bao hilo.
Bao hilo liliwafanya wapenzi wa Yanga kulala mapema na kuwafanya viongozi na wanachama wa Yanga waliokuwa wakitamba mapema kwamba Simba si saizi yao kuzima simu zao.
Ushindi huo umeifanya Simba kuendelea kuwatesa Yanga ambao walitoka kuwtaungua kwenye mechi ya Nani Mtani Jembe 2 Desemba mwaka jana.
Simba imefikisha pointi 26 kwa ushindi huo na kushika nafasi ya tatu ikiwaengua Kagera Sugar, japo Yanga wanaendelea kuongoza msimamo wakiwa na pointi 31, moja zaidi ya Azam waliopo nafasi ya pili.
Dalili za Simba kuitambia Yanga zilianza kuonekana mapema kwenye uwanja wa Taifa, baada ya timu yao ya vijana U20 kuwanyuka wa Yanga mabao 4-2.
Katika mchezo huo Haruna Niyonzima alitolewa uwanjani kwa kadi Nyekundu baada ya kupewa kadi ya njano ya pili kwa kupiga mpira huku filimbi ya mwamuzi Martin Saanya wa Morogoro, ikiwa imepulizwa. 
Vikosi vilikuwa hivi:
SIMBA SC: Ivo Mapunda, Kessy Ramadhan, Mohhamed Hussein, Hassan Isihaka, Juuko Murshid, Abdi Banda/Simon Sserunkuma, Ramadhani Singano, Jonas Mkude, Ibrahim Ajib/ Elias Maguli, Said Ndemla na  Emanuel Okwi.
YANGA SC: Ally Mustafa,Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir Haroub, Kelven Yondani, Said Juma, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Amis Tambwe, Mrisho Ngassa/ Khap Sherman na Danny Mrwanda/ Hussein Javu.

AIBU! Mtoto mwingine albino akatwa kiganja Rukwa

http://ak2.picdn.net/shutterstock/videos/3573986/preview/stock-footage-close-up-of-bloody-knife-with-blood-dripping.jpg 
MATUKIO ya Ukatili dhidi ya albino yanaendelea kuwa tishio nchini Tanzania baada ya mtoto wa miaka sita kukatwa kiganja cha mkono.
Shambulio hilop jipya limetokea mkoani Rukwa kusini magharibi mwa nchi hiyo.
Mtoto huyo kiume Baraka Cosmas alikuwa amelala na mama yake mzazi wakati wahalifu hao walipovamia nyumba yao.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Rukwa Jackob Mwaruanda amesema kwa sasa mtoto huyo anapata matibabu hospitali na hali yake inaendelea vizuri.
Polisi inaendelea na uchunguzi kubaini wahusika.
Shambulio hilo linajitokeza wiki moja tu baada ya watuhumiwa wanne kuhukumiwa adhabu ya kifo kwa mauaji ya albino.
Pia ni muda mfupi baada ya Rais Tanzania Jakaya Kikwete kukemea mauaji ya albino, ambao viungo vyao hutumika katika shughuli za kishirikina kwa imani potofu kuwa zinasaidia kuleta utajiri na madaraka.
Kadhalika kukiwa kumeanzishwa kampeni maalum ya 'Inatosha' kukomesha mauaji hayo ya albino ambayo yameitia aibu Tanzania katika usoa wa dunia.

Saturday, March 7, 2015

Real Madrid yazmishwa ugenini, Sevilla yaua

Karim Benzema (left) and Cristiano Ronaldo look on as the Bilbao team celebrate scoring in the first half
HAWAAMINI KAMA WAMETUNGULIWA!
Bilbao striker Inaki Williams (second left) tries to keep the ball away from the approaching Madrid player Asier Illaremendi 
Hata Bale alishindwa kuibeba Real Madrid leo kwa Athletic Bilbao
KLABU ya Real Madrid imechezea kichapo cha bao 1-0 ugenini mbele ya Athletic Bilbao katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Hispania (La Liga) huku Sevilla wakishinda ugenini mabao 4-3 dhidi ya Deportivo la Coruna.
Bao pekee lililowazamisha Mabingwa wa Ulaya, liliwekwa kimiani kwa kichwa na Aduriz katika dakika ya 26 akimalizia kazi nzuri ya Mikel Rico.
Madrid ilikuwa na wakali wake wote akiwamo Cristiano Ronaldo, Gareth Bale, Karim Benzema, Isco, Ton Kroos na wengine ilishindwa kabisa kufuruka kwa wenyeji na kukubali kichapo hicho kilichowafanya wasaliwe na pointi zao 61 na kutoa nafasi kwa wapinzani wao wakuu Barcelona kuwapiku kama watashinda katika mechi yao ya kesho. Barcelona wana pointi 59,wakiwa wana mchezo mmoja pungufu zaidi ya Real Madrid.
Katika mchezo mwingine wa mapema, Deportivo la Coruna wakiwa nyumbani walizamishwa mabao 4-3 na Sevilla, huku kwa sasa pambano la ligi hiyo Elche ikiwa nyumbani inaongoza bao 1-0 dhidi ya Almeria na baadae Granada itaikaribisha Malaga.

Taifa Stars kuvaana na Malawi Machi 29

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEib4Geg2HzkrM8BDCTZpyd28JL_3avjxBBFaqs6CZXbhBFNXd34kYVHku38wroT3X297kNVt2VCkmx9rSLIMggDqH4wRuJ5ATjbIOGZ4lQ8txrgyljcmrIChSqjATeLt9tVQ0kvzxrFiQvm/s1600/Taifa+Stars+group+picture.JPG
Taifa Stars itakayovaana na Malawi katika pambano linalotambuliwa na FIFA
TIMU ya soka ya taifa, Taifa Stars inatarajiwa kushuka dimbani Jumapili ya Machi 29 mwaka huu, kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya taifa ya Malawi, The Flames.
Pambano hilo litachezwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Mchezo huo wa kirafiki ambao upo katika kalenda ya FIFA kwa timu za Taifa (Machi 23-31) na utatarajiwa kuanza majira ya saa 10 na nusu jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Wawili waumia Twiga Stars ikijianda kuvaana na Zambia

WACHEZAJI wawili wa timu ya Taifa ya wanawake, Twiga Stars, wameshindwa kufanya mazoezi kutokana na kuwa majeruhi kwenye Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam

Wachezaji ambao ni majeruhi ni Fatuma Khatib anayecheza beki ya kulia na Ziada Ramadhani beki wa kushoto na waliumia kwenye mchezo wa kirafiki wa timu hiyo dhidi ya timu ya makipa ikiwa ni maandalizi ya mchezo wa kufuzu Kombe la Mataifa Afrika dhidi ya Zambia Machi 22, mwaka huu.

Akizungumzia hali zao kocha wa Twiga Stars, Rogasian Kaijage alisema kuwa wachezaji hao wanaendelea na matibabu na anatarajia wiki ijayo watakuwa wamepona.

“Leo hawakufanya mazoezi kwa sababu wana maumivu, lakini natarajia mapema wiki ijayo watakuwa wamepona kwani wanaendelea vizuri na matibabu”, alisema Kaijage

Kaijage alisema kutokana na program ya mazoezi aliyoendesha tangu timu hiyo ianze kambi mwishoni mwa mwezi uliopita anatarajiwa kuwa na mchezo mmoja wa kujipima nguvu katikati ya mwezi huu.

Twiga Stars ambayo imeweka kambi katika Hosteli za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) zilizopo ndani ya Uwanja wa Karume, Ilala, Dar es Salaam imeingia moja kwa moja katika hatua ya pili kucheza na Zambia kufuatia kuwa na matokeo mazuri katika msimamo wa viwango vya soka la wanawake barani Afrika.

Wachezaji waliopo kwenye kikosi cha Twiga ni Asha Rashid, Esther Chaburuma, Fatuma Bushiri, Fatuma Hassan, Fatuma Mustapha, Fatuma Omari, Eto Mlenzi, Mwajuma Abdallah, Sofia Mwasikili, Zena Khamis, Mwanahamisi Omar, Fadhila Hamad, Anastazia Anthony na Shelder Boniface.

Wengine ni Thereza Yonna, Happines Hezron, Amina Ally, Donizia Daniel, Fatuma Issa, Vumilia Maarifa, Maimuna Hamisi, Najiati Abbas, Stumai Abdallah, Zuwena Aziz, Irene Joseph, Dawa Haji Vuai, Belina Julius na Amina Ramadhani.

Spurs yailipua QPR kwao yaipumulia Liverpool

.
Muunganiko wa picha zilizochapishwa na Daily Mail zikionyesha mpambano wa Spurs na QPR ulivyokuwa leo
MSHAMBULIAJI Harry Kane amefunga mabao mawili jioni ya leo na kuiwezesha timu yake ya Tottenham Hotspur kupata ushindi muhimu ugenini dhidi ya QPR katika mechi ya kiporo cha Ligi Kuu ya England.
Kane ambaye amekuwa moto wa kuotea mbali alifunga mabao hayo katika kila kipindi na kuifanya Spurs kufikisha pointi 50 na kupaa hadi nafasi ya sita nyuma ya Liverpool iliwatanguliwa kwa pointi 51.
Mshambuliaji huyo kinda alifunga bao la kwanza dakika ya 34 kabla ya kuongeza la pili dakika ya 68 na wenyeji wanaopambana kuepuka kushuka daraja ilip[ata bao la kufutia machozi kupitia Sandro katika dakika ya 75.

Jonny Evance, Papiss Cisse wafungiwa England

http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2015/03/06/2652640E00000578-2983103-Evans_left_and_Cisse_clash_near_the_half_way_line_at_St_James_Pa-a-1_1425663667950.jpgBEKI wa Manchester United, Jonny Evance na Mshambuliaji wa Newcastle United, Papiss Cisse, wamefungiwa kwa kitendo chao cha kutemeana mate katika pambano lililochezwa majuzi.
FA iliwafungulia mashtaka wachezaji hao baada ya awali mwamuzi wa pambano hilo kutoliona tukio halisi ya wachezaji hao kujigeuza 'nyota'kwa kutemeana mate.
Evance aliyekanusha shtaka lake amefungiwa mechi sita wakati mwenzake amefungiwa mechi saba ikiwamo sita ya kosa hilo na moja kwa kosa alililowahi kulifanya hivi karibuni la kumpiga mtu kiwiko.
Awali Cisse alikubali  mashitaka yaliyotolewa na Chama cha Soka cha Uingereza-FA kwa kumtemea mate beki wa Manchester United Jonny Evans.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 29, aliomba radhi kutokana na tukio hilo lakini amekanusha kama alifanya kwa makusudi.

Kiingilio Simba, Yanga Buku 7 tiketi zaanza kuuzwa

Yanga
Simba
TIKETI za pambano la kesho kati ya Simba SC na Young African litakaofanyika kwenye dimba la Uwanja wa Taifa kuanzia majira ya saa 10 kamili za jioni zimeanza kuuzwa kama ilivyotangazwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Mchezo huo wa kesho utachezeshwa na mwamuzi Martin Saanya kutoka Morogoro, akisaidiwa na Soud Lila (DSM) mshika kibendera wa kwanza, Florentina Zabron (Dodoma) mshika kibendera wa pili, Mwamuzi wa akiba Israel Mjuni (DSM), na kamisaa wa mchezo ni Ame Santimeya (DSM).
Viingilio vya mchezo huo, VIP A sh. 40,000, VIP B sh. 30,000, VIP C sh. 20,000, Rangi ya Machungwa (Orange) sh. 10,000, huku Rangi ya Bluu na Kijani ikiwa ni sh. 7,000.
Tiketi zimeanza kuuzwa leo Jumamosi saa 2 kamili asubuhi katika vituo vya, Karume (Ofisi za TFF), Mgahawa wa Steers (Posta Mpya), Oilcom (Buguruni), BigBon (Kariakoo), Olicom (Ubungo), Dar Live (Mbagala), Uwanja wa Uhuru, Kivukoni (Ferry) na Makumbusho (kituo cha mabasi).
Magari yenye vibali maalum ndiyo yatakayoruhusiwa kuingia ndani ya uwanja kesho Jumapili kwa kupitia barabara ya Mandela na Uwanja wa Uhuru, barabara ya Chang'ombe itafungwa kuanzia saa 12 kamili asubuhi.
TFF inawaomba, wapenzi, washabiki na wadau wa mchezo kununua tiketi katika vituo vilivyotajwa ili kuepuka kuuziwa tiketi bandia, ili kuimarisha ulinzi na usalama wa mchezo, mashabiki wenye mabegi, silaha, vilevi na chupa za maji hawataruhusiwa kuingia navyo uwanjani.
Aidha katika mchezo huo TFF itatoa ujumbe maalum kupitia kwa wachezaji kuhamasisha juhudi za Taifa za kuzuia mauaji dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino)

Azam yalipa kisasi JKT , Coastal yabanwa Tanga

Mfungaji wa bao pekee la Azam

BAO pekee kutoka kwa Mrundi, Didier Kavumbagu limeiwezesha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara kulipa kisasi kwa JKT Ruvu.
Azam walipata ushindi huo kwenye uwanja wa Chamazi na kuifanya timu hiyo kuzidi kuwapumulia Yanga waliopo kileleni ambao kesho watashuka dimbani kuvaana na Simba.
Kavumbagu alifunga bao hilo lililokuwa la tisa kwake msimu huu katika ligi hiyo katika dakika ya 17 akiunganisha mpira wa krosi ya beki Shomari Kapombe na yeye kuufungwa kwa kichwa.
Azam imefikisha pointi 30, moja pungufu na ilizonazo Yanga yenye 31 ambao kesho watakuwa vitani dhidi ya Simba kwenye uwanja wa Taifa/ Kati mechi ya mkondo wa kwanza JKT Ruvu ndiyo iliyokuwa timu ya kwanzsa iliyovunja rekodi ya Azam ya kushinda mechi mfululizo 38 baada ya kuichapa bao 1-0.
Katika mchezo mwingine uliochezwa leo mabingwa wa zamani wa soka nchini, Coastal Union kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Mkwakwani Tanga walilazimishwa sare ya mabao 2-2 na Kagera Sugar.
Mabao ya Coastal yalifungwa na Seleman Kibuta na Rama Salim wakati wageni walipata mabao yake kupitia kwa Atupele Green na Enock Kyaruzi.
Pambano jingine kati ya Polisi Moro dhidi ya Ruvu Shooting limeshindwa kufanyika mpaka siku ya Jumanne kutokana nna uwanja wa Jamhuri Morogoro kutumika na shughuli za sherehe za Siku ya Wanawake inayofikia kilele kesho Jumapili.