FA YAMFUNGIA NA KUMPIGA FAINI JOHN TERRY KWA UBAGUZI
John Terry na Anton Ferdinand wakigombana katika tukio linalodaiwa Terry kumbagua Ferdinand
Terry akiwasili mahakamani kutoa ushahidi wa tuhuma hizo na kisha kukutwa hana hatia
LONDON, England
Katika sakata hilo
ambalo lilifikishwa mahakamani na Terry kukutwa hana hatia, nahodha huyo wa
zamani wa England anadaiwa kumbagua beki wa klabu ya QPR, Anton Ferdinand
HATIMAYE Chama cha Soka cha England (FA), leo kimefikisha
tamati sakata la ubaguzi wa rangi lililokuwa likimkabili beki na nahodha wa Chelsea,
John Terry na kutoa huku iliyotabiriwa na mtuhumiwa huyo mapema wiki hii.
Katika hukumu yake iliyotoka jana, iliyokuja baada ya
mfululizo wa siku nne za kuhojiwa kwa nyota huyo na wakili wake kutoa ushahidi
wa kumtetea, FA imemfungia nyota huyo mechi nne na faini ya pauni 220,000.
Katika sakata hilo ambalo
lilifikishwa mahakamani na Terry kukutwa hana hatia, nahodha huyo wa zamani wa England anadaiwa kumtolea lugha za kibaguzi beki
wa kimataifa wa England
anayechezea klabu ya Queens Park Rangers, Anton Ferdinand.
Terry tayari alishakana kuhusika na tuhuma hizo anazodaiwa
kuzitoa Oktoba mwaka jana wakati wa mechi baina ya Chelsea na QPR na kusema kuwa, FA inajaribu
kukwepa ukweli uliomuacha huru kwenye Mahakama ya Westminster Magistrates.
Kutokana na kuhisi kuonewa na kutambua kama FA ilipanga
kumhukumu isivyo, Terry mapema wiki hii alitangaza kustaafu kuichezea timu ya
taifa ya England, kama
sehemu ya kutoa hisia zake kuwa FA kwamba haimtendei haki katika sakata hilo.
Akitangaza uamuzi wa kustaafu soka la kimataifa, Terry, 31, alisema:
“Natangaza rasmi leo kuwa nastaafu soka la kimataifa. Napenda kutoa shukrani
kwa makocha wote wa England
walionichagua mimi kuwamo dimbani na timu hiyo mara 78.
“Nimefanya maamuzi haya mapema kabla hata ya kusikia nini
kitaamuliwa juu yangu kwa tuhuma zinazonikabili kwa sababu nahisi FA, imepanga
hukumu isiyo ya haki dhidi yangu, licha uamuzi mzuri wa mahakama ulionisafisha
na tuhuma hizo.”
No comments:
Post a Comment