STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, September 29, 2012

KARAMA, CHEKA KUONYESHANA KAZI LEO PTA

Bondia  Fransic Cheka akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Karama Nyilawila  litakalofanyika leo Jumamosi katika ukumbi wa PTA, Sabasaba Dar es Salaam.

 Karama Nyilawila akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Fransic Cheka litakalofanyika leo Jumamosi katika ukumbi wa PTA, Sabasaba Dar es Salaam.


MABONDIA Francis Cheka 'SMG' na Karama Nyilawila 'Captain' leo wanatarajiwa kumaliza ubishi nani mbabe baina yao wakati watakapopanda ulingoni jijini Dar es Salaam kupigana katika pambano linalosaiwa kuwa la kuwania ubingwa wa Mabara wa shirikisho la UBO.
Pambano hilo la uzito wa super middle la raundi 12 lililoandaliwa na kampuni ya Afrika Kabisa chini ya usimamizi wa Shirikisho la Ngumi za Kulipwa nchini, PST, litafanyika kwenye ukumbi wa PTA.
Cheka aliyemshinda kwa pointi Nyilawila katika pambano lao lililopita lililofanyika Februari 28 mwaka huu, ametamba amejiandaa vya kutosha kushinda mchezo huo wa leo ili kulinda heshima yake kwa mashabiki kwa kumpiga mpinzan wake.
Nyilawila amesisitiza rekodi yake ya kutoshindwa mapambano ya ubingwa inamfanya aamini atashinda leo.
"Sijawahi kupigwa kwenye pambano lolote la kuwania ubingwa, hivyo nina imani hata kesho nitaendeleza ubabe kwa kumpiga Cheka na kulipiza kisasi cha kupigwa nae mapema mwaka huu akiwa kwao Morogoro," alisema jana Nyilawila.
Mratibu wa pambano hilo, Robert Ekerege, alisema litasindikizwa na michezo kadhaa ya utangulizi na burudani ya bendi ya Mashujaa.
Ekerege aliwataja mabondia watakaopigana katika utangulizi kuwa ni Seba Temba dhidi ya Stan Kessy, Juma Kihiyo atakayepigana na Ibrahim Mahokola, Anthony Mathias atakayechapana na Shaaban Kilumbelumbe na Cosmas Cheka dhidi ya Fadhil Awadh.
Mapambano mengine ya utangulizi ni Husseni Kidebe atakayepigana na Deo Samuel huku Amos Mwamakula akionyeshana kazi na Sadiki Momba.
Michezo yoye hiyo imedhaminiwa na kampuni ya Coca Cola Kwanza itakayouza soda zake za chupa za plastiki, na Dume Condoms.

No comments:

Post a Comment