MARUFUKU WAGOMBEA KUFANYA KAMPENI-TFF
SHIRIKISHO la soka Tanzania (TFF) limepiga marufuku kwa wagombea
uongozi wa Shirikisho hilo kufanya kampeni kwa sasa na atakayebainika kufanya
hivyo kamati ya uchaguzi itamuondoa kwenye kinyang’anyiro hicho.
Ofisa habari wa
TFF, Boniface Wambura alisema kwamba kampeni bado zimesimamishwa hivyo
hairuhusiwi mtu yoyote kufanya kampeni mpaka itakapoangazwa.
Msemaji wa TFF, Boniface Wambura |
“Tunapenda kuwakumbusha wale waliopitishwa kuwania nafasi
mbalimbali za uongozi TFF kutoendesha kampeni kwa sasa mpaka watakapopewa barua
za ruhusa hiyo na yeyote atakayekiuka kamati ya uchaguzi inamamlaka ya
kumuengua katika kinyang’anyiro hicho.
Hivi karibuni, kamati ya uchaguzi ya TFF chini ya
mwenyekiti wake Deo Lyatto ilitangaza kusitisha kampeni za wagombea wa uchaguzi
wa viongozi wa TFF uliopangwa kufanyika Februari 24 pamoja na ule wa bodi ya
ligi uliopangwa kufanyika Februari 22.
Aidha, kumekuwa na sintofahamu juu ya uchaguzi huo baada ya
hivi karibuni kuwepo kwa shinikizo la kutaka kurejeshwa kwa aliyekuwa mgombea
nafasi ya Urais wa TFF,Jamal Malinzi ambaye jina lake lilienguliwa na kamati ya
Rufaa.
Kitendo cha kuenguliwa kwa Malinzi kimeibua hisia tofauti
kwa wadau wa soka ambao kwa nyakati tofauti wameinyooshea kidole TFF juu ya
suala hilo kwa madai kwamba imeingiza mkono katika hilo, huku wakipanga kwenda
kuzuia uchaguzi huo magakamani iwapo hatarejeshwa kwenye kinyang’anyiro hicho.
Kama hiyo haitoshi, mmoja ya wagombea aliyeenguliwa katika
kuwania nafasi ya Makamu Mwenyekiti, Michael Wambura naye ameitaka TFF kuifuta
kamati ya Rufaa kwa madai kuwa si halali, huku akipendekeza uchaguzi huo
kufanywa kwa kufuata kanuni za zamani.
No comments:
Post a Comment