STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, May 9, 2013

Mwakyembe amcharukia Cheka, ataka asijitangaze hana mpinzani wakati anawapiga mabodia wa Dar tu

 
Bondia Benson Mwakyembe (kushoto) alipokuwa akipambana na Charles Kakande

BONDIA machachari wa ngumi za kulipwa, Benson Mwakyemba amemcharukia na kumuonya Bingwa wa IBF-Afrika, Francis Cheka kuacha mara moja kuwakebehi mabondia wa Tanzania akijipata kwamba hana mpinzani ilihali mabondia anaowapiga ni kutoka jijini Dar es Salaam tu huku wa mikoani akiwakacha.
Akizungumza na MICHARAZO mapema leo asubuhi, Mwakyembe ambaye anamtaka kwa udi na uvumba kuzipiga na bondia huyo kwa kile alichodai kuzima ubabe wa bingwa huyo, alisema Cheka hapaswi kutamba kwamba hana mpinzani wakati yeye amekuwa kiomba kucheza naye bila mafanikio.
Mwakyembe alisema dai kwamba hana mpinzani nchini siyo sahihi kwa vile mabondia anaopigana nao ni wa jijini Dar esa Salaam tu, wakati Tanzania ni kubwa na ina mabondia wa uzito wa kati lakini hawapewi nafasi ya kuonwa na Watanzania.
"Sijajua anatapa kigezo gani cha kujiona yeye ni bingwa asiye na mpinzani Tanzania wakati mabondia wa mikoani hataki kucheza nasi, mimi nimeshamuomba mara kadhaa na iliwahi kuandaliwa pambano na Shomar Kimbau mwaka juzi au nyuma yake, lakini alichomoa sasa anajiitaje hana mpinzani," alihoji Mwakyembe.
Bondia huyo mwenye maskani yake mkoani Ruvuma katika mji wa Songea alisema ni kweli Cheka ni bondia nzuri na fahari ya Tanzania, lakini ni lazima akubali kupambana na mabondia wa mikoani kaka yeye badala ya kuwarudia mabondia wale wale wa jijini ambao ameshajua udhaifu wao na kuwapiga kila mara.
Mwakyembe, madai kwamba yeye siyo wa kiwango cha Cheka, alisema hizo ni dharau kwa sababu yeye ni ameshacheza na kuwapiga Rashid Matumla, Joseph Marwa, Karama Nyilawila na kwenye orodha yupo nafasi ya 4 kati ya mabondia 15 wa uzito wa kati.
"Simuelewi anavytoa madai kwamba mimi siyo saizi yake, wakati katika orodha anayoongoza nipo nafasi ya nne, pia ni bingwa wa Afrika Mashariki na Kati kwa kumtwanga Mganda na majuzi tu nimetoka kupigana na Uensal Arik wa Ujerumani ambaye amemtwanga yeye Cheka nchini Ujerumani," alisema Mwakyembe.
Kauli ya Mwakyembe imekuja baada ya Cheka kudai kwamba hawezi kupigana na bondia yeyote nchini kwani wengi wao wanalilia kupambana naye lakini hawan uwezo kwenye ulingoni hivyo anaona kama ni kupoteza muda wake.
"wengine wanataka kufufukia na kupata uimaarufu kupita kwa Cheka, kwa nini hawapigani na mabondia wengine niliowapiga kama akina Mada Maudo, kaseba au Nyilawila, mpaka niwe mimi, nataka kupigana na mabondia wa nje kukuza jina na kuitangaza Tanzania, nyumbani naona sina mpinzani," alisema Cheka.
Cheka aliyetoka kumdunda bondia aliyekuwa hapigiki, Thomas Mashali katika pambano lake la kutetea taji la IBF Afrika, hajawahi kupigwa nchini Tanzania tangu mwaka 2008 akiwa ametoa vipigo kwa karibu mabondia wote wanaofahamika kwa umahiri wao ulingoni pamoja na wale wa kimataifa.

No comments:

Post a Comment