Vumbi akiwa katika pozi |
Vumbi akiwa jukwaani akifanya vitu vyake |
Mwanamuziki Alain Dekula kahanga 'Vumbi' katika pozi jingine |
BAADHI ya wasomaji waliingiwa na hofu baada ya kusoma taarifa ya Mwanamuziki nyota wa zamani wa bendi ya Orchestra Marquiz, Alain Dekula Kahanga 'Vumbi' iliyohoji unajua kafanya nini?
Ukweli ni kwamba mwanamuziki huyo anayefanya kazi zake kwa sasa nchini Sweden, amerekodi nyimbo sita mpya kwa ajili ya kujiandaa kupakua albamu mpya itakayokuwa ya tatu kwake.
Akizungumza na MICHARAZO kutoka Sweden, Vumbi mcharazaji mahiri wa gitaa la solo, mtunzi na muimbaji alisema nyimbo hizo zimerekodiwa katika studio tatu tofauti ikiwa maandalizi ya albamu hiyo mpya anayotarajiwa kuipakua mwaka huu.
Vumbi alizitaja nyimbo hizo zilizokamilika wiki hii ni pamoja na 'Dunia Kuna Mambo', 'Mashoga, 'Amy', 'Bombalaka', 'Amani' na 'Justice'.
Mwanamuziki huyo alisema amebakisha nyimbo mbili tu kuhitimisha albamu hiyo itakayokuwa na nyimbo nane.
"Nimetoka kukamilisha nyimbo zangu sita kwa ajili ya albamu mpya itakayokuwa ya tatu na nimebakisha nyimbo mbili ambazo tayari mashairi na mazoezi yamekamilisha isipokuwa bado zijazipa majina mpaka nitakapoenda kuzirekodi," alisema Vumbi.
Mkali huyo alisema nyimbo mbili kati ya hizo amerekodia katika studio za mwanamuziki wenzake wa zamani wa kundi lao la Makonde Band, Mganda Sammy Kasule na nne zilizosalia katika studio za SF zote zilizopo nchini Sweden.
Kuhusu jina la albamu Vumbi alisema bado hajajua aiite kwa jina lipi, ila mara akimalizia nyimbo hizo za mwisho atajua iitwe jina gani kabla ya kuanza kuitangaza kisha kuizindua.
Albamu za awali za mwanamuziki huyo mwenye asili ya Kongo ni 'Sultan Qaboos' na 'Rumazila' ambayo alikuja kuizindulia nchini mwaka juzi.
No comments:
Post a Comment