SHEIKH PONDA HURU AFUNGWA KIFUNGO CHA MWAKA MMOJA NJE
HATIMAYE katibu
wa Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda na
wafuasiwake 49 leo wameachiliwa huru na mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini
Dar es Salaam kufuatia kushinda mashtaka yote yaliyokuwa yakiwakibili. Hata
hivyo Sheikh Ponda amehukumiwa kifungo cha nnje mwaka mmoja kutokana na utetezi
wake kuonyesha kulikuwa na nia yakutenda kosa hilo.
Mara baada ya kutolewa hukumu hiyomahakamani hapo pali ibuka
shangwe za furaha kutoka kwa mamia ya wafuasi wake waliokuwa wamejazana karibu
na eneo la Mahakama hiyo.
Pamoja na maelezo yote aliyoeleza Jaji aliyesoma hukumu hiyo
alifafanua mambo mbalimbali kuhusu kiwanja kinachodaiwa na waisilamu hao.
1.Mahakama hiyo haina uwezo wakuzungumzia mmiliki halali wa
kiwanja kutokana na masuala ya migogoro ya aridhi kuwa na mahakama yake ingawa
imegundua kuna tatizo umiliki.
2.Upande wa Serikali hakuwa na hoja ya kisheria wala
ushahidi wa kutosha wakuwatia hatiani watuhumiwa.
3. Hati ya Mashataka ilikuwa na mapungufu mengi ya kisheria.
4.Hakimu awaonyesha njia yakudai mali hiyo waisilamu kutokana
na kile alichodai mali ya wakfu huwa haiuzwi wala haibadilishwi matumizi
yaliyokusudiwa.
5.Upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha kwamba
watuhumiwa waliopo mbele ya mahakama ni wafuasi wa sheikh Ponda. Awasihi Waisilamu
kufuata taratibu za kisheria ili kuipata mali hiyo halali itumike kwa madhumuni
yaliyokusudiwa.
Baada ya hukumu wafuasi wa sheikh Ponda wakitoka kwenye mahakama ya Kisutu. |
Tumewashinda! |
Furaha! |
Machozi yalitiririka, Jazba na ahawali zikapanda! |
Safari ya kuelekea Mtambani Kinondoni Ikaanza. |
Barabara nazo zikavamiwa na wafuasi hao. |
Mmoja wa ndugu wa mtuhumiwa akilia baada ya kumkumbatia
nduguyake kutokana na kushinda kesi hiyo.
|
"Pole ndio safari ya kusaka haki" Ndugu alisikika kabla ya kulia. |
Waliopo kwenye majengo ya karibu wakatoka nnje kushuhudia! |
Polisi wakiwa wamejipanga kwa tahadhari kwa lolote
litakalotokea.
|
No comments:
Post a Comment