Daktari
wa kwanza kabisa kumkimbilia Irine Cheptai akihaha kuuzindua moyo wake
baada ya kuzimia, alipokuwa akimaliza mbio za mita 3,000 kwenye Uwanja
wa Olimpiki jijini London jana.
Jopo
la Madaktari wakihangaika kumpatia huduma ya kwanza Irine Cheptai,
alianguka na kuzimia wakati akimaliza mbio za mita 3,000 kwenye Uwanja
wa Olimpiki.
Cheptai
akiwa ametungikiwa mtungi wa hewa ya oksijeni, baada ya kuanguka na
kuzimia kutokana na shambulio la moyo. Hata hivyo alikuja kurejewa na
fahamu zake akiwa hospitali.
Cheptai (wa pili kulia) akikimbia mbio za mita 3,000 kwenye Uwanja wa Olimpiki jijini London.
MKIMBIAJI wa mbio ndefu wa kimataifa wa Kenya, Irine Chebet
Cheptai jana alikimbizwa hospitali kwa matibabu baada ya kupatwa na mshituko wa
moyo kwenye Uwanja wa Olimpiki baada ya kumaliza mbio za mita 3,000.
Cheptai, binti wa miaka 21, alimaliza mbio akiwa nafasi ya 11,
katika muda bora zaidi katika rekodi yake binafsi, alipotumia dakika 8:56.20, lakini
akaanguka ghafla na kupoteza fahamu baada tu ya kuvuka mstari wa kumalizia.
Madaktari waliokuwa uwanjani hapo wakaharakisha kumtundikia
mtungi wa Oksijeni, ambapo kwa mujibu wa taarifa kuhusiana na tukio hilo
zilipasha kuwa alikuja kurejewa na fahamu akiwa hospitalini.
Tukio lake limeshtua wengi kutokana na kukimbia katika mbio
fupi kulinganisha na zile alizozoea za mita 5,000, ambazo ameshiriki Diamond
League mara mbili msimu huu, na anakumbukwa kwa rekodi yake ya dakika 14:50.99
jijini Shanghai, Mei mwaka huu.
Daily Mail
No comments:
Post a Comment