Na Suleiman Msuya
SERIKALI
kupitia Wizara ya Sheria na Katiba ipo katika mchakato wa kutunga sheria ya
Msaada wa Kisheria ambayo inalenga kuwasaidia wananchi na uwezo wa kulipia
gharama zinazotozwa na Mawakili wa kujitegemea.
Hayo
yamebainishwa Msemaji wa Wizara hiyo Farida Khalfan wakati akizungumza na
waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Alisema
Wizara ya Sheria mwaka 2010 iliiunda kikosi kazi ambacho kilishirikisha wadau
mbalimbali kufanya utafiti na kutoa mapendekezo juu ya mfumo sahihi ambao
utakidhi hitaji kwa kila raia.
Msemaji
huyo alisema baada ya kikosi kazi hicho kuwasilisha mapendekezo s.erikali
kupitia Wizara ya Katiba na Sheria ilianza utaratibu wa kutunga sheria
itakayojulikana kama (Sheria ya Msaada wa Kisheria)
Khalfan
alisema maandalizi ya sheria hiyo yapo katika hatua za mwisho ambapo matarajio
yao ni kuhakikisha kuwa sheria hiyo inawasilishwa Bungeni ifikapo Januari mwaka
2014.
“Tumekuwa
tukifuatilia changamoto ambazo zinawakuta wananchi hasa katika masuala ya
kisheria ila kutokana gharama kubwa ila tunaaamini kuwa mwakani utatuzi utakuwa
ukipatikana,” alisema.
Alisema
katika sheria hiyo itaunda chombo huru kitakachokuwa na majukumu mbalimbali
ambayo ni kusajili taasisi zinazotoa msaada wa kisheria, kusajili watoa msaada
wa kisheria, kuweka ubora wa viwango katika utoaji msaada wa kisheria na
kuvisimamia.
Khalfan
alisema pia chombo hicho kitasimamia nidhamu na maadili ya watoa huduma za
msaada wa kisheria, kutambua wasaidizi wa kisheria na kutafuta fedha ili
kutekeleza majukumu yake.
Alisema
matoke ya kuwepo kwa sheria hiyo ni dhahiri kuwa watoa msaada wa kisheria
atatakiwa kusajiliwa ili waweze kutoa huduma hiyo kupitia vituo vilivyosajiliwa
kutoa msaada huo.
Msemaji
huyo alisema kukosekana kwa sheria hiyo ndio sababu mojawapo ya kuwepo kwa watu
wasio na sifa za kutoa huduma hiyo ambao wanatambulika kama (Bush Lawyers)
ambao wamekuwa wakiwarubuni wananchi kuwa wanaweza kuwasaidia kisheria.
Alisema
kupita kwa sheria hiyo kutasaidia jamii mbalimbali kama watoto, wajane na watu
wote ambao wamekuwa wakipata shida ya msaada wa kisheria nchini kutokana na
gharama kubwa zinazotozwa na wanasheria .
No comments:
Post a Comment