KLABU
ya Manchester United leo inatarajia kuwakumbuka watu 23 ambao
walipoteza maisha katika ajali ya ndege jijini Munich Februari 6 mwaka
1958. Wachezaji nane wa United na viongozi watatu ni miongoni mwa
waliokufa wakati ndege iliyowabeba wachezaji wa timu hiyo kutoka katika
mchezo wa Kombe la Ulaya jijini Belgrade kushindwa kupaa. Ndege hiyo
ilitua jijini Munich kwa ajili ya kuongeza mafuta na baada ya kushindwa
kuruka mara mbili ndege hiyo ilipata ajali wakati ikijaribu tena kuruka
kwa mara ya tatu. Watu 21 walifariki katika eneo la tukio huku rubani
wake Kenneth Rayment alifariki wiki tatu baadae na Duncan Edwards ambaye
anahesabika kuwa mmoja wa wachezaji nyota kabisa wa Uingereza yeye
alifia hospitali siku 15 baadae. Golikipa
wa United Harry Gregg yeye alifanikiwa kutoka salama lakini alirejea
katika eneo la tukio kujaribu kuwaokoa majeruhi katika sehemu salama.
Wachezaji wawili Johnny Berry na Jackie Blanchflower wote walishindwa
kucheza soka tena kutokana na majeraha ya ajali hiyo.Mashabiki wa United
Sir Bobby Charlton na Gary Neville walifika Old Trafford
Sir Bobby Charlton na Gary Neville walifika Old Trafford
No comments:
Post a Comment