TIMU ya Taifa ya mpira wa miguu ya wanawake (Twiga Stars) imehamishia
kambi yake jijini Dar es Salaam kutoka Mlandizi mkoani Pwani ikiwa ni
sehemu ya maandalizi ya mechi ya michuano ya Afrika (AWC) dhidi ya
Zambia.
Kikosi hicho chini ya Kocha Rogasian Kaijage kimepiga kambi katika
hosteli ya Msimbazi Center kikiwa na wachezaji 25 kutoka 30 ambao
kilianza nao katika kambi ya Mlandizi mkoani Pwani.
Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya kwanza dhidi ya Zambia itachezwa
Februari 14 kwenye Uwanja wa Nkoloma jijini Lusaka. Timu zitarudiana
wiki mbili baadaye jijini Dar es Salaam.
Wachezaji waliopo katika kikosi hicho ni Amina Ally, Amisa Athuman,
Anastasia Anthony, Asha Rashid, Esther Chabruma, Eto Mlenzi, Evelyn
Sekikubo, Fatuma Bashiri, Fatuma Hassan, Fatuma Issa, Fatuma Mustafa na
Fatuma Omari.
Wengine ni Flora Kayanda, Happiness Hezron, Maimuna Said, Mwajuma
Abdallah, Mwapewa Mtumwa, Najiat Abbas, Pulkeria Charaji, Shelder
Boniface, Sophia Mwasikili, Therese Yona, Vumilia Maarifa, Winfrida
Daniel na Zena Khamis.
No comments:
Post a Comment