|
Kikosi cha Simba |
|
Kikosi cha Yanga |
KLABU za Simba na Yanga zimeingiza jumla ya Sh. Mil. 100 katika mechi zao za mwishoni mwa wiki viwanja vya ugenini.
Pambano lililowakutanisha wenyeji timu ya Stand United kwenye Uwanja wa Kambarage mjini
Shinyanga dhidi ya timu ya Simba umeingiza jumla ya Sh. Mil.31.
Jumla la watazamaji
5,439 waliingia uwanjani kushuhudia mchezo huo, ambao timu ya Stand imepata mgao
wa Sh. 6,564,268.22 na Simba wakipata mgao wa 4,661,581.78.
VAT (18%) tshs. 4,763,135.59
huku FA mkoa wakipata tsh.665,940.25,
FDF tsh. 1,141,611.86, Bodi ya Ligi tsh. 1,522,149.15, Gharama za mchezo tsh.
1,617,283.47, Uwanja tsh. 2,854,029.66, Gharama ya tiketi tsh. 1,593,000,00,
FDF tsh. 2,921,000.00, TFF tsh.2,921,000.00
Wakati kwenye uwanja wa
Sokoine Mbeya, jumla ya Sh. 74, 600,000.00, zilipatikana kutokana na watazamaji
14,920 waliokata tiketi kushuhudia mchezo huo, lililozihusisha wenyeji Mbeya City na Yanga.
Kwa mujibu wa mgao VAT(18%) tsh.11,379,661.02, CDRB (5%)
tsh.3,730.000.00, FDF tsh. 5,222,000,00, TFF tsh. 2,238,000.00, Uwanja tsh.
7,804,550,85, Gharama za mchezo tsh 4,442,578.81, Bodi ya Ligi tsh.
4,162,427,12.
Chama cha soka mkoa
(FA) Mbeya kimepata tsh. 1,821,061.86, FDF(TFF) tsh. 3,121,820.34, wenyeji timu
ya Mbeya city wakipata tsh. 17,950,466.95 na klabu ya Yanga tsh. 12,747,438.98.