STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, October 14, 2012

Messi aing'arisha Argentina

Lionel Messi wa Argentina


MENDOZA, Argentina
Lionel Messi aliiongoza Argentina kuilaza timu ngumu ya Uruguay katika nusu saa ya mwisho ya mchezo kwa mabao mawili ya kifundi katika ushindi wa 3-0 jana ambao umeibakiza kileleni mwa msimamo wa kundi la Amerika Kusini la michuano ya awali ya Kombe la Dunia.
Argentina inaongoza kundi la timu tisa la Amerika Kusini ikiwa na pointi 17 katika mechi nane ambazo ni nusu ya kampeni. Colombia na Ecuador zipo pointi moja nyuma, Uruguay na Chile tano nyuma yake.
Messi alitengeneza na kumalizia goli lake la kwanza katika dakika ya 66, alipotoa pasi kwa Angel Di Maria kabla ya kukimbia kwenda kuusukumizia wavuni mpira huo uliompita Fernando Muslera.
Argentina ilipata bao la pili dakika tisa baadaye kwa muvu nyingine kwenye wingi ya kushoto, Messi akimpa pasi tena Di Maria ambaye alirudisha mpira huo kwa 'tachi' ya kwanza ambapo Sergio Aguero aliugusa na kutumbukia nyavuni.
Goli la tatu katika dakika ya 80 lilitokana na mpira wa kijanja wa adhabu ndogo wa Messi, ambaye aliudanganya ukuta wa Uruguay kwa kupitisha mpira huo chini yao na kufunga wakati wenyewe wakiruka wakitaraji atalenga lango kwa juu.
Kilikuwa kisasi kizuri kwa Messi, ambaye sasa amefunga magoli 12 katika mechi saab zilizopita za timu ya taifa, na Argentina ambayo ilitolewa na Uruguay kwa penalti katika fainali za mwaka 2011 za Copa America ambazo washiriki hao wa nusufainali ya Kombe la Dunia mwaka 2010 walikuja kutwaa ubingwa.
Reuters

No comments:

Post a Comment