Onesmo Waziri 'Ticotico' (4) wa Golden Bush akitafuta mbinu za kumtoka mchezaji wa wahenga Fc (kulia) huku Abdallah Msheli akiwa tayari kumsaidia |
Katina George (14) wa Golden Bush akijaribu kufunga bao mbele ya msitu wa mabeki wa Wahenga Fc katika pambano lao lililochezwa jana Sinza, Dar es Salaam. |
NYOTA wa zamani wa klabu za Simba na Yanga jana walishindwa kutambiana baada ya timu walizokuwa wakizichezea za Golden Bush na Wahenga Fc kutoshana nguvu ya kutoka sare ya 1-1 katika pambano la kirafiki.
Wazir Mahadhi, Abdul Ntiro, Ally Yusuf 'Tigana', Abdallah Msheli na Steven Marashi walioichezea Golden Bush ya Mabibo walishindwa kuwazidi ujanja wenzao Mengi Matunda na Madaraka Seleman 'Mzee wa Kiminyio' wa Wahenga ya Sinza katika mchezo huo uliochezwa uwanja wa TP, Sinza.
Nyota hao walionyesha bado wamo katika usakataji soka kwa jinsi walivyokuwa wakikimbiza dimbani ili kuzisaidia timu zao, lakini mpaka wakati wa mapumziko Wahenga ndio waliokuwa wakiongoza kwa bao 1-0.
Bao lao lilifungwa na Mohammed Ibrahim katika dakika ya 38 baada ya kufanikiwa kuihadaa ngome ya Golden Bush iliyokuwa chini ya Msheli na kumchambua kipa Steven Marashi kwa shuti la karibu.
Kipindi cha pili Golden Bush chini ya nahodha wake Onesmo Wazir 'Ticotico', iliingia kwa kasi baada ya kufanya mabadiliko kadhaa na kufanikiwa kurejesha bao hilo katika dakika ya 64 kupitia Dau 'Messi' aliyemegewa pande zuri Ally Yusuf 'Tigana'.
Licha ya timu zote kushambuliana kwa zamu na kufanya kosa kosa nyingi, mpaka kipyenga kilichokuwa kikipulizwa na Ally Mayay Tembele kilipolia matokeo yalikuwa yamesalia kama awali kwa timu hizo kutoka sare ya bao 1-1.
Mwisho
No comments:
Post a Comment