Afisa Mipango Miji wa Ilala, Paul Mbembela akisisitiza jambo alipozungumza na wakazi za Kitunda |
Baadhi ya watu waliohudhuria mkutano huo |
Mmoja wa wakazi wa Kitunda akiuliza swali ili apate ufafanuzi juu ya hatma ya makazi yao katika eneo wanaloishi |
Aidha serikali na Manispaa hiyo ya Ilala imeweka bayana kwamba haitakuwa na huruma wala kuwaonea haya wavamizi wa maeneo hayo ya shuleni wakati wa zoezi la kuwaondoa kwa lazima.
Afisa Mipango Miji wa Ilala, Paul Mbembela, ndiye aliyeyasema hayo juzi katika mkutano wa pamoja kati ya ofisi yake na wakazi wa Kitunda, nje kidogo ya Dar es Salaam.
Mbembela alisema Manispaa haitakuwa na huruma na wale wote waliovamia na kujenga ndani ya maeneo ya shule kwa madai waliofanya hivyo wamevunja sheria na hawapaswi kuchekewa.
"Tutakuwa wakali kwa wale wote waliovamia na kujenga katika maeneo ya shule, kuchekea jambo hilo ni kutaka kuwafanya vijana na watoto wete wawe mbumbumbu kwa kushindwa kusoma katika mazingira mazuri," alisema.
Aliongeza kuwa, wananchi wote wanaojitambua kuwa wamefanya hivyo waanze mapema kuchukua uamuzi wa kuondoka wenyewe kwa hiari katika maeneo hayto kabla ya Manispaa ya Ilala haijaenda kuwatoa kwa nguvu.
Afisa huyo, alisema kumekuwa na desturi ya watu kuvamia maeneo ya shule ya kuweka makazi au sehemu za biashara na kusababisha wanafunzi kushindwa kusoma kwa utulivu, kitu ambacho Manispaa yao haipo tayari kuvumilia.
Alisema wananchi wanapaswa kutambua kuwa shule ni moja ya vitu muhimu vinavyopaswa kutochezewa kwani ndiko kunakozalisha viongozi na wataalam kwa baadaye wa taifa hivyo kila mmoja ana jukumu la kuzilinda shule.
Mwisho
No comments:
Post a Comment