STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, December 19, 2014

Hawa ndiyo walioingia na kutoka katika dirisha dogo la usajili Bara

http://darcitycenter.com/wp-content/uploads/2014/12/IMG_0173.jpg
Kpeh Sean Sherman aliyetua Yanga
http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2014/11/54.png
Pascal Wawa aliyetua Azam

http://static.goal.com/227600/227665_heroa.jpg
Dan Sserunkuma aliyetua Simba
http://api.ning.com/files/xMCtlOLhuRdvIKJ4IqlKQo5swrvUDSiogHOrPOVEYWIequGvkbAoW7Wk7MyessH-3CcKu48nulnsNIcpKw9FPSciLbck8jnD/SIMBANAYANGA4.jpg
Tambwe katemwa Simba na kuibukia Yanga
DIRISHA Dogo la Usajili nchini Tanzania, lilifungwa rasmi siku ya Jumatatu baada ya pilikapilika ya klabu za soka kupigana vikumbo kuingia hapa na kutoka kule kusaka wachezaji wa kuimarisha vikosi vyao.
Kwa sasa mashabiki wanasubiri kusikia nani na nani waliopitishwa katika klabu zao, baada ya majina kuwasilishwa kwenye ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania, TFF.
Katika heka heka hizo za usajili kuna mambo ya kushangaza yaliyojitokeza ikiwamo kwa aliyekuwa Mchezaji Bora wa mwezi (Septemba), Antony Matogolo, kiungo mkali wa Mbeya City kupelekwa kwa mkopo katika timu ya Daraja la Kwanza ya Panone ya Kilimanjaro ili tu kuongeza kiwango chake, huku Deo Julius alivunjia mkataba baada ya dirisha la usajili kufungwa.
Kama hiyo haitoshi, Mbeya City pia iliamua kumtoa Mfungaji Bora wa FDL 2012/13 Saad Kipanga waliyemsajili katika dirisha dogo la msimu uliopita kutoka Rhino Rangers kwend kukuza kiwango chake Polisi Tabora ya Daraja la Kwanza. Kipanga aliyeifungia mabao 12 katika mechi 14 Rhino na kuipandisha Ligi Kuu, alikuwa akiwaniwa kwa udi na uvumba na Simba SC msimu huu lakini dili lake lilikwama.
Cha kushangaza kingine ni Yanga kumtema mkali wao wa mabao Hamis Kiiza 'Diego' na kumsajili mchezaji toka Liberia ambaye hakuna mwenye hakika kama ataibeba timu hiyo kama ilivyokuwa kwa Mganda huyo, huku watani zao wakitoa kali ya mwaka kwa kumtema Mfungaji Bora wa msimu uliopita, Mrundi Amissi Tambwe.
MICHARAZO inakudondolea baadhi ya walioingia na kutoka katika dirisha hilo dogo la usajili kwa ajili ya Ligi Kuu Tanzania Bara, pia majina ya walioombewa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) baada ya dirisha dogo la usajili msimu wa 2014/2015 kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Tanzania, TFF kama alivyoweka bayana Mkurugenzi wa Mashindano wa shirikisho hilo, Boniface Wambura.
Wambura alidokeza kuwa wachezaji 15 kutoka nje wameombewa ITC kutoka nchi mbalimbali na kufafanua kuwa, Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF itakutana muda wowote kupitia usajili wa dirisha dogo ili kuweka mambo hadharani nani karuhusiwa kucheza wapi kutoka wapi na yupi amekwama.
Walioombwewa ITC kwa timu za Ligi Kuu ni Abdulhalim Humoud kutoka Sofapaka ya Kenya kwenda Coastal Union, Brian Majwega kutoka KCC (Uganda) kwenda Azam FC, Castory Mumbara kutoka Three Star Club (Nepal) kwenda Polisi Mara, Charles Misheto kutoka SP Selbitiz (Ujerumani) kwenda Stand United na Chinedu Michael Nwankwoeze kutoka Nigeria kwenda Stand United.
Dan Sserunkuma kutoka Gor Mahia (Kenya) kwenda Simba, Emerson De Oliveira Neves Roque kutoka Bonsucesso FC (Brasil) kwenda Yanga, Halidi Suleiman kutoka Flambeau (Burundi) kwenda Stand United na Juuko Murshid kutoka SC Victoria University (Uganda) kwenda Simba.
Kpah Sean Sherman kutoka Aries FC (Liberia) kwenda Yanga, Meshack Abel kutoka KCB (Kenya) kwenda Polisi Morogoro, Moussa Omar kutoka Flambeau (Burundi) kwenda Stand United, Nduwimana Michel kutoka Flambeau (Burundi) kwenda Stand United, Serge Pascal Wawa kutoka El Merreikh (Sudan) kwenda Azam na Simon Sserunkuma kutoka Express FC (Uganda) kwenda Simba.
Orodha kamili ya waliosajiliwa katika dirisha dogo lipo kama ifuatavyo;

AZAM;
Walioingia: Serge Pascal Wawa, Bryan Majwega na Amri Kiemba.
Waliotoka: Ismail Diara raia wa Mali (katemwa) na Mhaiti Lionel Saint-Preux (katemwa).

COASTAL UNION;
Walioingia: Humud na Geofrey Wambura (huru), Bakari Thabit (Friends Rangers).
Walioondoka: Razak Khalfan (mkopo Mwadui FC), Peter Heri (katemwa).

JKT RUVU: hakuna aliyeingia waka kutoka safari hii.

KAGERA SUGAR; hakuna aliyeingia wala kutoka.

MBEYA CITY;
Walioingia: Kalyesubula Hannington (huru), Juma Issa ‘Nyoso’ (huru), Idrisa Rashid, Fredy Cosmas, Soneka Peter (U20) na Selemani Hassan (U20).
Walioondoka: Anthony Matogolo (mkopo Panone FC), Saad Kipanga (mkopo Polisi Tabora), Ramadhani Abdu (mkopo Majimaji FC), Medson Mwakatundu – U20 (mkopo Rhino Rangers), Ramadhani Kapela – U20 (mkopo Coca Cola Mbeya), Majid Shabani – U20 (mkopo Coca-Cola Mbeya), Abdalah Said – U20 (mkopo Coca-Cola Mbeya) na Waziri Ramadhani – U20 (mkopo Burkinafaso FC) na Deo Julius (Aliyesitishiwa mkataba).

MGAMBO JKT; hakuna aliyeingia wala kutoka.

MTIBWA SUGAR;

Walioingia: Henry Joseph (huru) na Miraj (mkopo Simba) na Ibrahim Jeba (huru).
Walioondoka: Hassan Kessy (Simba).

NDANDA;
Walioingia: Omega (Yanga), Kiggi Makasi (huru), Stamili Mbonde (Villa Squad), Raymond Zabron (Villa Squad), Issa Said (huru), Mohamed Masoud 'Chile' (huru) na Zuberi Ubwa (huru).
Walioondoka: Amri Msumi (mkopo Kurugenzi Iringa) na Hamis Saleh (huru).

POLISI MORO;
Walioingia: Said Bahanunzi (Yanga), Zahoro Pazi (huru), Meshack Abel (KCB, Kenya) na Iman Mapunda (huru). Walioondoka: Danny Mrwanda (Simba), Makungu Siame (mkopo Malindi, Unguja), Emilian Mgeta (mkopo Villa Squad) na Mosses Mtitu (Majimaji FC).

PRISONS-MBEYA; hakuna aliyeingia wala kutoka.

RUVU SHOOTING;
Walioingia: Mwita Kimaronge (Toto Africans), Betram Mwombeki (huru), Yahya Tumbo (Mtendeni FC, Zanzibar) na Ally Yusuph (Ruvu Shooting B).

STAND UNITED;

Walioingia: Hamis Thabit (Yanga), Chanongo (Simba), Nduwimana (Burundi), Shaban Kondo, Chinedu, Hamis Shengo na Misheto (Ujerumani).
Walioondoka: Nelson Kimath na Omar Mtaki (wote Geita FC), Hussein Chepe na Lucas Charles (wote Polisi Tabora), Robert Magadula na Patrick Mrope (wamevunja mikataba).

SIMBA;
Walioingia: Dan Sserunkuma, Simon Sserunkuma, Murshid na Hassan Kessy (Mtibwa Sugar).
Walioondoka: Kiemba (Azam), Miraj Adam (mkopo Mtibwa Sugar), Haroun Chanongo (mkopo Stand United), Joram Mgeveke (mkopo Mwadui FC) na Uhuru Seleman (Mwadui FC – Uhuru kavunja mkataba Simba).

YANGA;
Walioingia: Sherman, Amissi Tambwe, Danny Mrwanda, Athuman Majogo (Friends Rangers) na Emerson (amesajiliwa na kutemwa).
Walioondoka: Hamis Kiiza (katemwa), Omega Seme (mkopo Ndanda FC), Hamis Thabit (mkopo Stand United), Geilson Santos Santana ‘Jaja’ (ametemwa) na Said Bahanunzi (mkopo Polisi Morogoro).

No comments:

Post a Comment