Kikosi cha Simba a.k.a Mnyama |
Rais wa Simba, Evance Aveva anayetatarajiwa kuzungumza na wanahabari leo |
Wachezaji Simba wakishangilia ushindi wao dhidi ya Yanga katika Nani Mtani Jembe |
Aveva anayetoka Kundi la Matajiri wa Simba (FoS), aliahidi kuzungumza na waandishi wa habari kwa kina juu ya suala linalotajwa la Simba Ukawa wanaohusishwa na matokeoa mabaya ya timu hiyo iliyoifunga Yanga SC Jumamosi.
Hamphrey Nyasio, Msemaji wa Simba SC, amesema Aveva atavunja ukimya juu ya Simba Ukawa na masuala mengine mengi yanayoihusu klabu hiyo.
Simba imekuwa na mwanzo mbaya katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu huu ikitoka sare katika michezo sita ya awali kabla ya kushinda 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mechi yao ya raundi ya saba.
Wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Simba SC, Aveva alikuwa na sera ya vidole vitatu kila mkono akimaanisha kila mechi pointi tatu na magoli matatu lakini sera hiyo inaonekana kufeli katika mechi zote zilizopita tangu aingie madarakani kwani Simba haijawahi kuonja ushindi huo
katika hatua nyingine baada ya kuacha kilio Jangwani, kikosi cha Simba kinaingia kambini jijini Dar es Salaam leo kabla ya keshokutwa kwenda Zanzibar kujiandaa kwa mechi ya ufunguzi wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar.
Simba, iliyoichapa Yanga mabao 2-0 katika mechi ya 'NanI Mtani Jembe 2' iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Jumamosi na kumfukuzisha kazi kocha Mbrazil Márcio Máximo, itakuwa na kibarua kigumu mbele ya kikosi cha Kagera Sugar katika mechi ya raundi ya nane ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Desemba 26.
Kocha wa Simba, Mzambia Patrick Phiri alisema jijini kuwa kikosi chake kinaingia kambini leo kwenye Hoteli ya Ndege Beach kabla na baadaye Jumapili kitarejea visiwani Zanzibar kuandaa dozi kwa ajili ya kukiua kikosi cha kocha Mganda Jackson Mayanja cha Kagera Sugar kilichoifunga Yanga bao 1-0 katika mechi ya raundi ya sita ya VPL msimu huu.
Simba iko nafasi ya saba katika msimamo wa VPL ikiwa na pointi tisa, moja nyuma ya Kagera Sugar wanaokamata nafasi ya tano.
No comments:
Post a Comment