Jerry Muro Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Yanga |
KLABU ya Yanga imetangaza watendaji wake wapya wa kuajiriwa na kuweka hadharani taarifa za kumtema rasmi kocha Marcio Maximo na msaidizi wake Leornado Nieva.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro, klabu yao imemuajiri Dk Daktari Jonas Tiboroha kuwa Katibu Mkuu kuchukua nafasi ya Beno Njovu.
Njovu ameondoka Yanga baada ya mkataba wake
kwisha na amekuwa akiendelea na shughuli zake mbalimbali kwa kuwa alihitaji
muda zaidi.
Mbali na DK Tiboroha ambaye ni mhadhiri katika vyuo vikuu mbalimbali vya ndani na nje
ya Tanzania, aliyewahi kufanya kazi
Norway na Sweden, pia wengine waliolamba shavu Jangwani ni Muro mwenyewe aliyekuwa mtangazaji wa zamani wa ITV na TBC.
Wengine ni Omar Kaya anayekuwa Mkuu wa Idara ya Masoko , Frank Chacha-Idara ya Sheria na Baraka Deusdedit anayekuwa Mkuu wa Idara ya Fedha.
Pia imefahamika wazi kuwa kocha Maximo na msaidizi wake wametimuliwa klabu hapo na nafasi zao kushikwa na 'Babu' Hans van der Pluijm na Charles Boniface Mkwasa 'Master'.
Makocha hao awali waliwahi kuinoa Yanga kwa nusu msimu uliopita kabla ya kupata kazi Umangani na kutimkia huko na sasa wanarudi kuendeleza libeneke.
No comments:
Post a Comment