KIUNGO nyota wa klabu ya Arsenal, Mesut Ozil amebainisha kuwa anakaribia kurejea kutoka katika majeruhi yaliyokuwa yakimsumbua na kusisitiza ataweza kubadilisha mwelekeo wa timu hiyo.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani amecheza mechi tisa pekee msimu huu, baada ya kupata majeraha ya goti mwezi Oktoba mwaka huu.
Arsenal imekuwa ikiyumba toka kuumia kwa nyota huyo wa zamani wa Real Madrid ambapo kwasasa wanashika nafasi ya sita katika msimamo wa Ligi Kuu.
Ozil aliuambia mtandao wa klabu hiyo anafanya bidii kila siku ili aweze kuwa fiti na hadhani kama itakuwa ni kipindi kirefu sana kabla ya hajarejea tena uwanjani.
Ozil aliendelea kudai kuwa ana matumaini ya kurejea mazoezini tena haraka iwezekanavyo ili aweze kuisaidia timu yake.
Arsenal ina kibarua kizito Jumapili hii pale watakaposafiri kuifuata Liverpool katika Uwanja wa Anfield na ushindi katika mchezo huo utakuwa muhimu ili kuwaweka katika nafasi nzuri ya kukaa katika nafasi nne za juu katika msimamo wa ligi
No comments:
Post a Comment