Kesho Mambo yatakuwa kama haya kwa wanaridha mbalimbali kuchuana Karatu Marathon |
Mratibu wa tamasha hilo ambalo mbali na riadha, ambao ndio mchezo mkuu, michezo mingine inayoshindaniwa ni pamoja na soka, mpira wa wavu na mbio za baiskeli, Meta Petro alisema kuwa mbio za mwaka huu zitakuwa na msisimko wa aina yake.
Akizungumzia mbio za kilometa 10 na zile za kilometa tano na 2.5 kwa wanaume, wanawake na watoto, Petro alisema kuwa mwaka huu msisimko ni mkubwa sana kwa washiriki na ushindani utakuwa wa aina yake.
Alisema tayari zaidi ya wanariadha 200 hadi juzi walikuwa wamejiandikisha kushiriki mbio hizo za wanaume na wanawake, huku watoto wa shule wenyewe wakitarajia kujisajili mapema leo asubuhi muda mfupi kabla ya kuanza kwa mbio hizo.
Alisema kuwa mbio za baiskeli zitakuwa za kilometa 60 kwa wanawake na wanaume huku, fainali za soka na mpira wa wavu zilitarajiwa kufanyika jana na washindi wake kuzawadiwa leo na mgeni rasmi, ambapo zawadi za fedha taslimu, jezi na mipira hutolewa kwa washindi.
Meta alisema kuwa mingoni mwa wanariadha nyota waliothibitisha kushiriki mbio hizo ni bingwa wa Uhuru Marathoni Fabiano Joseph aliyeng’atwa kidole gumba na mshiriki mwenzake baada ya kumaliza mbio hizo.
Alizitaja klabu za riadha zitakazoshiriki mbio hizo ni pamoja na Magereza, Jambo, Winning Spirit, Arusha Sports Training Centre (ASTC), Ambassador, Hakika na Polisi Kilimanjaro.
Wakati klabu zingine ni pamoja na Magereza na Mukojope zote za Zanzibar, CCP Moshi, TPC Moshi, Guwangw ya Mbulu na Manyara Athletics Club ya Babati.
Meta aliongeza kuwa pia watakuwepo wanariadha wengi binafsi kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo Arusha, Singida na kwingineko.
Mbio za Karatu zimekuwa zikiandaliwa na Filber Bayi foundation (FBF) na kudhamiwa na Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) kupitia Kamati ya Olimpiki ya Tanzania (TOC).
No comments:
Post a Comment