WATU
zaidi ya 8 wamenusurika kifo wakati wakiwa wamelala nyumbani mwao mtaa
wa Heri manispaa ya Tabora, baada ya gari la mizigo aina ISUZU
kuparamia nyumba yao, lilipomshinda dereva alipokuwa akikata kona,
ambapo mama mjamzito aliyenusurika amekimbizwa hospitalini akiwa na hali
mbaya kutokan a na mshituko na hali yake ya ujauzito.
Mashuhuda
wa ajali hiyo walioharibiwa thamani zao mbali mbali wamesema kuwa,
umefika wakati serikali kubadili adhabu za madreva wazembe ambao
wanaendesha vyombo vya usafiri bila kuzingatia sheria zilizowekwa na
serikali huku wakipoteza maisha ya wananchi na mali zao.
Akizungumza
juu ya ajali hiyo na kubaini uzembe wa dereva wa gari hilo lenye namba
za usajili t 396 AGS, ambaye hakupatikana mara moja, kamanda wa polisi
mkoani tabora kamishina msaidizi Suzani Kaganda aliyefika eneo la ajali
hiyo amesema kuwa, mwendesha gari hilo atatafutwa na hatua stahiki
zitachukuliwa dhidi yake.
Aidha
mmiliki wa nyumba hiyo bw.Ramadhani Musa Kaswezi, anayeishi kijijini
ilolangulu hakusema lolote akidai kikao cha familia kitatoa maamuzi ili
kuelezea hatua atakazochukua kutokana na wapangaji wake wawili kubolewa
nyumba.
No comments:
Post a Comment