STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, December 19, 2014

Manchester City kuikamata Chelsea kesho?

http://news.bbcimg.co.uk/media/images/64785000/jpg/_64785248_goal-getty.jpgMABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya England, Manchester City ambayo imerudi katika kasi itakuwa na nafasi ya kutoa presha kubwa katika mbio za ligi hiyo dhidi ya vinara Chelsea kwa mara ya kwanza msimu huu endapo kesho watashinda dhidi ya Crystal Palace.
Wakati Chelsea haitacheza dhidi ya Stoke City hadi Jumatatu, ushindi wa City kwenye Uwanja wa Etihad dhidi ya Palace ambayo imeshindwa kuibuka na ushindi kwenye mechi nne za Ligi Kuu, itakifanya kikosi hicho cha Manuel Pellegrini kufikisha pointi 39 ambazo ni sawa na za vijana wa Jose Mourinho.
Msimu huu vinara Chelsea wamewahi kuongoza kwa pointi nane zaidi, lakini City imeshinda mechi tano za mwisho za Ligi Kuu, wakati Frank Lampard alifunga na kuiwezesha timu hiyo ya Pellegrini kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya timu inayoburuza mkia ya Leicester City mwishoni mwa wiki iliyopita hivyo kuikaribia kwa pointi.
Hata hivyo, City itashuka uwanjani bila kumenyana na timu hiyo inayoshika nafasi ya 16 katika ligi, bila mshambuliaji wao Sergio Aguero, Stevan Jovetic na Edin Dzeko, wakati pia nahodha na beki wa kati Vincent Kompany naye akikumbwa na majeraha kwenye mechi dhidi ya Leicester.
Lakini licha ya lundo hilo la majeraha katika safu ya ushambuliaji, Pellegrini anaamini kikosi chake kitapata wachezaji sahihi wakuwasaidia kuibuka na ushindi dhidi ya Palace.
"Wiki hii tutafanya kazi na wachezaji ambao wataweza kucheza nafasi hiyo," Pellegrini aliwaambia wanahabari. "Kwa kipindi hiki tunajaribu kuwaweka fiti wachezaji wote kwa sababu hatuna mshambuliaji.
"David Silva, Samir Nasri na wengine waliobaki pia wanafunga hivyo lazima tuone katika wiki njia gani iliyo sahihi kucheza kwa siku zijazo hadi washambuliaji wetu watakapokuwa fiti."

No comments:

Post a Comment