STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, October 15, 2012

CAMEROON NJE TENA MATAIFA YA AFRIKA, YATOLEWA NA CAPE VERDE

Cameroon

CAMEROON imekosa tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani kwa mara ya pili mfululizo, baada ya visiwa vya Cape Verde kwa jumla ya mabao 3-2. Jana Camroon imeshinda mabao 2-1 katika mchezo wa marudiano dhidi ya Cape Verde mjini Yaunde.
Ikumbukwe Cape Verde iliilaza Cameroon 2-0 katika mechi yao kwanza, hivyo wenyeji jana walitakiwa washinde si chini ya 3-0 ili kusonga mbele.
Cape Verde sasa imeweka historia kwa kufuzu mara ya kwanza kwenye fainali hizo za kuwania kombe la Mataifa Afrika, zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.
Katika mechi nyingine ya kufuzu, Ethiopia ilivaana na Sudan ambapo Ethiopia imeibuka na ushini wa mabao 2-0. Katika mechi ya kwanza Sudan ilishinda 5-3. Ethiopia sasa imufuzu kupitia kwa sheria ya bao la ugenini baada ya timu hizo kufungana jumla ya mabao 5-5.
Mechi kati ya Senegal na Ivory Coast ilivunjika juzi baada ya mashabiki wa soka kuzua ghasia wakati wa mechi hiyo mjini Dakar.
Mashabiki hao wa Senegal, waliwasha moto na kuanza kurusha mawe uwanjani wakati Ivory Coast, ilikuwa ikiongoza kwa mabao 2-0, matokeo ambayo yangeiondoa timu yao. Mashabiki wa Ivory Coast, walilazimika kuingia uwanjani ili kukwepa ghasia hizo.
Wachezaji na mashabiki hao wa Ivory Coast walisindikizwa na Polisi wa kupambana na ghasia ambao walirusha mabomu ya machozi ili kuwatawanya mashabiki wa Senegal.
Ripoti zinasema watu 10 akiwemo Waziri wa Michezo wa Senegal, Hadhi Malick Gakou, walijeruhiwa kwenye vurugu hizo zilizotokea katika Uwanja wa Leopold Sedar Senghor.
Ghasia hizo zilianza wakati mshambuliaji nyota wa Ivory Coast, Didier Drogba, alipofunga bao lake la pili kwa mkwaju wa penalti, huku zikiwa zimesalia dakika 15 mechi hiyo kumalizika.
Kama mechi hiyo ingelimalizika matokeo yakiwa hivyo, Ivory Coast ingeliibuka na ushindi wa jumla wa mabao 6-2 na kusonga mbele.
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) halijatoa taarifa yoyote kuhusiana na tukio hilo, lakini maafisa wa Shirikisho la Soka Senegal, wamesema, timu hiyo ya Senegal huenda ikaadhibiwa vikali na CAF.
MATOKEO KAMILI NA TIMU ZILIZOFUZU:
Ethiopia 2-0 Sudan - Addis Ababa
Matokeo ya Jumla: Sudan 5-5 Ethiopia
Ethiopia wamefuzu kwa faida ya mabao ya ugenini
Cameroon 2-1 Cape Verde  -Yaounde-
Matokeo ya Jumla: Cape Verde 3-2 Cameroon
Cape Verde wamefuzu kwa mara ya kwanza fainali zijazo za Afcon 2013 kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-2.
Angola 2-0 Zimbabwe – Luanda
Matokeo ya Jumla: Angola 3-3 Zimbabwe
Angola wamefuzu kwa faida ya mabao ya ugenini.
MECHI ZA JUMAMOSI (Oktoba 13, 2014)
Malawi 0-1 Ghana - Lilongwe
Matokeo ya Jumla: Ghana 3-0 Malawi
Ghana imefuzu kwa mara nyingine
Botswana 1-4 Mali - Gaborone
Matokeo ya Jumla: Mali 7-1 Botswana
Mali imefuzu
Uganda 1-0 Zambia - Kampala
Matokeo ya Jumla: Uganda 1-1 Zambia
Zambia wameshinda kwa penalti 9-8 na kufuzu
Nigeria 6-1 Liberia - Calabar
Matokeo ya Jumla: Nigeria 8-3 Liberia
Nigeria imefuzu
Tunisia 0-0 Sierra Leone - Monastir
Matokeo ya Jumla: Sierra Leone 2-2 Tunisia
Tunisia wamefuzu kwa faida ya mabao ya ugenini
Senegal 0-2 Ivory Coast - Dakar
Mechi imevunjwa kwa sababu ya vurugu za mashabiki
Matokeo: Morocco 4-0 Msumbiji - Marrakech
Matokeo ya Jumla: Msumbiji 2-4 Morocco
Morocco imefuzu

MABAO YA DROGBA YALIVYOCHAFUA AMANI SENEGAL, DAKAR YANUKA MOSHI

Kimenuka... Drogba akilindwa na Polisi wakati akitolewa uwanjani.
Shabiki wa Senegal akidakwa na polisi baada ya kuingia uwanjani wakati Didier Drogba (kulia) akitaka kupiga penati iliyowapa Ivory Coast uongozi wa mabao 2-0 dhidi ya Senegal katika mechi yao ya kuwania kufuzu kwa fainali zijazo za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2013) kwenye Uwanja wa Leopold Sedar Senghor mjini Dakar, Senegal jana, Octoba 13, 2012. (Picha: AP)
Hatari...!  Mashabiki wa 'chama' la kina Drogba wakihaha kujiokoa jana baada ya vurugu kuibuka katika mechi yao dhidi ya Senegal.

Duh...! Kimenuka hadi kitaa.... mashabiki wa Senegal wakikimbia mitaani huku wakiandamwa na mabomu ya machozi baada ya kuzuka kwa vurugu uwanjani jana.

Yaya Toure (kulia) na wachezaji wenzake wa Ivory Coast wakitolewa uwanjani na 'FFU' wa Senegal baada ya vurugu zilizotokea uwanjani jana.


Sasa uwanjani hapakaliki tena...!

Ni vurugu mtindo mmoja baada ya mashabiki wa Senegal kukasirishwa na kipigo cha Ivory Coast dhidi ya timu yao jana.

Wachezaji Ivory Coast wakitolewa uwanjani.

Wachezaji wakitolewa uwanjani wakisindikizwa na polisi baada ya mawe, chupa na vitu mbalimbali  kurushwa uwanjani na mashabiki wenye hasira wa Senegal waliokasirishwa kuona timu yao ikichapwa na kina Drogba.

Mashabiki wa Ivory Coast wakihaha kujiweka pamoja ili kujiokoa jana.



Kimenuka mwanaa... hapakaliki tena uwanjani!


DAKAR, Senegal 
Mechi muhimu ya kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Senegal na Ivory Coast imefutwa baada ya mashabiki kuvamia uwanja mjini Dakar juzi.

Mashabiki wa wenyeji walianza kwa kuwasha moto majukwaani na kurusha mawe na vitu vingine uwanjani wakati Senegal wakiwa nyuma kwa mabao 2-0, matokeo ambayo yangewatoa katika michuano hiyo.

Mashabiki wa Ivory Coast walikimbilia uwanjani kuepuka mashambulizi.

Mashabiki na wachezaji wa Ivory Coast baadaye walitolewa nje na polisi, ambao walifyatua mabomu ya machozi kuelekea kwenye majukwaa yaliyofurika mashabiki.

Taarifa zimesema kuwa takriban wati 10 -- akiwamo Waziri wa Michezo wa Senegal,Hadji Malick Gakou -- walijeruhiwa katika vurugu hizo kwenye Uwanja wa  Leopold Sedar Senghor.

Vurugu hizo zilitokea baada ya mshambuliaji wa Ivory Coast, Didier Drogba kufunga goli lake la pili kwa njia ya penati, huku zikiwa zimebaki dakika 15 kabla mechi kumalizika. Kabla ya goli hilo la penati lililokuwa la 58 kwake kuifungia Ivory Coast, Drogba alifunga goli la kwanza katika mechi hiyo kwa njia ya 'fri-kiki'. 

Matokeo hayo yangeiwezesha Ivory Coast kuongoza kwa jumla ya mabao 6-2 baada ya kushinda pia kwa mabao 4-2 katika mechi yao ya kwanza.

"Vyakula, vinywaji na chochote kile kilichoweza kurushwa kilirushwa uwanjani, kutoka katika kona tofauti," Chris Fuglestad, mwanafunzi wa Marekani anayesoma mjini Dakar, aliiambia BBC.

Shirikisho la Soka la Afrika (Caf) bado halijatoa taarifa rasmi kuhusiana na tukiuo hilo. Lakini afisa mmoja wa Senegal alikaririwa akisema kwamba sasa timu yao itafungiwa na Caf.

Wachezaji ndugu wa Manchester City, Yaya na Kolo Toure walikuwamo katika kikosi cha Ivory Coast, na klabu hiyo ya Ligi Kuu ya England ilisema katika taarifa yake kuwa: "Yaya na Kolo Toure wote wako salama baada ya vurugu za mashabiki kuvunja mechi wakati Senegal walipoikaribisha Ivory Coast mjini Dakar."

SOURCE: straikamkali.blogspot.com

IBRAHIM CLASS AMCHAPA JONAS SEGU, ILALA SHANGWE TUPU

Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kushoto akioneshana ufundi wa kutupiana masumbwi na Jonas Segu waakati wa mpambano wao uliofanyika jumapili siku ya kumbukumbu ya Baba wa tiafa Class alishinda kwa point picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Refarii wa mpambano akimuinua mkono juu bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' baada ya kumtwanga Jonas Segu kwa point na kupereka furahaa ya ushindi katika Kambi ya Ilala anaefurahi kushoto ni kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D' picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com


Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila katikati akiwa katika picha ya pamoja  na Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' baada ya kumdunda kwa point bondia Jonas Segu picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe'  kushoto akioneshana ufundi wa kutupiana masumbwi na Jonas Segu waakati wa mpambano wao uliofanyika jumapili siku ya kumbukumbu ya Baba wa tiafa Class alishinda kwa point picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe'  kushoto akioneshana ufundi wa kutupiana masumbwi na Jonas Segu waakati wa mpambano wao uliofanyika jumapili siku ya kumbukumbu ya Baba wa tiafa Class alishinda kwa point picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com


Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Ngumi Rajabu Mhamila 'Super D' akimpereka ulingoni bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kwenda kupambana na bondia Jonas Segu wakati wa kumbukumbu ya kifo cha baba wa Taifa Class alishinda kwa Point picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Ngumi Rajabu Mhamila 'Super D' akimpereka ulingoni bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kwenda kupambana na bondia Jonas Segu wakati wa kumbukumbu ya kifo cha baba wa Taifa Class alishinda kwa Point picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

  MASHALI AMTWANGA MGANDA NA KUTWAA UBINGWA EAC

Mchezaji wa Mpira wa Timu ya Simba na Timu ya Taifa ya Tanzania Juma Nyoso kulia akiwa wakiomba Duwa kwa ajili ya bondia Thomas Mashali katikati wa pili kulia ni msanii Maarufu wa bongo Fleva Josephe Haule Pr. J ambapo walikwenda kumpa kampani bondia huyo na kufanikisha ushindi wake na kumuenzi muhasisi wa taifa hili baba wa taifa picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
bondia Thomas Mashali akiwa na mikanda yake ya ubingwa wa Tanzania pamoja na wa Afrika Mashariki na Kati
Rais wa TPBO Yasini Abdallah akisalimiana na Prof.J kwenye kona ya Mashali
Mchezaji wa Mpira wa Timu ya Simba na Timu ya Taifa ya Tanzania Juma Nyoso kulia akiwa amebeba bendera ya Taifa wakati ukipigwa wimbo wa taifa kwa ajili ya bondia Thomas Mashali katikati wa pili kulia ni msanii Maarufu wa bongo Fleva Josephe Haule Pr. J ambapo walikwenda kumpa kampani bondio huyo na kufanikisha ushindi wake na kumuenzi muhasisi wa taifa hili baba wa taifa picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Baadhi ya Viongozi pamoja na mgeni rasmi wakisimama kwa ajili ya wimbo wa tafa kabla ya mpambano
BONDIA THOMAS MASHALI kushoto akioneshana uwezo wa kutupiana masumbwi na  MEDY SEBYALA wa Uganda wakati wa mpambano wao uliofanyika kwa ajili ya kumbukumbu ya baba wa taifa Mashali alishinda kwa Point picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Medy Sebyala akioneshana ufundi wa kutupiana makonde na bondia Thomas Mashali wakati wa mpambano wao wa kugombea ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati Mashali alishinda kwa point picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

BONDIA THOMAS MASHALI kushoto akioneshana uwezo wa kutupiana masumbwi na  MEDY SEBYALA wa Uganda wakati wa mpambano wao uliofanyika kwa ajili ya kumbukumbu ya baba wa taifa Mashali alishinda kwa Point picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Medy Sebyala akioneshana ufundi wa kutupiana makonde na bondia Thomas Mashali wakati wa mpambano wao wa kugombea ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati Mashali alishinda kwa point picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Charles Kenyela kushoto akiwa amekinga ngumi huku akiwa na furahaa baada ya bondia Thomas Mashali kuibuka na ubigwa kwa kumpiga bondia kutoka Uganda wakati wa maazimisho ya kumbukumbu ya baba wa taifa picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Thomasi Mashali akiwa na mkanda wake wa ubingwa wa Afrika Mashaliki katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com



Mbunge wa Kinondoni Iddy Azani akiwa katika picha na Bondia Thomas Mashali baada ya kuvishwa ubingwa wa Afrika Mashariki picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Medy Sebyala akioneshana ufundi wa kutupiana makonde na bondia Thomas Mashali wakati wa mpambano wao wa kugombea ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati Mashali alishinda kwa point picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Sunday, October 14, 2012

RAIS KIKWETE ATEMBELEA MAKANISA YALIYOHARIBIWA KATIKA VURUGU ZA WAISLAMU MBAGALA



Rais Jakaya Kikwete akiangalia uharibifu mkubwa uliofanywa katika kanisa la Pentekoste la Mbagala jijini Dar es Salaam, wakati wa vurugu za Waislamu jana Ijumaa kufuatia habari kuwa kuna mtoto amekojolea Qur an.
Rais Jakaya Kikwete akioneshwa na Mchungaji Alkwin Mbawi uharibifu uliofanywa kwenye magari yaliyokuwa yameegeshwa ndani ya kanisa la Pentekoste la Mbagala jijini Dar es Salaam wakati wa vurugu za Waislamu jana Ijumaa.
Rais Jakaya Kikwete akioneshwa na Katibu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam M Mkosimonga, uharibifu uliofanywa kwenye kanisa hilo huko Mbagala jijini Dar es Salaam wakati wa vurugu za Waislamu jana Ijumaa.
Rais Kikwete akioneshwa na Katibu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam M. Mkosimonga  uharibifu uliofanywa kwenye kanisa hilo wakati wa vurugu za Waislamu jana.
Rais Kikwete akioneshwa na Askofu Msaidizi wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheli Dayosisi ya Dar es Salaam na Pwani, Mkosimonga uharibifu uliofanywa kwenye kanisa hilo huko Mbagala wakati wa vurugu za Waislamu jana Ijumaa.
You might also like:

Messi aing'arisha Argentina

Lionel Messi wa Argentina


MENDOZA, Argentina
Lionel Messi aliiongoza Argentina kuilaza timu ngumu ya Uruguay katika nusu saa ya mwisho ya mchezo kwa mabao mawili ya kifundi katika ushindi wa 3-0 jana ambao umeibakiza kileleni mwa msimamo wa kundi la Amerika Kusini la michuano ya awali ya Kombe la Dunia.
Argentina inaongoza kundi la timu tisa la Amerika Kusini ikiwa na pointi 17 katika mechi nane ambazo ni nusu ya kampeni. Colombia na Ecuador zipo pointi moja nyuma, Uruguay na Chile tano nyuma yake.
Messi alitengeneza na kumalizia goli lake la kwanza katika dakika ya 66, alipotoa pasi kwa Angel Di Maria kabla ya kukimbia kwenda kuusukumizia wavuni mpira huo uliompita Fernando Muslera.
Argentina ilipata bao la pili dakika tisa baadaye kwa muvu nyingine kwenye wingi ya kushoto, Messi akimpa pasi tena Di Maria ambaye alirudisha mpira huo kwa 'tachi' ya kwanza ambapo Sergio Aguero aliugusa na kutumbukia nyavuni.
Goli la tatu katika dakika ya 80 lilitokana na mpira wa kijanja wa adhabu ndogo wa Messi, ambaye aliudanganya ukuta wa Uruguay kwa kupitisha mpira huo chini yao na kufunga wakati wenyewe wakiruka wakitaraji atalenga lango kwa juu.
Kilikuwa kisasi kizuri kwa Messi, ambaye sasa amefunga magoli 12 katika mechi saab zilizopita za timu ya taifa, na Argentina ambayo ilitolewa na Uruguay kwa penalti katika fainali za mwaka 2011 za Copa America ambazo washiriki hao wa nusufainali ya Kombe la Dunia mwaka 2010 walikuja kutwaa ubingwa.
Reuters

Simba hawashikiki Bara licha ya kunasa kwa Coastal Union


Mabingwa wa ligi kuu ya Bara Simba jana walipunguzwa kasi na Coastal Union hapa Tanga, lakini angalau wakamudu kuendeleza rekodi ya kutopoteza mchezo mpaka robo ya msimu, kufuatia sare ya 0-0 kwenye Uwanja wa Mkwakwani.
Kwa sare hiyo dhidi ya Coastal iliyokuwa na wachezaji 10 uwanjani kwa zaidi ya dakika 20, Simba imeendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Bara baada ya kufikisha pointi 17 kutokana na michezo saba. Wenyeji wamefikisha pointi 10.
Azam imejichimbia katika nafasi ya pili, pointi moja nyuma ya Simba baada ya jana kuifunga Polisi Morogoro bao 1-0 kwenye Uwanja wa Jamhuri, huku ikiwa na mechi moja mkononi.
Simba ambayo ilishinda michezo minne mfululizo kabla ya kutoka sare ya 1-1 na Yanga na kurejea kushinda katika mchezo uliopita dhidi ya JKT Oljoro, ingeweza kuwa imepoteza mechi yake ya kwanza jana kama Coastal iliyoonyesha soka maridadi ingekuwa makini.
Hemedi Morocco, kocha wa Coastal Union, alisema anashukuru kupata pointi moja licha ya timu yake kushindwa kutumia vizuri nafasi nyingi za kufunga ilizotengeneza.
Kocha wa Simba Milovan Cirkovic aliwaambia waandishi wa habari baada ya mchezo huo kuwa Coastal ilicheza vizuri, lakini pia hakufurahishwa na uchezaji wa mshambuliaji wake wa kulipwa kutoka Ghana Daniel Akuffor.
Chipukizi Haruna Chanongo alikaribia kuipatia Simba bao la kuongoza katika dakika ya 12 baada ya shuti lake kugonga mwamba wa juu na kutoka nje.
Kama Chanongo angefunga, Nsa Job angeweza kuwa ameisawazishia Coastal Union katika dakika ya 39 wakati shuti lake lililopotoka nje akiwa katika nafasi nzuri, kutokana na krosi ya Selemani Kassim ambaye alikuwa amemtoka beki Pascal Ochieng.
Siku ya mshambuliaji wa kati Job ilimalizika vibaya dakika 20 hivi kabla ya filimbi ya mwisho hata hivyo, baada ya kutolewa uwanjani na muamuzi Haji Mbelwa kutokana na kosa la pili la kadi ya njano dhidi ya mabeki wawili wa kati wa Simba.
Katika kosa la kwanza, Job ambaye ni mchezaji wa zamani wa Simba, alimchezea vibaya Shomari Kapombe kabla ya kumfanyia madhambi Ochieng katika kipindi cha pili.  
Timu zilikuwa:
COASTAL: Jackson Chove, Said Sued, Juma Jabu, Mbwana Hamisi, Jamal Machelenga, Jerry Santo, Mohammed Athumani, Selemani Kassim, Green Atupele, Nsa Job, Razak Khalfani (Lameck Dayton dk.45).
SIMBA: Juma Kaseja, Said Nasoro, Amiri Maftah, Pascal Ochieng, Shomari Kapombe, Mwinyi Kazimoto, Amri Kiemba, Haruna Moshi (Uhuru Selemani dk.58), Felix Sunzu, Daniel Akuffor (Salum Kinje dk.72), Haruna Chonongo.
Kutoka Morogoro Idda Mushi anaripoti kwamba bao la Azam lilifungwa na Kipre Tchetche katika dakika ya 54 hivyo kuiweka timu hiyo katika nafasi nzuri ya kukaa kileleni kama itashinda mechi yake ya mkononi.
Kocha wa Azam Boris Bunjak alielezea kutoridhishwa na ukubwa wa ushindi huo kutokana na Polisi kuwa timu ya mkiani.
John Simkoko, mwalimu wa Polisi alisema makosa madogo madogo ya mchezaji mmoja mmoja na si timu, ndiyo yaliyowagharimu.

Nnyota wa Simba, Yanga washindwa kutambiana 'mchangani'

Onesmo Waziri 'Ticotico' (4) wa Golden Bush akitafuta mbinu za kumtoka mchezaji wa wahenga Fc (kulia) huku Abdallah Msheli akiwa tayari kumsaidia

Katina George (14) wa Golden Bush akijaribu kufunga bao mbele ya msitu wa mabeki wa Wahenga Fc katika pambano lao lililochezwa jana Sinza, Dar es Salaam.

NYOTA wa zamani wa klabu za Simba na Yanga jana walishindwa kutambiana baada ya timu walizokuwa wakizichezea za Golden Bush na Wahenga Fc kutoshana nguvu ya kutoka sare ya 1-1 katika pambano la kirafiki.
Wazir Mahadhi, Abdul Ntiro, Ally Yusuf  'Tigana', Abdallah Msheli na Steven Marashi walioichezea Golden Bush ya Mabibo walishindwa kuwazidi ujanja wenzao Mengi Matunda na Madaraka Seleman 'Mzee wa Kiminyio' wa Wahenga ya Sinza katika mchezo huo uliochezwa uwanja wa TP, Sinza.
Nyota hao walionyesha bado wamo katika usakataji soka kwa jinsi walivyokuwa wakikimbiza dimbani ili kuzisaidia timu zao, lakini mpaka wakati wa mapumziko Wahenga ndio waliokuwa wakiongoza kwa bao 1-0.
Bao lao lilifungwa na Mohammed Ibrahim katika dakika ya 38 baada ya kufanikiwa kuihadaa ngome ya Golden Bush iliyokuwa chini ya Msheli na kumchambua kipa Steven Marashi kwa shuti la karibu.
Kipindi cha pili Golden Bush chini ya nahodha wake Onesmo Wazir 'Ticotico', iliingia kwa kasi baada ya kufanya mabadiliko kadhaa na kufanikiwa kurejesha bao hilo katika dakika ya 64 kupitia Dau 'Messi' aliyemegewa pande zuri Ally Yusuf  'Tigana'.
Licha ya timu zote kushambuliana kwa zamu na kufanya kosa kosa nyingi, mpaka kipyenga kilichokuwa kikipulizwa na Ally Mayay Tembele kilipolia matokeo yalikuwa yamesalia kama awali kwa timu hizo kutoka sare ya bao 1-1.

Mwisho

Waliovamia maeneo ya shule Ilala kukiona

Afisa Mipango Miji wa Ilala, Paul Mbembela akisisitiza jambo alipozungumza na wakazi za Kitunda

Baadhi ya watu waliohudhuria mkutano huo

Mmoja wa wakazi wa Kitunda akiuliza swali ili apate ufafanuzi juu ya hatma ya makazi yao katika eneo wanaloishi
WAKAZI wote waliovamia na kujenga ndani ya maeneo ya shule wilayani Ilala, jijini Dar es Salaam wametahadharishwa kuanza kuondoka wenyewe kabla ya kuchukuliwa hatua za kuondolewa kwa lazima katika maeneo hayo.
Aidha serikali na Manispaa hiyo ya Ilala imeweka bayana kwamba haitakuwa na huruma wala kuwaonea haya wavamizi wa maeneo hayo ya shuleni wakati wa zoezi la kuwaondoa kwa lazima.
Afisa Mipango Miji wa Ilala, Paul Mbembela, ndiye aliyeyasema hayo juzi katika mkutano wa pamoja kati ya ofisi yake na wakazi wa Kitunda, nje kidogo ya Dar es Salaam.
Mbembela alisema Manispaa haitakuwa na huruma na wale wote waliovamia na kujenga ndani ya maeneo ya shule kwa madai waliofanya hivyo wamevunja sheria na hawapaswi kuchekewa.
"Tutakuwa wakali kwa wale wote waliovamia na kujenga katika maeneo ya shule, kuchekea jambo hilo ni kutaka kuwafanya vijana na watoto wete wawe mbumbumbu kwa kushindwa kusoma katika mazingira mazuri," alisema.
Aliongeza kuwa, wananchi wote wanaojitambua kuwa wamefanya hivyo waanze mapema kuchukua uamuzi wa kuondoka wenyewe kwa hiari katika maeneo hayto kabla ya Manispaa ya Ilala haijaenda kuwatoa kwa nguvu.
Afisa huyo, alisema kumekuwa na desturi ya watu kuvamia maeneo ya shule ya kuweka makazi au sehemu za biashara na kusababisha wanafunzi kushindwa kusoma kwa utulivu, kitu ambacho Manispaa yao haipo tayari kuvumilia.
Alisema wananchi wanapaswa kutambua kuwa shule ni moja ya vitu muhimu vinavyopaswa kutochezewa kwani ndiko kunakozalisha viongozi na wataalam kwa baadaye wa taifa hivyo kila mmoja ana jukumu la kuzilinda shule.

Mwisho

Wakazi Kitunda wahakikishiwa makazi ya kudumu mradi wa viwanda



Afisa Mipango Miji wa Manispaa ya Ilala, Paul Mbembela akifafanua jambo katika mkutano wake na wakazi wa Kitunda waliojenga makazi yao ndani ya mradi wa viwanda uliotengwa na serikali miaka kadhaa iliyopita

Prisca Bassu mmoja wa wakazi wa Kitunda akiuliza swali katika mkutano huo

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kipunguni B, Novatus Nyiratu akifafanua jambo katika mkutano huo wa jana

Mkazi mwingine wa eneo la Kitunda akiuliza swali

Sehemu ya umma uliohudhuria mkutano huo wa jana kujua mustakabali wa waliojenga ndani ya mradi wa viwanda

Nataka kujua tusiokuwa na leseni za makazi inajuwaje hatma yetu? Ndivyo mmoja wa wakazi hao alihoji katika mkutano huo

Ibrahim Ismail naye alisimama na kuuliza swali

Hata kinamama nasi tumo kwa maswali

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kitunda Kati, Seleman Abdallah Mtama akieleza jambo kabla ya kuufunga mkutano huo







UONGOZI wa Manispaa ya Ilala, umewatoa hofu na kuwahakikishia wakazi wa eneo la Kitunda, waliojenga na kuweka makazi ndani ya eneo lililotengwa kwa ajili ya mradi wa viwanda kwamba kamwe hawataondolewa.
Pia uongozi huo umewahakikishia wakazi hao kuwa maeneo yao yatapimwa upya na kumilikishwa ardhi ili yawe makazi yao ya kudumu mara taratibu za kubadilisha matumizi ya eneo hilo zilizoanza zitakapokamilika.
Akizungumza na wakazi hao katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na uongozi wa serikali za mitaa ya Kipunguni B na Kitunda Kati, uliofanyika juzi kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Kipunguni, Afisa Mipango Miji Manispaa ya Ilala, Paul Mbembela alisema wakazi hao hawapaswi kuwa na hofu.
Mbembela alisema licha ya kwamba wakazi wa eneo hilo wapo ndani ya ardhi iliyotengwa kwa miaka mingi na serikali kwa ajili ya mradi wa viwanda, bado hawana hofu kwa vile unafanyika mchakato wa kubadilishwa matumizi yake.
Alisema katika mabadiliko hayo ya matumizi, wakazi waliojenga na kumiliki viwanja katika eneo hilo watafanyiwa utaratibu wa kupimwa maeneo yao na kisha kumilikishwa upya kihalali na mradi huo wa viwanda utahamishiwa maeneo mengine ya viwanja vya serikali vilivyopimwa tayari.
Afisa huyo aliyataja baadhi ya maeneo ambayo mradi huo unaweza kuhamia ni pamoja na Buyuni, Chanika na kwingineko katika manispaa ya Ilala ambayo tayari yameshapimwa na kutengwa.
Aliwasisitiza wakazi hao waliowatuma viongozi wa serikali zao za mitaa katika ofisi za manispaa kuhakikisha wanaipa ushirikiano kamati hiyo katika zoezi la kuwatambua wamiliki halali wa sasa waliopo katika eneo hilo ili kurahisisha mchakato wa kuyapima na kuwamilikisha upya.
Kabla ya ufafanuzi huo wananchi wa maeneo hayo kupitia serikali zao za mitaa walikuwa na hofu kubwa ya kubomolewa na kupoteza mali zao katika eneo hilo baada ya kubainika eneo hilo lilitengwa kwa mradi wa viwanda.
Baadhi ya wananchi katika mkutano huo uliohudhuriwa na Mwenyekiti wa Serikali ya Kitunda Kati, Seleman Mtama na ile ya Kipunguni B, Novatus Nyiratu walitaka kujua hatma yao iwapo watatimuliwa katika eneo  hilo.
Miongoni mwa wakazi hao, Ibrahim Ismail, Prisca Bassu walitaka kufahamu iwapo wananchi ambao hawana hati au leseni ya makazi katika eneo hilo hatma yao itakuwaje na kuelezwa watasaidiwa  kumilikishwa bila ya tatizo mradi wahakikiwe na kamati yao.

Saturday, October 13, 2012

Mashali, Sebyala wapima uzito kuvaana kesho Friends Cornerupimwa uzito kesho


BONDIA Thomas Mashali wa Tanzania na Mganda Medi Sebyala wamepima uzito leo kwenye ukumbi uliopo Manzese jijini Dar es Salaam tayari kwa ajili ya pambano lao la ubingwa wa Afrika Mashariiki na Kati litakaofanyika Jumapili kwenye ukumbi wa Friend's Corner, Manzese jijini Dar es Salaam.
Mabondia hao walipimwa uzito na afya hizo asubuhi ya leo tayari kwa pambano hilo lililoandaliwa na mratibu Regina Gwae chini ya TPBO.
Mbali na mabondia hao wengine waliopimwa leo ni  Abdul Awilo atakayepanda ulingoni kuchuana na Shedrack Juma, Selemani shaaban atakayechapana na Hamis Mohamed,  Jonas Segu atakayemkabili Ibrahim Class  na  Charles Mashali atakayevaana na Teacher Aaron.
Regina alisema maandalizi yote yamekamilika ikiwamo waamuzi wenye sifa za kuchezesha mapambano ya kimataifa anbao tayari wameshapatikana na mgeni rasmi katika pambano hilo atakuwa Kamanda wa  Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Charles Kenyela ambaye anatarajiwa kuambatana na wageni wengine maalum akiwamo Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Mhe. Idd Azzan.
---

Kiemba akana kuziba pengo la Mafisango Simba

Amri Kiamba akishangilia bao moja ya mabao yake katika Ligi Kuu msimu huu

KIUNGO nyota wa Simba, Amri Kiemba, licha ya kuwashukuru mashabiki wa klabu hiyo kumfananisha na kiungo wa kimataifa wa timu hiyo Patrick Mafisango, aliyefariki kwa ajali ya gari Mei mwaka huu, amekiri hajaliziba pengo la kiungo huyo.
Akizungumza na MICHARAZOE muda mchache kabla ya kuondoka jijini na kikosi cha timu yake kuelekea Tanga kuwahi pambano lao dhidi ya Coastal Union, Kiemba alisema licha ya kuanza msimu kwa kung'ara, bado anajiona hajaliziba pengo la Mafisango hata kama watu wanaridhika na kiwango chake.
Kiemba, alisema ni vigumu pengo la kiungo huyo aliyefariki Mei 17 kuzibika kirahisi na kwa ukamilifu kutokana na uwezo na kipaji kikubwa alichokuwa nacho nyota huyo kutoka nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.
"Nashukuru mashabiki kuridhika na juhudi zangu uwanjani kiasi cha kuona kama nimeziba pengo la Mafisango, ila ukweli ni vigumu pengo la kiungo huyo kuzibika kirahisi hata mie mwenyewe najiona sijaliziba hata kidogo, " alisema
Kiemba aliongeza, binafsi alikuwa akimkubali Mafisango kwa umahiri wake hivyo anajisikia vibaya kufananishwa naye japo anafurahia kuona mashabiki wanakikubali kiwango chake kwa mechi chache zilizoanza za msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Kiungo huyo wa zamani wa Yanga, aliyeigomea Simba msimu uliopita kumtoa kwa mkopo kwenda kuichezea timu iliyokuja kushuka daraja ya Polisi Dodoma ameanza  msimu kwa kuonyesha kiwango cha hali ya juu akiifungia Simba mabao yaliyoiweka kileleni mwa msimamo huku mwenyewe akiongoza orodha ya wafungaji mpasa sasa.
Mchezaji huyo ameifungia Simba jumla ya mabao manne mpaka sasa, matatu akiyafunga katika mechi mbili zilizopita dhidi ya Yanga waliotoka nao sare ya bao 1-1 na ile ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya JKT Oljoro, jingine alifunga walipilaza JKT Ruvu.

Mwisho

Miyeyusho, Nassib kuvaana Uhuru Day


MABONDIA wanaozidi kupanda chati nchini, Francis Miyeyusho na Nassib
Ramadhani wanatarajia kuvaana jijini Dar es Salaam siku ya Desemba 9 katika pambano la kuwania ubingwa wa Mabara unaotambuliwa na WB-Forum.
Pambano hilo linatarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa PTA na limeandaliwa na promota Mohammed Bawazir wa kampuni ya Dar World Link chini ya usimamizi wa Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Tanzania, PST.
Hilo litakuwa pambano la kwanza kwa mabondia hao wenye rekodi ya kuwapiga wapinzani wao kukutana.
Akizungumza kwenye utambulisho wa mabondia hao, promota wa pambano hilo la uzani wa Bantam (kilo 53.5), Mohammed Bawazir, alisema maandalizi ya mchezo huo yamekamilika ikiwemo kumalizana na mabondia hao.
Bawazir alisema ana imani litakuwa la aina yake kulingana na rekodi za mabondia hao.
Kwa mujibu wa rekodi za Miyeyusho mwenye umri wa miaka 32 amecheza jumla ya mapambano 44 akishinda michezo 32, 19 ikiwa ya KO amepigwa 10 na kutoka sare michezo miwili.
Kwa upande wa rekodi za Nassib inaonyesha amecheza mapambano 12 akishinda 10 na kupoteza mawili.
Kabla ya kuvaana na Miyeyusho bondia huyo anatarajiwa kuvaana na Mkenya Nick Otieno atakayepigana nae Novemba 30 kwenye pambano la kuwania ubingwa wa IBF Afrika na Ghuba ya Uajemi.

GOLDEN BUSH WALIPOPIMANA UBAVU NA WAHENGA FC UWANJA WA TP-SINZA


BAADHI YA PICHA ZA MATUKIO YA PAMBANO LA TIMU YA SOKA YA GOLDEN BUSH ILIYOKUWA IKIUNDWA NA NYOTA WA ZAMANI WA YANGA KAMA AKINA ALLY YUSUF 'TIGANA', ABDALLA MSHELI, WAZIR MAHADH 'MANDIETA' CHINI YA UNAHODHA WA ONESMO WAZIR 'TICOTICO' DHIDI YA WAHENGA FC ILIYOKUWA IKIONGOZWA NA MKONGWE MADARAKA SELEMAN 'MZEE WA KIMINYIO'.
Patashika dimbani kati ya Golden Bush na Wahenga FC

Onesmo Wazir 'Ticotico' wa Golden Bush (kushoto), akitafuta mbinu za kumpotoka China wa Wahenga Fc, huku mchezaji wenzake akiwa tayari kumsaidia.

Twende sasa kama 'Ronaldo'

Ticotico akitafuta mbinu za kumtoka mchezaji wa Wahenga Fc

China wa Wahenga Fc akiambaa na mpira dimbani katika mechi yao leo dhidi ya Golden Bush ambapo mpaka tunaondoka uwanjani matokeo yalikuwa bao 1-1. Wahenga wakitangulia kupata bao dakika ya 38 kupitia Moahmmed Ibrahim kabla ya Golden Bush kurejesha katika kipindi cha pili kupitia kwa Dau 'Messi'

China wa Wahenga akimtokea beki wa Golden Bush (14) huku wachezaji wengine wakiwa tayari kutoa msaada.

Machota wa Golden Bush akimiliki mpira mbele ya mchezaji wa Wahenga Fc