STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, December 2, 2014

TPBO-Limited yafichua siri ya mabondia wa Tz kupigwa ughaibuni

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEix_ikFUVQYo2XFuYXtUqvjRzHYr5VnfbR27zD1v1mQO9vDKcyGTWjAyDe3E9fbTST0rnQCVDupyg8mHUY0b4E6Sd-_s4zemsQTsSDaMD7Fz_DjHVmpMzcqxBTIkpxN200Ne6-sNZjJDms7/s1600/IMG_0009.JPG
Rais wa TPBO-Ltd, Yasin 'Ustaadh' Abdallah
RAIS wa Oganaizesheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBO-Ltd) Yasin Abdallah 'Ustaadh' amefichua siri za mabondia wengi wa Tanzania kushindwa kufanya vema kwenye mapambano yao ya kimataifa nje ya Tanzania, akidai inachangiwa na maandalizi duni na pia kutohimili kucheza mbele ya umati mkubwa wa watazamaji.
Ustaadh, alisema siyo kweli kama mabondia wa Tanzania wanapigwa na kupoteza michezo yao nje ya nchi kwa sababu ya hujuma, bali ni kutokana na kutojiandaa vema kwa utamaduni uliipo miongoni mwa mabondia wengi nchini kutotambua kama ngumi za kulipwa ni biashara zinazohitaji wahusika kuzingatia miiko, maadili na nidhamu ya hali ya juu kufikia mafanikio ya wenzao wanaotamba duniani.
"Siyo kama wanapigwa kwa hila, wengi huwa hawafanyi maandalizi mazuri, hukurupuka tu kwenda nje kupigana na mwishowe kutia aibu imefika wakati sasa mabondia wakazinduka na kujitambua," alisema Ustaadh.
Alitoa maoni yake kufuatia bondia Fadhili Majiha kupigwa kwa KO ya raundi ya 3 kwenye pambano la utangulizi wakati Manny Pacquiao akitetea taji lake la WBO mbele ya Chris Algieri, ambapo Ustaadh alisema inawezekana kucheza mbele ya umati mkubwa na kukosa kwake maandalizi yamechangia kupata matokeo mabaya kulinganisha na yale aliyopata Russia alipoenda kupigwa kwa pointi.
Kwa muda mrefu mabondia wa Tanzania wamekuwa wakipata matokeo mabaya kwenye mapambano yao nje ya Tanzania, kiasi cha kuzushiwa kuwa huenda ni 'dili' zinazofanywa na baadhi ya mawakala wa mabondia wanaotoa ofa ya Watanzania kwenda kupigana katika nchi zao ili kulinda na kuboresha rekodi  za mabondia wanaowasimamia, wakishirikiana na viongozi wa mchezo huo nchini.
Hata hivyo mara kadhaa viongozi wa vyama vya ngumi za kulipwa wamekuwa wakikanusha kuwepo kwa suala hilo na kusisitiza kuwa mabondia wa Tanzania wanapigwa kwa sababu ya maandalizi ya zima moto na kutokuwa na mameneja wa kuwasimamia.

Yanga yampa mkataba wa mwaka mmoja Mbrazil Emerson

EMERSON AKISAINI MKATABA WA MWAKA MMOJA KUICHEZEA YANGA MBELE YA MTAALAMU WA MAMBO YA IT NA MSEMAJI WA YANGA, BARAKA KIZUGUTO.
KLABU ya soka ya Yanga imemsainisha mkataba wa mwaka mmoja kiungo mkabaji mpya kutokla Brazil,  Emerson De Oliveira Neves Roque.
Tukio la usainiwaji wa mkataba huo wa mwaka mmoja lilifanyika jana baada ya kiungo huyo kuliridhisha benchi la ufundi la klabu hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotangazwa na mtandaop wa klabu ya Yanga benchi la ufundi liliridhika na uwezo wake,na mchezaji mwenyewe kufikia makubaliano hayo ya kuwatumikia watoto wa Jangwani.

Baada ya kufanya mazoezi kwa siku nne mfululizo chini ya makocha Marcio Maximo, Leonardo Neiva na makocha wazawa Salavatory Edward, Shadrack Nsajigwa kwa pamoja wameridhiswa na uwezo wake na kuomba apewe kandarasi la kuitumikia klabu ya Young Africans.
Emerson aliyekua akichezea katika timu ya Bonsucesso iliyopo daraja la pili kwenye jimbo la Rio de Janeiro anachukua nafasi ya mshambuliaji Geilson Santos "Jaja" ambaye ameshindwa kureje nchini kutokana na matatizo ya kifamilia na kuomba klabu ya Young Africans imuache.
Kocha wa Young Africans Marcio Maximo amesema wamerizishwa na uwezo na kiungo mkabaji Emerson na kusema ataisaidia timu katika michuano mbali mbali ya Ligi na Kimataifa.
Ujio wa Emerson unafanya klabu ya Young Africans kufikisha jumla ya wachezaji watano wa kimataifa, wengine wakiwa ni Mbuyu Twite, Haruna Niyonzima, Hamis Kizza na Andrey Coutinho.

Klabu za Simba, Yanga zapigwa vijembe

http://ehabari.com/wp-content/uploads/2014/12/7a19Simba-Yanga.jpgUONGOZI wa Ruvu Shooting umezipiga 'madogo' klabu za Simba na Yanga kwamba zimekuwa mahiri katika kuviza vipaji vya soka vya wachezaji nchini kutokana na kuwasajili kwa papara kila wanapong'ara katika timu nyingine, kisha kushindwa kuwatumia.
Aidha uongozi huo umewazindua wachezaji vijana kuwa makini na kuzikimbilia klabu hizo hata kama ni kweli zina masilahi makubwa miongoni mwa klabu za soka za Afrika Mashariki, lakini ni vema pia wakaangalia vipaji vyao.
Akizungumza na MICHARAZO, msemaji wa Ruvu Masau Bwire, alisema Simba na Yanga ni klabu za 'kuviza' vipaji ndiyo maana asilimia kubwa ya wachezaji waliokuwa nyota katika klabu zao wanaposajiliwa na klabu hizo hufifia na hata kuzimika kama baadhi yao ambao licha ya kusajiliwa kwa mamilioni ya fedha wamekuwa watu wa kukaa benchi.
"Ni lazima wachezaji wanaozikimbilia Simba na Yanga wajiulize mara mbili, ni kweli zina mvuto wa kifedha lakini vipaji vyao ni muhimu, kuna maana gani kusajiliwa kwa mamilioni ya fedha kisha ukaishia kukaa benchi na mwishowe kutemwa ukiwa haina thamani," alihoji.
Bwire alisema wapo wachezaji kadhaa waliokuwa waking'ara nje ya Simba na Yanga, lakini walipotua katika timu hizo wamekuwa hawana maana yoyote wakiishia kuwa wasugua benchi kisha kuachwa kwa kudaiwa kushuka viwango na wanaposajiliwa na timu nyingine zinazowapa nafasi ya kucheza hurejea kwenye viwango vyao na klabu hizo kubwa kuwavizia tena kutaka kuwasajili.
Baadhi ya wachezaji wamekuwa wakizikimbilia Simba na Yanga kwa sababu ya usajili wa donge nono, lakini mrundikano wa wachezaji wengi mastaa umewafanya kuishia kukalia benchi na kushuka viwango kabla ya kutemwa, kitu kinachodaiwa kinachangia kudidimiza soka la Tanzania.

RT kuamua hatma yao Desemba 6

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgF-lOhMYrCVlKenUdlFeY7QpbkcfwIJuaSC7FRgOrlXV1EJeCdVq0X8PHDRiN_zLwblmyeveKZjHa8mlDA2bS2ynAPJPiO9n0eTW0O5zXJ3aS4QS-pNbzMwCxd3_BYkbSpnr_Oyf4Eadk/s1600/IMG_9856.JPG
Katibu Mkuu wa RT, Suleiman Nyambui
SHIRIKISHO la Riadha Tanzania (RT) linatarajiwa kufanya kikao cha Kamati ya Utendaji ambacho kitapitia na kujadili maoni ya mikoa wanachama wao kwa ajili ya Rasimu ya Katiba Mpya ya shirikisho hilo.
Katibu Mkuu wa RT, Suleiman Nyambui aliiambia MICHARAZO kuwa, awali kikao hicho kilikuwa kifanyike juzi Jumapili ila kilisogezwa mbele kwa sababu ya kutoa fursa kwa mikoa kuwasilisha maoni yao.
Nyambui alisema ni mikoa saba tu ambayo ilikuwa imewasilisha maoni yao tofauti na idadi ya mikoa wanachama wa shirikisho hilo ambayo ni 25.
"Kikao cha Kamati ya Utendaji cha RT kilichokuwa kifanyika Novemba 30 kimesogezwa mbele hadi Desemba 6 na ajenda zake zitakuwa ni kupitia na kujadili maoni ya mikoa juu ya Rasimu ya Katiba Mpya," alisema Nyambui.
Nyambui alisema ajenda nyingine ni kujadili maendeleo ya jumla ya mchezo huo na namna ya kuukwamua ili kuweza kufanya vema kwenye mashindano ya kimataifa yaliyopo mbele yao. Mikoa iliyowasilisha maoni yao mpaka sasa ni Dar es Salaam, Arusha, Mara, Mbeya, Majeshi, Tanga na Morogoro.

Mgambia wa Simba kujaribiwa wiki mbili kabla ya mkataba

https://hivisasa.co.tz/wp-content/uploads/2014/12/mboob.jpg
MSHAMBULIAJI mpya aliyetua Simba, Omary Mboob kutoka nchini Gambia, amepewa wiki mbili kwa ajili ya kufanya majaribio na kikosi hicho na kama akifuzu atasajiliwa kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo kwenye mechi zijazo za Ligi Kuu Bara.
Mboob amewasili nchini juzi kimya kimya na jana aliripoti mazoezi katika Uwanja wa Sigara, Chang'ombe jijini Dar es Salaam na kuanza mazoezi rasmi.
Akizungumza jana, Kocha Mkuu wa Simba, Mzambia Patrick Phiri, alisema wamempa wiki mbili mchezaji huyo kutokana na kwamba hajawahi kumuona katika mechi zake alizowahi kucheza.
"Tumempa wiki mbili za mazoezi ili tumuone kama anafaa au hafai, akifuzu atasajiliwa," alisema Phiri.
Alisema mshambuliaji huyo ni tofauti na Mganda Dan Sserunkuma ambaye atasajiliwa moja kwa moja kutokana na kwamba wameshawahi kumuona akiwa na timu yake katika baadhi ya mechi za kimataifa na nchini yake.
Phiri alisema baada ya wiki mbili watajua kama kiwango cha mchezaji huyo kinaweza kuisaidia timu kuanzia mzunguko wa nane wa Ligi Kuu unaotarajiwa kuanza kutimua vumbi Desemba 26, mwaka huu.
Kwa upande wa mazoezi kwa ujumla, alisema yanaendelea vizuri kutokana na wachezaji kujifua kwa bidii kuelekea mechi ya 'Nani Mtani Jembe 2' dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga Desemba 13, mwaka huu.

Ommy Lax achekelea video yake kupokewa vema

MSANII anayekuja kwa kasi nchini, Iman Omari 'Ommy Lax' amesema amefurahi namna mashabiki wa muziki walivyoipokea video yake mpya ya wimbo uitwao 'Mimi na Wewe' ambao inaendelea kutamba kwa sasa katika vituo mbalimbali vya runinga.
Ommy anasema jambo hilo limemtia nguvu na kujipanga kuandaa kazi nyingine mpya ili kuzidi kuwapa burudani mashabiki wake, sambamba na kulitangaza jina lake.
Video hiyo mpya ya Ommy Lax imetengenezwa na Zolla D, na 'audio' yake imetengenezwa katika studio za Bokaz Entertainment chini ya Man DVD.
Kabla ya video hiyo msanii huyo aliyejitumbukiza kwenye sanaa hiyo mwaka 2006 alitamba na video za nyimbo za 'Kioo Changu' alioimba na Matonya na 'Wapotezee' aliyomshikisha PNC.

Dokii asisitiza, 'Sijam-beep mtu Uchaguzi Mkuu 2015'

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjnoMKLupYtlqQbGVaMutBdYjiLDa_mTiB1b27_5dckqSFFO_3yEs6iO6nO9RgKk6rh8A8pH149EjrqLLJhL5hoLNlSUmoNeQjV6qnkBsvva7m50eRarf7ZV0SGQER1CqbvXFwyBQ0Y-tE/s1600/dokii%2525202%255B1%255D.JPG

MWANAMITINDO na muigizaji mahiri wa filamu nchini, Ummy Wenceslaud 'Dokii' amesema kauli yake ya kutaka kuwania ubunge siyo ya utani na kwamba ‘hajambeep’ yeyote bali amedhamiria kweli 2015 kuingia bungeni.
Akizungumza na MICHARAZO, Dokii alisema tofauti na wasanii wenzake ambao wamekuwa wakitangaza nia ya kujitosa kwenye siasa kisha kuishia njiani yeye hatanii na kwamba uchaguzi ujao atakuwa miongoni mwa wanawake watakaowania ubunge jimboni.
"Sitanii na wala ‘simbeep’ mtu, nimenuia kabisa kujitosa kwenye mbio za uchaguzi wa 2015, nautaka ubunge wa Kilosa na ninaamini ninaweza nikipewa nafasi na chama changu cha CCM," alisema Dokii.
Dokii ambaye pia ni muimbaji muziki, alitangaza nia yake hiyo wiki mbili zilizopita, lakini baadhi ya mashabiki wake wanadhani ni kauli kama zilizowahi kutolewa na wasanii mbalimbali akiwamo JB, King Majuto, Steve Nyerere, Shilole na wengine lakini wasioaminika kama watajitosa kwenye uchaguzi huo.
Katika bunge la sasa linaloelekea ukingoni wapo wasanii kadhaa walitwaa viti vya ubunge akiwamo mmoja wa waasisi wa Bongofleva nchini, Joseph Mbilinyi 'Sugu' ambaye ni Mbunge wa Mbeya-Chadema, huku muimbaji Vick Kamata akiwa Mbunge-CCM Viti Maalum.

Marehemu Senzo Meyiwa atinga Tano Bora tuzo za CAF 2014

http://www.timeslive.co.za/sport/soccer/2014/10/27/senzo-meyiwa6/ALTERNATES/crop_630x400/Senzo+MeyiwaALIYEKUWA nahodha na kipa tegemeo wa timu ya taifa ya Afrika Kusini 'Bafana Bafana' na klabu ya Orlando Pirates, Senzo Meyiwa aliyeuwawa na majambazi mwezi uliopita ni miongoni mwa nyota waliotinga Tano Bora ya Tuzo ya Mwanasoka Bora Anayecheza Soka barani Afrika.
Kipa huyo aliyeuwawa kwa kupigwa risasi akiwa kwa hawara yake, ametangazwa katika orodha hiyo ya mwisho iliyotolewa na Shirikisho la Soka Afrika, CAF.
Wengine wanaochuana na marehemu huyo ni  Akram Djahnit, El Hedi Belamieri wote wa Algeria na E.S. Setif, Fakhreddine Ben Youssef wa Tunisia na C.S. Sfaxien na Firmin Mubele Ndombe wa DRC na AS Vita.

Yaya Toure aongoza orodha ya mwisho Mwanasoka Bora Afrika 2014

http://www.football-marketing.com/wp-content/uploads/2012/01/PUMA-Yaya-Toure.jpg
KIUNGO nyota wa Manchester City na timu ya taifa ya Ivory Coast, Yaya Toure ameongoza orodha ya wachezaji watano walioingia Fainali za kuwania Tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika 2014.
Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limetoa orodha ya mwisho ya wachezaji hao watano wanaowania tuzo hiyo ambayo awali ilikuwa na wachezaji 25.
Mtetezi wa tuzo hiyo anayetarajiwa kutwaa kwa marta ya nne anachuana na Wanigeria wawili, Mghana mmoja na Mgabon.
Orodha hiyo inaonyesha kuwa Toure anachuana na  Vincent Enyeama na Ahmed Musa wote wa Nigeria, Mghana Asamoah Gyan na Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon.
Toure alitwaa tuzo hiyo miaka mitatu iliyopita na kama akifanikiwa kuitwaa tena msimu huu, atakuwa amefikia rekodi ya Mcameroon Samuel Eto, ambaye ameitwaa mara nne.
Mshindi atatangazwa jijini Lagos, Nigeria Alhamis Januari 8, 2015

Kocha Manchester Utd akerwa ratiba kuelekea X-mass Mwaka Mpya

http://www.nerdoholic.com/wp-content/uploads/2014/07/Van-Gaalmoyes1.jpg
Kocha Luis Van Gaal
RATIBA ya Ligi Kuu na michuano mingine nchini England kuelekea Sikukuu ya Krismasi inaonyesha kumkera Kocha wa Manchester United, Louis Van Gaal.
KOcha huyo ameonyesha kutofurahishwa na ratiba ya Ligi Kuu itakavyokuwa katika kipindi cha sikukuu hiyo na ile ya Mwaka mpya.
Kuna uwezekano mkubwa United ikacheza mechi nne ndani ya siku tisa katika kipindi cha kati ya Desemba 29 mpaka Januari 3 kutegemeana na ratiba ya Kombe la FA itakavyokuwa. 
Ratiba katika Ligi Kuu inaonyesha kuwa watakuwa wenyeji wa Newcastle United Desemba 26, kabla ya kucheza wa ugenini dhidi ya tottenham Hotspurs siku mbili baadae na siku ya mwaka mpya watapepetana na Stoke City. 
Akihojiwa Van Gaal amesema ana mke, watoto na wajukuu na hawezi kuwaona katika kipindi cha krismasi lakini alitaka kufanya kazi katika Ligi Kuu hivyo anapaswa kuzoea hali iliyopo. 
Van Gaal amesema hafurahishwi na suala hilo lakini hawezi kubadilisha na hadhani kama ni jambo zuri kwa wachezaji pia.

Stars Maboresho yaingia kambini Bulyanhulu kuiwinda Burundi

https://silajilimbu.files.wordpress.com/2014/10/savedpicture-2014103164047.jpghttp://tff.or.tz/wp-content/uploads/2014/11/Star-U-23.jpgKIKOSI cha pili cha timu ya taifa, maarufu kama Taifa Stars Maboresho kimeingia kambini Bulyanhulu mkoani Shinyanga kujiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi itakayochezwa Desemba 9 mwaka huu jijini Dar es Salaam. Ikiwa chini ya Kocha Mart Nooij, Stars Maboresho itapiga kambi mkoani humo hadi Desemba 6 mwaka huu ambapo itarejea jijini Dar es Salaam tayari kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa Uwanja wa Taifa. Wachezaji walioingia kambini ni Abubakar Ally (Coastal Union), Abubakar Ally Mohamed (White Bird), Aishi Manula (Azam), Andrew Vicent (Mtibwa Sugar), Atupele Green (Kagera Sugar), Edward Charles (Yanga) na Emmanuel Semwanda (African Lyon).
Gadiel Michael (Azam), Hashim Magoma (Stand United), Hassan Banda (Simba), Hassan Mwasapili (Mbeya City), Joram Mgeveke (Simba), Kassim Mohamed Simbaulanga (African Lyon), Kelvin Friday (Azam) na Makarani Ally (Mtibwa Sugar).
Miraji Adam (Simba), Mohamed Hussein (Simba), Muzamir Ally (Mtibwa Sugar), Omari Nyenje (Ndanda), Pato Ngonyani (Yanga), Rashid Mandawa (Kagera Sugar), Said Hamisi (Simba), Salim Hassan Mbonde (Mtibwa Sugar) na Shiza Ramadhan (Mtibwa Sugar).
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linaishukuru kampuni ya kuchimba madini ya Acacia Mining PLC (zamani African Barrick Gold PLC) kwa kufadhili kambi ya Stars kupitia mgodi wa Bulyanhulu.

Yacine Brahimi ndiye Mwanasoka Bora wa Afrika wa BBC 2014

 
http://www2.pictures.zimbio.com/gi/Yacine+Brahimi+Algeria+v+Armenia+International+DPgMxDsahSgl.jpgNYOTA wa Algeria anayeichezea Porto ya Ureno, Yacine Brahimi ndiye mshindi wa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika 2014.
Brahimi alitangazwa kushinda tuzo hiyo iliyokuwa ikishikiliwa na Yaya Toure wa Manchester City jana.
Tuzo hizo uandaliwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza,BBC na Brahimi, 24, anakuwa mchezaji wa kwanza kutoka Algeria kushinda tuzo hiyo ambayo hupigiwa kura na mashabiki kutoka pande mbalimbali za bara la Afrika. 
Akihojiwa mara baada ya kukabidhiwa tuzo yake Brahimi amesema ni heshima kubwa kwake kushinda tuzo hiyo muhimu na anawashukuru watu wote nchini kwake na popote pale ambao walimpigia kura. 
Brahimi alikuwa akichuana na Yaya Toure na Gervinho kutoka Ivory Coast, Pierre-Emerick Aubameyang kutoka Gabon na Vincent Enyeama kutoka Nigeria.

Ronaldo, Messi, Neuer wapambanishwa Ballon d'Or 2014

 
SHIRIKISHO la Soka Duniani, FIFA limetangaza orodha ya wachezaji watatu watakaogombea tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Dunia, Ballon d’Or. Wachezaji hao waliopenya katika mchujo wa wachezaji 23 ni mtetezi wa tuzo hiyo nyota wa Ureno na klabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo, Lionel Messi wa Argentina na klabu ya Barcelona na Manuel Neuer wa Ujerumani na timu ya Bayern Munich. Sherehe za utoaji tuzo inatarajiwa kufanyika Januari 12 mwakani huku Ronaldo akiwa ndio mshindi wa mwaka jana. Kwa upande wa wanawake walioteuliwa kugombea tuzo hiyo ni pamoja na Nadine Kessler wa Ujerumani, Marta wa Brazil na Abby Wambach kutoka Marekani. Kwa upande wa makocha walioteuliwa kugombea tuzo ni pamoja na Carlo Ancelotti wa Real Madrid, Joachim Loew aliyeiwezesha Ujerumani kunyakuwa Kombe la Dunia na kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone.

Monday, December 1, 2014

Inter Milan yapigwa 4-2 na Roma, Gervinho atupia moja

http://www.iberita.com/wp-content/uploads/2014/11/Jadwal-Liga-Italia-2014-Terbaru-Pekan-Ini-30-November-dan-1-2-Desember-2014.jpg
AS Roma wakishangilia moja ya mabao yao yaliyoizamisha Inter Milan
KLABU ya Inter Milan usiku wa jana imeshindwa kufurukuta nyumbani kwa AS Roma baada ya kubanduliwa mabao 4-2 katika pambano kali la Ligi Kuu ya Italia, Serie A.
As Roma iliwakaribisha wapinzani wao kwa bao la dakika ya 21 kupitia kwa Gervinho kabla wa wageni hao kusawazisha kupitia kwa Ranocchia dakika ya 36.
WWEnyeji waliongeza bao la pili dakik achache baada ya kuanza kwa kipindi cha pili kupitia kwa Holebas kabla ya funga nikufunge kuendelea kwa Inter Milan kurejesha bao hilo kwa mkwaju wa Osvaldo dakika ya 57.
Magoli mawili ya Pjanic ya dakika ya 60 na 90 yaliisaidia wenyeji kuibuka na ushindi huo na kuendelea kuwafukuza Juventus waliopo kileleni wakitofautiana pointi tatu, Juve wakiwa na 34 na Roma 31 zote zikiwa zimecheza mechi 13kila moja.

Macho vya Vishal, Pingu videoni, audio njiani

Pingu na Vishali katika pozi

Vishali
BAADA ya kuachia video ya 'Macho' inayoendelea kutamba hewani, msanii Vishal Milanzi 'Vishal' yupo katika maandalizi ya kutengeneza kazi nyingine mpya atakayoanza kuirekodi mara baada ya kurusha hewani 'audio' ya wimbo huo wa Macho alioimba na mzoefu Pingu.
Akizungumza na MICHARAZO, Vishal alisema alitanguliza video hewani na wiki ijayo ndiyo ataachia 'audio' kabla ya kuanza mipango ya kurekodi kazi nyingine mapya akimshirikisha pia Pingu mmoja wa wasanii wa muda mrefu nchini anayetamba na nyimbo mbalimbali.
"Niliamua kutanguliza video hewani, kabla ya 'audio' yake na ninashukuru mashabiki wameikubali kazi na imenitia moyo wa kuanza kutengeneza kazi nyingine mpya. Kazi hizo zitafuata baada ya 'audio' ya 'Macho' kutoka," alisema Vishal.
Msanii huyo alidokeza kuwa wimbo huo atakaouachia hewani wiki ijayo umerekodiwa studio za Triple One Records kwa Kizo One na video yake imetengenezwa Rubby Videos na ‘Audio' na zitatengenezwa katika studio nyingine kwa lengo la kuipa vionjo tofauti.

Barcelona yaipumia Real Madrid, Messi apigwa

Otamendi falls to the floor in theatrical fashion, but Neymar had forcefully moved his head towards the Valencia man's jaw
Kulaaa! Neymar akimlamba kichwa beki wa Valencia aliyemchezea kitemi kabla
Players of both Valencia and Barcelona then got involved in a heated discussion after the incident
Mzozo baina ya wachezaji wa Valencia na Barcelona
Messi looks to get Barcelona on the attack during the second half of their clash with ValenciaKLABU ya Barcelona imezidi kuwapumulia wapinzani wao Real Madrid baada ya usiku wa jana kupata ushindi mwembamba ugenini dhidi ya Valencia huku nyota wake Lionel Messi akipigwa na chupa uwanjani.
Barcelona walioivaa Valencia katika uwanja wa Mestalla walipata ushindi huo kupitia bao la 'jioni' lililofungwa na Sergio Busquets dakika ya 90, kabla ya Lionel Messi kupigwa na chupa. Katika pambano hilo lilishuhudiwa undava ukitembezwa uwanjani kwatai Neymar alipompiga kichwa Nicolas Otamendi baada ya beki huyo kuanza kumcheza ‘kitemi’ Mbrazil huyo. Otamendi alimchezea kibabe Neymar kwenye eneo la hatari, lakini alipokwenda kumuinamia kumuomba msamaha, alilambwa kichwa ‘kishikaji’ kabla ya kuibuka mzozo uliohusisha wachezaji wote.
Hata hivyo Neymar hakuchukuliwa hatua zozote na refa wa pambano hilo, David Fernandez.
Ushindi huo umeifanya Barcelona kufikisha pointi 31, mbili nyuma ya Real Madrid wanaoongoza msimamo ambao walishinda mabao 2-1 ugenini siku ya Jumamosi dhidi ya Malaga.

Mkurugenzi Zugo Sports ahimiza wanawake kujifunza Martial Arts

Zuwena Idd Kipingu akionyesha umahiri kwa kunyanyua chuma katika gym yake
WANAWAKE na wasichana wamehimiza kujenga utamaduni ya kupenda kujifunza na kucheza michezo ya mapigano kwa lengo la kuwasaidia kuwaepusha na matukio la kudhalilishwa mitaani.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Klabu ya Michezo ya Zugo, Zuwena Idd Kipingu, alipozungumza na blogu hii na kudai ili kuepukana na kubakwa au kuporwa na unyanyasaji mwingine wasichana na wanawake wanapaswa kujifunza na kucheza michezo ya mapigano (Martial Arts).
Zuwena alisema michezo hiyo mbali na kuwaweka kuwa fiti pia itawasaidia kwa ulinzi wao binafsi pale wanapovamiwa au kukumbana na wahalifu mahali popote.
"Wanawake na wasichana wamekuwa wakifanyiwa uonevu na baadhi ya wanajamii kwa kuwaona ni wanyonge na legelege ni fursa yao kujifunza michezo kama ya karate, Judo, Kung-fu au ngumi ili kujiweka fiti na kukomesha unyanyasaji dhidi yao," alisema.
Mkurugenzi huyo ambaye pia ni Mwakilishi wa Wanawake, Maendeleo ya Vijana na Ajira kwa Wachezaji wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT) alisema klabu yake ipo tayari kuwapa mafunzo wanawake wanaohitaji kufanya hivyo.
"Klabu yangu ya Zugo Sports, inafundisha michezo mbalimbali, lakini wengi wao ni wanaume, nilidhani ni wakati wanawake na wasichana wakachangamka ili kujisaidia kwa mambo mengi."
Alisema mbali na kupata ulinzi binafsi katika matukio madogo madogo, lakini pia michezo itawafanya wawe na afya njema pamoja na kujitengenezea mazingira mazuri ya ajira.
Mwanadada huyo mwenye mkanda mweusi katika mchezo wa Taekwondo na aliyewahi kung'ara kwenye michezo ya kunyanyua vitu vizito na ngumi, alisema wanawake wasijiweke nyuma.
"Wasijiweke nyuma au kutishwa na madai kwamba ukicheza michezo kama hiyo hataweza kuzaa, huo ni uongo mimi nimeanza michezo hii mwaka 1980 na nina watoto saba kwa sasa," alisema.
Aliongeza kuwa, michezo ni afya, hivyo ni wajibu hata kwa wazazi kuwazoesha watoto wao kuicheza ili kuiweka miili yao salama na kuepukana na maradhi madogo madogo.

Sunday, November 30, 2014

Juventus yazidi kujichumbia kileleni Italia

Juventus celebrateAndrea PirloMABINGWA watetezi wa Serie A ya nchini Italia, Juventus, imezidi kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo baada ya usiku huu kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wapinzani wao wa jadi Torino.
Katika pambano hilo lililochezwa kwenye mjini wa Turin, wenyeji walijikuta wakimaliza mchezo huo wakiwa pungufu baada ya beki waoStephan Lichtsteiner kulimwa kadi nyekundu kutokana na kupewa kadi ya pili ya njano.
Wenyeji hao walitangulia kuandika bao mapema kupitia kwa Arturo Vidal kwa mkwaju wa penati iliyotolewa na mwamuzi dakika ya 15 kabla ya wageni wao kurejesha bao hilo dakika saba baadae kupitia kwa Bruno Peres.
Wakati wengi wakidhani matokeo yangeisha kwa sare ya 1-1, kiungo mkongwe  Andrea Pirlo aliifungia Juventus bao muhimu la ushindi dakika za lala salama na kuifanya 'Kibibi' cha Turin, kufikisha jumla ya pointi 34 kutokana na michezo 13.
MUda mchache ujao wanaoshikilia nafasi ya pili AS Roma wenye pointi 28 watakuwa nyumbani kuwakaribisha Inter Milan katika pambano linalotarajiwa kuwa kali.

UWAJIBIKAJI! Polisi aliyeua kijana mweusi ajiuzulu!

Daren Wilson Afisa wa polisi aliyempiga risasi na kumuua kijana mweusi nchini Marekani amejiuzulu. Wakili wa Darren Wilson ambaye ni afisa wa polisi aliyempiga risasi na kumuua kijana mweusi Michael Brown kwenye eneo la st Louis nchini Marekani mwezi Agosti anasema kuwa polisi huyo amejiuzulu.
Mapema wiki hii bwana Wilson aliondolewa mashtaka hatua iliyozua ghadhabu miongoni mwa waamerika weusi.Afisa huyo amekuwa likizoni tangu mauji hayo yafanyike, mauaji ambayo yalisababisha majuma kadha ya maandamano. 
Michael Brown,kijana mweusi nchini Marekani alipigwa risasi na kuuawa. Gazeti la St Louis limesema kuwa afisa huyo mwenye miaka 28 aliamua kujiuzulu baada ya kitengo chake cha polisi kupokea vitisho kwamba ghasia zitafutia iwapo ataendelea kuhudumu kama mfanyikazi.

Gazeti hilo lilichapisha kile lilichodai kuwa barua yake ya kujiuzulu ambayo ilisoma:''nimearifiwa kwamba iwapo nitaendelea kuwa mfanyikazi wa idara ya Polisi basi hatua hiyo itawachochea maafisa wa polisi na raia wa eneo la Furguson kuishi kwa hofu,hali ambayo siwezi kuikubali hata kidogo.''

Spurs yainyoa Everton mabao 2-1

Roberto Soldado
Roberto Soldado scores for SpursTIMU ya Tottenham Hotspur imetakata nyumbani baada ya kuinyoa Everton kwa mabao 2-1 katika pambano kali la Ligi Kuu ya England lililomalizika hivi punde.
Spurs iliyokuwa uwanja wa White Hartlane, ilishtushwa na wenyeji waliotangulia kuandika bao dakika ya 15 kupitia Kevin Mirallas kabla ya Christian Eriksen kusawazisha dakika ya 21 na Saldado aliongeza bao la pili dakika za nyongeza kabla ya mapumziko.
Kwa ushindi huo imeifanya Spurs kufikisha jumla ya pointi 20 sawa na wapinzani wao Arsenal isipokuwa wanakamata nafasi ya saba kwa tofauti na uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena siku ya Jumanne kwa mechi sita ambapo Burnley itaikaribisha Newcastle United, Leicester itaialika Liverpool, huku Manchester United ikiikaribisha Stoke City na Swansea City ikiumna ana QPR, wakati Crystal Palace itaumana na Aston Villa na West Brom itapepetana na West Ham.
Jumatano kutapigwa mechi nne, Arsenal dhidi ya Southampton, Chelsea itailika Spurs, Everton itapepetana na Hull City na Sunderland itaialika watetezi Manchester City.

AC Milan yaifumua Udinese, Essien alimwa nyekundu

B3sxrK5IUAAcGQY Michael Essiens epic reaction to sending off during AC Milan v Udinese [video]
Michael Essien akiwa haamini kama kalimwa kadi nyekundu baada ya kupewa kadi ya pili ya njano
Italy Soccer Serie A
Jeremy Menez akifunga bao la Ac Milan
 MABAO mawili yaliyowekwa kimiani na Jeremy Menez, moja likiwa na mkwaju wa penati yametosha kuipa ushindi timu ya AC Milan katika pambano la Ligi Kuu ya Italia 'Serie A' dhidi ya Udinese.
Milan ikiwa nyumbani hata hivyo kama ilivyokuwa kwa wageni wao, walijikuta wakipoteza mchezaji mmoja baadaya Michael Essien kulimwa kadi mbili za njano, dakika chache tangu Udinese wampoteze Domizzi kwa rafu aliyomchezea Kaisuyke Honda na kusababisha penati ilifungwa na Menez katika dakika ya 65.
Menez aliongeza bao la pili dakikia 10 baadaye akimalizia kazi nzuri ya Boneventura na kuifanya AC Milan kukwea hadi nafasi ya tano ikiwa na pointi 21.
Katika mechi nyingine zilizochezwa leo, Cagliari ikiwa nyumbani ilijikuta ikifumuliwa mabao 4-0 na Fiorentina nayo Cesena pia ililala nyumbani kwa mabao 3-0 na genoa huku Empoli na Atalanta zilitoshana nguvu kwa kutofungana na Palermo ikitakata nyumbani kwa kushinda mabao 2-1 dhidi ya Parma na hivi sasa watetezi Juventus wapo nyumbani ikiumana na Torino na mpaka sasa ikiwa ni mapumziko matokeo ni 1-1.

Shabiki afa, Atletico Madrid ikiilaza Deportivo la Coruna

arda
SHABIKI mmoja wa soka amefariki dunia huko nchini Hispania kufuatia vurugu zilizotokea muda mfupi kabla ya mchezo kati ya Atletico Madrid na Deportivo La Coruna .
Mtu huyo mwenye umri wa miaka 43 alifariki dunia baada ya kupata shinikizo la damu wakati akiwa miongoni mwa watu waliokuwa katikati ya vurugu zilizotokea kati ya mashabiki wa timu zote mbili.
Awali uongozi wa ligi ya Hispania ulijaribu kuahirisha mchezo huo lakini jaribio la kufanya hivyo lilizuiliwa na Shirikisho la soka la Hispania .
Picha ikiwaonyesha mashabiki wa Deportivo na Atletico madrid wakifanyiana vurugu saa chache kabla ya mchezo baina ya timu hizo mbili .
Picha ikiwaonyesha mashabiki wa Deportivo na Atletico madrid wakifanyiana vurugu saa chache kabla ya mchezo baina ya timu hizo mbili .
Vurugu kati ya mashabiki zilitokea saa tatu kabla ya mchezo kuanza ambapo mashabiki kadhaa waliumia wakiwemo watu 10 ambao walipata majeraha yaliyohitaji kuwahishwa hospitalini .
Viongozi wa juu wa klabu zote 20 za ligi kuu ya Hispania wametoa tamko la kukemea vurugu zilizotokea baina ya mashabiki wa Deportive na Atletico Madrid nab ado haiajfahamika kama kuna hatua zozote zitakazochukuliwa kwa timu hizo kufuatia vurugu zilizotokea .
Mchezo huo uliendelea kama kawaida ambapo Atletico Madrid walishinda 2-0 baada ya mabao yaliyofungwa na Saul Nigez na Arda Turan.
Katika mechi nyingine Sevilla ikiwa nyumbani iliikwangua Granada kwa mabao 5-1 kwa sasa timu za
Cordoba na Villarreal zipo dimbani na baadae Valencia itaikaribisha Barcelona.

Kaka 'amchana' Emmanuel Adebayor kumtuhumu mama yake kumroga

ade n mum
Sakata linaloendela kati ya mshambuliaji star wa Totenham Emmanuel Adebayor  na mama yake mzazi anayefahamika kama Alice Adebayor limechukua sura nyingine baada ya ndugu wa mshambuliaji huyo kuingilia kati .
Ndugu huyo  anayeitwa Kola Adebayor ambaye ni kaka wa Emmanuel amesema kuwa madai ya mshambuliaji huyo ya kusema kuwa mama yao mzazi amemroga si ya  kweli.
Kola amesema kuwa kinachomfanya Adebayor kuamini kuwa mama yake amemfanyizia kwa waganga ili asiwe na bahati ni mawazo anayoyapata toka kwa watu wenye Imani ya dini ya kiislamu ambao wanamshauri vibaya nyota huyo .
Kola mwenye umri wa miaka 42 ambaye kazi ni dereva wa Malorry huko Ujerumani amesema kuwa amekerwa sana na kitendo cha mshambuliaji huyo kumuita mama yao mzazi mchawi kwani inaonyesha jinsi gani alivyokosa heshima kwa mzazi wake .
ade
Kwa mujibu wa Kola , Adebayor aliwafuata watu wanaojiita watakatishaji wa nafasi ambao kwa lugha ya kiingereza huitwa Spiritual Cleansers ili wamsaidie kwa sababu mambo yake hayaendi vizuri na kwa mshangao mkubwa watu hao walimwambia kuwa mama yake mzazi na dada yake ndio chanzo cha mikosi inayompata .
Kola anaendelea kusema kuwa Adebayor alifuata ushauri wa watu hawa na kuwafukuza dada na mama yake kwenye nyumba aliyojenga huko Afrika na tangu siku hiyo amegoma kuwatumia fedha za kujikimu .
Kwa upande mwingine dada wa Emmanuel Adebayor anayeitwa Maggie ndio aliyefichua sakata hili huko Ghana wakati akizungumza moja kwa moja kwenye kipindi cha radio ambapo alisema kuwa mchezaji huyo amemfukuza mama yake na ametelekeza tangu siku hiyo .
Kola Adebayor anadai kuwa mama yao mzazi tangu siku aliyofukuzwa hadi leo hii amekuwa akilia kila siku hali ambayo inahatarisha afya yake .
Mshambuliaji huyo amekanusha sakata hilo akisema kuwa sio kweli kuwa amemfukuza mama yake bali mama huyo ameamua kuondoka yeye mwenyewe , Adebayor ameongeza kuwa hayuko kwenye mawasiliano mazuri na mama yake kwani amekuwa akisambaza maneno kwa watu kuwa mambo hayatamwendea vizuri .

Man City yaipiga Southampton 3-0

Toure skips past the challenge of Southampton midfielder Victor Wanyama in the first half at St Mary's
Yaya Toure akichuana na mchezaji wa Southampton
Midfielder Lampard celebrates his fifth goal for the club with Aguero, after a typical finish from the edge of the box
Wachezaji wa City wakishangilia moja ya mabao yao lililofungwa na Lampard
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya England, Manchester City jioni ya leo imepata ushindi mnono wa mabao 3-0 ugenini dhidi ya 'wagumu' Southampton na kukwea hadi katika nafasi ya pili.
City, hata hivyo ilimaliza pambano hilo ikiwa pungufu kufuatia beki wake Eliaquim Mangala kulimwa kadi nyekundu baada ya kulimwa kadi mbili za njano.
Wageni walianza kuhesabu mabao yake katika dakika ya 51 baada ya kiungo Yaya Toure kuandika bao akimaliza kazi nzuri ya Sergio kun Aguero.
Bao la pili la City liliwekwa kimiania na mkongwe Frank Lampard dakiia ya 80 kabla ya dakika nane baadaye Gael Clichy kumaliza udhia kwa kuandika bao la tatu.
Ushindi huo umeifanya City kupanda hadi nafasi ya pili ikiwa na pointi 27, nane nyuma ya vinara Chelsea na wakiiporomosha Southampton waliokuwa wameng'ang'ania nafasi hiyo kwa muda mrefu ikiwa na pointi zake 26.
City itasafiri siku ya Jumanne kuifuata Sunderland ambayo jana iliikomaliza Chelsea na kutoka nao suluhu.
Ligi hiyo inaendelea tena muda huu kwa pambano jingine linalopigwa Uwanja wa White Hartlane kwa wenyeji Tottenham Hotspur wakiwa mbele kwa mabao 2-1 dhidi ya wageni wao Everton.

Diamond aweka historia tuzo za Channel O

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhIVUPj90sCe-xi1lGAmtEnUNWcQ20yj9jfRJVF30cfL1-o_qdrHJJEzLI-eDQqTYBZcfEDA6anCwlETFgQsVU0zLUJWC-PP5P8llZAXFy7SdINX7cQvnbDK6bttBVHRGCI6hb4dmHZNys/?imgmax=800
MSANII nyota wa muziki wa kizzi kipya nchini, Nassib Abdul 'Diamond Platnumz' juzi Jumamosi aliweka historia baada ya kufanikiwa kunyakua tuzo tatu za 'Channel O Music Video Awards' (CHOMVA-2014).
Diamond mshindi wa kihistoria wa tuzo za Kili Music Awards 2014 baada ya kunyaku tuzo saba kwa mpigo aliweka rekodi hiyo kwenye ukumbi wa  Nasrec Expo Centre, nchini Afrika Kusini zilipotolewa tuzo hizo.
Staa huyo wa 'Nitampata Wapi', 'Mdogomdogo' na 'My Number One', alishinda tuzo tatu kati ya nne alizokuwa akiziwinda katika vipengele vya  Most Gifted East, Most Gifted Afro Pop na Most Gifted Newcomer.
Hii tuzo ya tatu ya kimataifa kwa Diamond kwa mwaka huu baada ya awali kunyakua tuzo ya AFRIMMA na Kora Music (ambayo hata hivyo mpaka sasa imekuwa na na utata).
Orodha kamili ya washindi wa tuzo hizo za Channel O ni kama ifuatavyo;
Most Gifted R&B video ni Crazy but Amazing-Donald, Most Gifted West Video
ni ‘Turn Up-Olamidem, Most Gifted Ragga/Dancehall ni Buffalo Soulja na The Most Gifted Kwaito akiwa ni  Uhuru ft Oskido & Professor Kalawa -tjukutja.
Tuzo nyingi kama za Most Gifted East Video ni Diamond Platnumz, Most Gifted Dance Video ni Busiswa-Ngoku, Most Gifted Hip Hop Video ni AKA- Congratulate, Most Gifted Newcomer akiwa ni Diamond Platnumz tena.
Katika kipengele cha Most Gifted Male Video mshindi ni Casper Nyovest-Doc Shebeleza, Most Gifted Female Video alikuwa Tiwa Savage-Eminado, Most Gifted Afro Pop Video ni Mtanzania Diamond Platnumz, Most Gifted duo/group/featurning ni KCEE ft Wizkid-Pull Over na Most Gifted Video of the Year alikuwa ni Carsper  Nyovest- Dos Shebeleza.